DC Jokate Mwegelo aweka mkakati wa kuboresha elimu na ufaulu Wilayani Temeke

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
DC JOKATE MWEGELO AWEKA MKAKATI WA KUBORESHA ELIMU NA UFAULU WILAYANI TEMEKE

Leo hii Mkuu wa Wilaya Mh. Jokate Mwegelo amefanya kikao maalumu cha wataalamu wa elimu wakiwamo viongozi na kutoka Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), wasimamizi na maafisa Elimu ya Temeke. Dhima ya kikao hicho ni kuweka mkakati wa kuboresha elimu na ufaulu wa wanafunzi katika wilaya ya Temeke.

Akifafanua katika kikao hicho Dr. Mabula Nkuba amesema suala la utoro limechangia sana katika kushusha kiwango cha elimu nchini. Amefafanua kuwa ili kupambana na hilo DUCE walivumbua mradi uitwao Digitalizing Our Schools for Success (DOSS). Mradi huu unalenga kutatua tatizo la ukosefu wa mawasiliano kati wazazi, walimu na wanafunzi. Pia utasaidia kupunguza idadi ya wanafunzi ambazo wanaoacha shule bila sababu za msingi.

Naye, Naibu Mkuu wa Chuo (Utawala), Dr. Method Samwel ameishukuru Wizara ya Elimu, Sayansi na teknolojia kwa kuleta mradi wa Higher Education for Economic Transformation (HEET). Huu ni mradi wa miaka mitano (2021/22- 2025/26) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia wizara husika. Mradi huu utasaidia Vyuo vikuu teule vya serikali katika kukarabati na kujenga majengo mapya, kuboresha mitaala, kununua vifaa vya TEHAMA, mafunzo kuhusu jinsia na kuwasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Akichangia katika kikao hicho, Naibu Mkuu wa Chuo (taaluma), Dr. Christina Raphael amesema ufaalu wa somo la Hisabati na masomo ya Sayansi unahitaji mikakati maalumu ikiwa na pamoja na kufunza masomo hayo kwa kuzingatia mtaala uliojikita katika umahiri, yaani Competence based Curriculum.


#temeketukutaneshuleni
#kaziiendelee🇹🇿

Screenshot_20220118-142208.jpg
 
Hesabu mwaka huu ufaulu upo chini ya 20%

Hizi mbinu zinazotumika ni rahisi mno kutatua tatizo

Mimi mtu angeniuliza ningemjibu kuwa lazima motisha ya kusoma na kujifunza hesabu uanzie chini

Walimu wa hesabu ni wachache sana na HAKUNA motisha yoyote ya kusoma hilo somo
 
Back
Top Bottom