DC Jerry Muro hongera kwa kuanzisha English Medium School Arumeru

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
33,972
2,000
DC Jerry Muro ni DC kijana na mchapa kazi kwani katika wilaya yake anewezesha uanzishwaji wa Shule ya mchepuo wa kingereza yaani English Medium.

Katika mkoa wa Arusha kuliwahi kuwa na Shule ya English Medium ijulikanayo kama Arusha School ambayo mfadhili wa Simba Mo Dweji alipata kusoma hapo. Shule hiyo ni ya Serikali.

Leo hii kijana mpambanaji na mlokole ndugu Jerry Muro ameweza kujenga Shule nyingine ya mchepuo wa kingereza ambayo itashindana na shule binafsi.

Kongole kwake..
 

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
8,132
2,000
Yaani Mo kusoma hapo ndiye amekuwa mfano kwa kila mtu, yaani kuna ujinga mkubwa vichwani mwa watu, sawa na kile chuo cha uandishi wa habari pale gorofani Philips arusha, wanamtolea mfano Mirald utadhani hakuna wengine waliosoma hizo sehemu.
 

Jon Stephano

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
5,802
2,000
Mkuu m
Wakati Magufuli amepewa Tuzo ya kuenzi Kiswahili wewe unamsifia Jerry kwa kuanzisha Shule ya kizungu , lugha ya mabeberu ! hivi nyie wachumia tumbo huwa mnaamini katika nini ?
Mkuu malala huyo jingalao ndie pekee mwenye elimu ya juu kwenye hilo genge la MATAGA/LB7. Ana diploma ya theory in welding aliyoipata kwenye chuo kilichosajiliwa na VETA juu ghorofani Kariako.
 

Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
19,538
2,000
Alichoniudhi zaidi JERRY MURO ni kimoja tu, alishirikishwa kwenye ujenzi wa daraja la Mto wa pale Ilboru kupandia Visiwani akaitikia wito na akachangia mifuko 50 ya cement

Lakini, akashindwa kufuatilia na kusimamia ujenzi huo, alipaswa atumbue watu wazembe wanaochelewesha zoezi la ujenzi huo

Asipoangalia atakuja kutumbuliwa yeye...hajui kuwa watu wanapeleka taarifa kwa Boss wake kimyakimya
 

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
3,931
2,000
Wakati Magufuli amepewa Tuzo ya kuenzi Kiswahili wewe unamsifia Jerry kwa kuanzisha Shule ya kizungu , lugha ya mabeberu ! hivi nyie wachumia tumbo huwa mnaamini katika nini ?
Madhara ya kufikiri kwa kutumia makalio. Kwa hiyo English medium hawasomi kiswahili?
 

Mr Q

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,707
2,000
Miaka 50 ijayo watoto kwenye somo la historia topic iitwayo ukoloni mamboleo tanzani watakutana na swali lisemalo eleza ni kwanamna gani ubeberu ulishamiri miaka ya 2021 sababu ya kwanza itakuwa hiyo uliyoileta mtoa mada
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom