DC Kihongosi ambana Mbunge Gambo "usitetee hoja inayovunja sheria"

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Kenan Kihongosi amekataa hoja ya Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo aliyotaka waendesha Bajaj na pikipiki waruhusiwa kupakia abiria hadi wanne na kumtaka Mbunge huyo kuzingatia Sheria za usalama barabarani.

Kihongosi alidai kwamba hoja hiyo inakiuka Sheria za usalama barabarani na Mbunge huyo hapaswi kutetea hoja ambayo anajua inavunja Sheria na kuhatarisha usalama wa raia huku akiwataka waendesha Bajaj kufuata Sheria.

"Hoja ya Mbunge tumeielewa na tunamheshimu Sana, lakini afuate Sheria za nchi hatuwezi kuruhusu hoja ambayo inahatarisha usalama wa raia yatakapotokea maafa ataulizwa nani bila Shaka ni jeshi la polisi"Alisema

Aidha amewaonya waendesha bodaboda hususani wanaochezea ekzosti na kuzifanya zitoe mlio mkubwa unashtua wananchi,kwamba watachukuliwa hatua Kali za kisheria huku akiliagiza jeshi la polisi kuhakikisha linasimamia Sheria kudhibiti vitendo hivyo.

Awali Gambo akiongea kwenye mkutano wa waendesha Bajaj na pikipiki jijini Arusha ulioitishwa na jeshi la polisi kwa lengo la kuwakumbusha Sheria za usalama barabarani na kusikiliza kero zao, aliomba waendesha Bajaj waruhusiwa kupakia abiria wanne kinyume Cha Sheria Jambo ambalo lilipingwa vikali na mkuu hiyo wa wilaya.

Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,Salumu Hamduni alisema hivi karibuni kumeibuka matukio ya uhalifu wa kutumia bodaboda katika kutekeleza uhalifu, ndio maana tumeitisha kikao hiki ili kuzungumzia changamoto zinazojitokeza.

"Zipo changamoto zinazohusiana na usalama barabarani ila changamoto kubwa ni uhalifu wa kutumia bodaboda ninachowaasa waache Mara moja tutawashughulikia "alisema Hamduni

Kamanda Hamduni akiwataka waendesha Bajaj au pikipiki wanaoshiriki matukio ya uhalifu kuacha Mara moja kwani jeshi la polisi lipo macho na watashughulikiwa kwa mujibu wa Sheria.

Ends
 
Ndio ujue wanafiki Ni wengi, hiyo hoja kwa Nini wakati Ni RC hakuruhusu ifanyike
 
Hao madereva boda wanaochezea sijui ekzost wachukuliwe hatua maana ni kero na usumbufu mkubwa kwa raia
 
Back
Top Bottom