DC Kasesela: Napendekeza kuwa 10% ya michango ya harusi na vyakula vinavyobaki wapewe watu wasiojiweza

huyu mwehu anajoha jinsi arusi zinavyopangwa!kila kitu calculated hakunaga kusaza vikibaki havitupwi ni take away yooo!
 
Ni bora mtu akupe msosi hata kama kwa dharau kuliko ushibe mwingine analala njaa......

Utaunda chombo na watu hawatochangia, ni bora hilo wazo la kasesela sio baya....
Kwanini vyakula vilivyo baki ndio wapewe hiyo dharau na kupewa asilimia 10 nayo sio sawa kiundwe chombo cha kuwa saidia hawa na kutatua changamoto zao
 
Swala si usimamizi ila ni kwanini wasiojiweza walishwe makombo ya harusini? Kwanini asiwanunulie chakula kisafi?
Sidhani kama kwenye harusi wanakula chakula kisicho safi, kinaweza kutengwa/kupakuliwa maalum kwa ajili yao kama ilivyo kwa wahudhuria sherehe ya harusi.
 
Mkuu wa wilaya ya Iringa mjini mh Kasesela amependekeza kuwa asilimia 10 ya michango ya harusi iwe inawekwa pembeni maalum kuwasaidia wasio na uwezo.
Kadhalika chakula kitakachobaki kwenye bufee kiwe kinapelekwa kwa watu wenye uhitaji kwani haipendezi kutupa chakula wakati wengine wana njaa.

DC Kasesela aliyasema hayo alipowatembelea watu wenye shida mbali mbali katika kitongoji cha Kihesa manispaa ya Iringa.

Source ITV
Kwanini asitoe kwenye mshahara wake? Watu wachangie kufanikisha sherehe husika wewe uwapangie matumizi!!
 
Sidhani kama kwenye harusi wanakula chakula kisicho safi, kinaweza kutengwa/kupakuliwa maalum kwa ajili yao kama ilivyo kwa wahudhuria sherehe ya harusi.
Kwahiyo kabla ya wahusika kula mnapakua chakula cha wasiojiweza tuseme sitini mnawapelekea kwenye sahani zenu usiku huo wakishakula mnabeba sahani ili sasa wahusika mle kilichobakia! Fikiri kabla ya kuandika, bora ungesema kila harusi ikaribishe wasiojiweza 30! Pamoja na familia zao ni 30×4=120 yaani baba, mama na watoto wawili! Tanzania tunaviongozi wa ajabu sana, wengine wanakataza tusinyonye maziwa ya wake zetu!
Namshauri kila familia inapotaka kula itenge chakula mbele ya nyumba yako ili wasiojiweza nao wapate mlo kama ilivyokuwa Ramadan miaka ya hamsini, pia dhifa za taifa nazo zichukue wasiojiweza miambili.
 
Ni bora mtu akupe msosi hata kama kwa dharau kuliko ushibe mwingine analala njaa......
Utaunda chombo na watu hawatochangia, ni bora hilo wazo la kasesela sio baya....
Nijulishe unapoishi ili mimi na familia yangu tuwe tunakuja kula hata kama utatusimanga tuko radhi kuvumilia.
Natanguliza shukurani toka familia yangu.
 
Mwalimu mmoja alitufundisha juu ya utopian socialists, na hapo ndipo utamjua mtawala au kiongozi ni yupi!
Kuongoza kwa mfano ni kutoa 10% ya mshara wako na kuwasaidia hao wahusika then utaona jinsi watu watakavyofuata kwa kuchangia pia.
This is 100% Sure; Watu wengi wanatumia Muda mwingi sana kuwafundisha watu kwa maneno; Ila Mtu anaelewa zaidi kwa Vitendo.
Hapo ndipo hata watu wa Ulaya waliopotupiga gap; Elimu za Huko Tz nyingi ni za Nadharia, wakati ulaya ni vitendo zaidi.
 
Maana yake yeye kama DC ameshindwa kabisa kuhamasisha jamii anayoingoza kuwachangia wasiojiweza, total failure as leader... Mfano ameshawahi kwenye vikao vyake kusema mwezi huu mshahara wangu nikatwe 20 % upelekwe nyumba za wazee na kuomba wengine wamuunge mkono??
 
Mwalimu mmoja alitufundisha juu ya utopian socialists, na hapo ndipo utamjua mtawala au kiongozi ni yupi!
Kuongoza kwa mfano ni kutoa 10% ya mshara wako na kuwasaidia hao wahusika then utaona jinsi watu watakavyofuata kwa kuchangia pia.
Vision sahihi ya kuondoa matatizo haya ni kulipa kodi, na zoezi la kodi daima linafanikiwa pale mkusanyaji na mlipaji wanapokuwa na mtazamo wa pamoja kivitendo na kifikra.
Utopian social ism = ujamaa wa njozi
 
Mkuu wa wilaya ya Iringa mjini mh Kasesela amependekeza kuwa asilimia 10 ya michango ya harusi iwe inawekwa pembeni maalum kuwasaidia wasio na uwezo.
Kadhalika chakula kitakachobaki kwenye bufee kiwe kinapelekwa kwa watu wenye uhitaji kwani haipendezi kutupa chakula wakati wengine wana njaa.

DC Kasesela aliyasema hayo alipowatembelea watu wenye shida mbali mbali katika kitongoji cha Kihesa manispaa ya Iringa.

Source ITV

Wakipewa 10% watakuwa wanajiweza
 
Back
Top Bottom