DC Jerry Muro: Watendaji wa vijiji wanamsubiri DC atoke ofisini akachome bangi wakati Rais Magufuli sisi alishatukataza

Nadhani DC Jerry Muro ameshaichoka hiyo Nafasi aliyonayo, kwani kwa Maelezo yake haya sidhani kama yakimfikia Rais JPM atabakia kuwa DC.

Anamsingizia Mh. Rais, ukweli Rais hajawakataza kukomesha kilimo cha bangi, alichosema ni kuwa wakikuta shamba la bangi wawalazimishe wananchi wa eneo hilo kuifyeka na kuiharibu bangi hiyo na kamwe kazi hiyo isifanywe na askari wetu.

Jerry Muro hawezi kukwepa kikombe hicho kwani yeye ndiye mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama Wilayani kwake,sasa kama Kamati nzima imeboronga hadi Mh. Rais kuamua itumbuliwe yeye anaponaje hapo?
 
Mkuu wa wilaya ya Arumeru mh Jerry Muro amesema watendaji wa vijiji wamekuwa na tabia ya kuwataka wakuu wa wilaya watoke ofisini kwenda kuchoma moto mashamba ya bangi ilhali wao madc walishakatazwa na Rais Magufuli.

Muro amesema hayo wakati wa mkutano kati ya mkuu wa mkoa wa Arusha na viongozi wa wilaya ya Arumeru kuhusiana na mashamba ya bangi yaliyogunduliwa wilayani humo.

Source ITV habari

My take; Sikumbuki madc kukatazwa na Rais Magufuli kuchoma mashamba ya bangi

Maendeleo hayana vyama!
Alizungumza akiwa Chuga hapo



Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
 
Hebu tutaje vijiji korofi kwa bangi ili shughuli ifanyike kuhitimisha ulimaji wa bangi.
Vipo vijiji korofi na kata korofi kwa bangi...vijiji hivyo ukichunguza vimejishikiza na matycoon na maharamia flani wanaodeal na na fursa ikiwemo bangi.
Nashauri ianzishwe operesheni maalumu ya kusafisha mitandao iliyejengwa kwenye vijiii hivyo..yaani wenyeviti wa vijiji na vitongoji,watendaji wa kata na vijiji,maafisa tarafa ,wazee wa kimila ,wenyeviti na wajumbe wa kamati za Siasa za vyama.
Wawekezaji waliojipenyeza ambao inawezekana ndio wanunuzi ...matajiri wa maeneo hayo n.k

Haiwezekani vijiji au kata kama za Mwandeti,Oldonyosambu,Ngarenanyuki,Kisimiri,Siha,EngareOlmotonyi,ngabobo na ukanda wote huo wa kaskazini mwa jiji la Arusha ukawa ndio ukanda korofi wa bangi miaka nenda rudi.
Yaani vikundi vya wananchi,wazee wa mila,wanasiasa na wengine ni wa CCM wanakuwa ni sehemu ya kutetea uhalifu...halafu huwa wanajikosha kwa kuwa wa kwanza kupeleka umbea kwa wakuu wa mikoa au mawaziri.

Watendaji mahiri wa Serikali wanaathirika kwa kutumbuliwa huku vikundi vya kihalifu au vinavyofanya biashara ya bange vikijificha nyuma ya pazia la kisiasa.
All inAll kwa sasa ifanyike massive operesheni ya kusafisha kata na vijiji hivi bila kujali siasa au utajiri wa wanaowatumia.
Pia ifanyike thorough review ya hali ya usalama maeneo haya kuanzia longido,Arumeru ,Siha na Hai...watafutwe popote walipo King makers wa maeneo haya na wadhibitiwe vilivyo na mapema kwani wao ndio iawezekana kuwa wasafirishaji wa bange nje ya nchi.
Naomba orodha ya vijiji maarufu vya uuzaji bangi,madawa ya kulevya,ujangili wa Tembo,uporaji wa ardhi n.k kama wewe ni mzalendo tajahapa......

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
Wewe unaonekana ni Mmbea sana halafu Mkuda mkuda hivi
 
Ndio amesema hapo walishakatazwa. Hawezi kumsingizia Rais

Walikatazwa wapi na lini. ..?? SISI HATUWEZI KUJUA
 
Yani huyu dc jerry ni kilaza sijaona, yani aone shamba la bangi asubiri watendaji wa vijiji ndiyo wakateketeze, bila hata kujiongeza
 
Kama sijakosea Magufuli alishawahi kutoa hilo katazo akasema hao watu sio kazi yao kuchoma bangi.

Implicitly, kama kweli JIWE aliwakataza wasichome bangi basi mkemia wetu anajua faida za bangi na ndio maana aliwakataza wasiichome!!! JIWE legalize ganja!!!
 
Mkuu wa wilaya ya Arumeru mh Jerry Muro amesema watendaji wa vijiji wamekuwa na tabia ya kuwataka wakuu wa wilaya watoke ofisini kwenda kuchoma moto mashamba ya bangi ilhali wao madc walishakatazwa na Rais Magufuli.

Muro amesema hayo wakati wa mkutano kati ya mkuu wa mkoa wa Arusha na viongozi wa wilaya ya Arumeru kuhusiana na mashamba ya bangi yaliyogunduliwa wilayani humo.

Source ITV habari

My take; Sikumbuki madc kukatazwa na Rais Magufuli kuchoma mashamba ya bangi

Maendeleo hayana vyama!
View attachment 1500603
Amekuwa Mamlaka ya Nidhamu tangu lini??

hawa wanahitaji Induction
 
Nyie ndio wale mnaojidai mmefanikiwa kimaisha kumbe mnapiga deal za bangi
Wewe mwenyewe umesomeshwa kwa hela za .... huko Oldonyo. Umewasahau wale ndugu zako waliokimbizwa Border ya Namanga wakatelekeza punda bila mizigo??
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom