DC Kasesela: Nimezuia dhamana ya mtuhumiwa wa ubakaji na ulawiti watoto kwa sababu kwanza simpendi halafu pili wananchi wana hasira wangemuua

jd41

JF-Expert Member
Aug 23, 2015
3,756
4,842
Wanabodi Salaam.

Hiyo hapo juu ni kauli iliyotolewa na Mkuu wa wilaya ya Iringa alipoulizwa na mwananchi kuhusu tukio la kukamatwa kwa mtuhumiwa wa ubakaji.

Ninajiuliza, kama humpendi sasa tena mbona unamlinda kwa kuzuia hao wananchi wenye hasira kali wasimuue? Kwa hiyo humpendi ila bado unamuhifadhi sio?

Wanabodi, kisheria inajulikana wazi, kuna sababu kadhaa za kumnyima mtu dhamana, ikiwemo hiyo ya kumlinda kwa usalama wake kama wananchi wana hasira nae, lakini hiyo sababu ya kusema humpendi sijawahi kuiona wala kuisikia popote kwenye nchi yetu hii.

Ni vyema viongozi waliopewa madaraka wakajizuia kutoa kauli zenye ukakasi kama hizi, kwa sababu kwanza mahakama bado haijatoa maamuzi kuhusu mtuhumiwa, na pili, kauli yake ya simpendi inaweza ku-influence maamuzi ya mahakama, hivyo ni vyema haki za mtuhumiwa zikalindwa mpaka mahakama itakapoamua.

Muwe na Jumapili Njema!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Mbakaji:
"Simpendi lakini Namlinda"
2.Mbakaji :
"Nampenda lakini Simlimdi"
3. Mbakaji:
"Nampenda na Namlinda"
4. Mbakaji:
"Sipendi na Simlimdi"
Haya maneno manne wewe uko wapi?
 
1. Mbakaji:
"Simpendi lakini Namlinda"
2.Mbakaji :
"Nampenda lakini Simlimdi"
3. Mbakaji:
"Nampenda na Namlinda"
4. Mbakaji:
"Sipendi na Simlimdi"
Haya maneno manne wewe uko wapi?
1. Siwezi chukia mtu halafu nimlinde, huo ni Unafiki!.
2. Kama unampenda lazima umlinde, ndio nature ilivyo.
3. Yes, correct; nampenda na kumlinda, mpaka mahakama itakapoamua vinginevyo!.
4. Siwezi chukia mtu kwa hisia//maneno ya wengine, nitabaki neutral mpk nitakapoujua ukweli; baada ya mahakama kuamua!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom