DC Kasesela: Napendekeza kuwa 10% ya michango ya harusi na vyakula vinavyobaki wapewe watu wasiojiweza

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,745
139,516
Mkuu wa wilaya ya Iringa mjini mh Kasesela amependekeza kuwa asilimia 10 ya michango ya harusi iwe inawekwa pembeni maalum kuwasaidia wasio na uwezo.
Kadhalika chakula kitakachobaki kwenye bufee kiwe kinapelekwa kwa watu wenye uhitaji kwani haipendezi kutupa chakula wakati wengine wana njaa.

DC Kasesela aliyasema hayo alipowatembelea watu wenye shida mbali mbali katika kitongoji cha Kihesa manispaa ya Iringa.

Source ITV
 
agree 101%.
for once ametoa pointi ya maana!
 
Mwalimu mmoja alitufundisha juu ya utopian socialists, na hapo ndipo utamjua mtawala au kiongozi ni yupi!
Kuongoza kwa mfano ni kutoa 10% ya mshara wako na kuwasaidia hao wahusika then utaona jinsi watu watakavyofuata kwa kuchangia pia.
Vision sahihi ya kuondoa matatizo haya ni kulipa kodi, na zoezi la kodi daima linafanikiwa pale mkusanyaji na mlipaji wanapokuwa na mtazamo wa pamoja kivitendo na kifikra.
 
Wazo la kipumbavu hilo.

Aanze kwana kuishauri serikali kwa sababu ndio inayotengeneza hao wasiojiweza.

Imagine deni la Heslib tu.

Sijaongelea ajira za waalimu hasawa arts ambao wengi wao wametokea familia Maskini.
 
Mkuu wa wilaya ya Iringa mjini mh Kasesela amependekeza kuwa asilimia 10 ya michango ya harusi iwe inawekwa pembeni maalum kuwasaidia wasio na uwezo.
Kadhalika chakula kitakachobaki kwenye bufee kiwe kinapelekwa kwa watu wenye uhitaji kwani haipendezi kutupa chakula wakati wengine wana njaa.
DC Kasesela aliyasema hayo alipowatembelea watu wenye shida mbali mbali katika kitongoji cha Kihesa manispaa ya Iringa.
Source ITV
Kwahiyo DC atakuwa akipita kwenye harusi kukusanya makombo na kuwapa wasiojiweza! Dharau.
 
Yaani amuagize Mchungaji Peter Msigwa asimamie hilo zoezi! Kasesela hana ubavu wa kumpelekesha mtu ambaye mkuu wake wa Mkoa mwenyewe anamgwaya! Kile kichwa kiko vizuri sana kwenye kujenga hoja. Na hilo wazo pia ni la hovyo tu.
Hahahaa....... Mchungaji Msigwa atapata fursa ya kuhudhuria kila mnuso!
 
Kina nani wanatupa chakula harusini..., au anamaanisha makombo ndio wapewe wasiojiweza..., na hizo food poisoning watakazopata wakati hawana hata BIMA ???

Pili Harusi siku hizi kuna mpishi keshapima kabisa plates ngapi kwa watu wangapi.., zikipungua yupo radhi afiche ili apeleke akale na wafanyakazi wake.., hapo bado wanakamati hawajafanya uroho wao..., By the way hata hao wenye harusi sio kwamba wanajiweza bali watu wanachanga ili waende outing na kula kile walichochanga to the fullest
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom