DC Kakonko amsimamisha kazi Mwenyekiti wa Kijiji cha Kakonko kwasababu hajahudhuria mkutano wake

Mar 3, 2018
75
799
Kanali Hosea Ndagala,Mkuu wa Wilaya ya Kakonko leo jioni ameamua kujifurahisha Mbele ya Wananchi eti anamsimamisha Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Kakonko na Mwenyekiti wa vijana BAVICHA Wilaya ya Kakonko kwa kile alichokieleza kwamba hajahudhuria mkutano wake.

Kabla ya mkutano Mkuu wa Wilaya alielezwa kuwa Mwenyekiti huyo yupo kuanua Matanga ya Kaka yake ambae alifariki Wiki iliyopita na Matanga yalikua ni leo tar 11/02/2019.

Kabla ya hapo Bwana Fanuel Nzenda aliwafungulia kesi wajumbe wa serikali ya kijiji cha Kakonko Katika Mahakama kuu masjala ndogo ya Tabora kwa kitendo cja kumchafua ambayo mpaka sasa inaendelea.

Ninasema Mkuu huyu wa Wilaya amejifurahisha kwasababu ameamua kumleta Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbizi kumfungulia mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Kakonko.
Ni kweli kwamba hiki kitu kwa taratibu na sheria hakipo na hakitakaa kitokee mwenyekiti wa kijiji kimoja kuwa na hadhi sawa kwenye kijiji kingine.

Yaani Diwani wa Kakonko apewe nafasi ya kuwa diwani wa Gwarama huku mimi nikiwa natembea?

Hii ni akili ya asie jua utaratibu wa serikali za mitaa.
Nimemzuia asikabidhi muhuri,ili tumuonyeshe huyu Mkuu wa Wilaya kwamba sisi ni wagumu zaidi ya Chuma cha Mjerumani.

Tumesubiri barua ya kumsimamisha tuone maamlaka hayo katoa wapi,naona Ameshatamani Ukuu wa Mkoa maana anajua Boss wao anataka hivyo.

Ndagala kaa vizuri uyanywe maji uliyo yachemsha mwenyewe.

Kwanza hasimami mtu,kama mnamuogopa Mwenyekiti huyu tafuteni wagombea wazuri na sio kwa utaratibu huo.

Kwanini mteseke?
Uchaguzi ni mwaka huu mnasutwa nini,tulieni hapo mlipo.

Nyie ni wanajeshi sisi sheria ni kama maji ya kunywa.

Hongera kwa kujifurahisha Bwana Ndagala,mimi nilikua nakuheshimu ila kwa hii akili unafaa kuitwa mdogo wangu.

Elia F Michael.
Diwani Gwarama.
Mbunge nje ya Bunge.
11/02/2019.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huoni aibu kwa ulichoandika? Huyo DC hajui taratibu za uongozi... Kama mwenyekiti wa kijiji hayupo anayekaimu nafasi yake ili kuongoza mkutano ni mwenyekiti wa kitongoji atakayekuwepo. Huwezi kuchukua mwenyekiti wa kijiji jirani, na kama angekutana na wananchi wanaojua wangesusia mkutano huo. Halafu DC hana mamlaka ya kumuondoa mwenyekiti wa kijiji, wenye mamlaka hayo ni wananchi wenyewe au labda apatikane na hatia afungwe jela.
tangu ushindwe ubunge umekuwa kasuku wa vijihabari vya kipuuzi.endelea kula miwa dogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kanali Hosea Ndagala,Mkuu wa Wilaya ya Kakonko leo jioni ameamua kujifurahisha Mbele ya Wananchi eti anamsimamisha Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Kakonko na Mwenyekiti wa vijana BAVICHA Wilaya ya Kakonko kwa kile alichokieleza kwamba hajahudhuria mkutano wake.

Ipo siku watatukana mawe baada ya kukosa wa kuwasemesha
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom