DC Jerry Muro acha kupotosha umma kwa kutetea Ukatili wa Elibariki Kingu

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Ndugu yangu Jerry Muogope Muumba wako na kama wewe ni mkristo nenda katubu achana na roho ya Kinyama kiasi hiki.

Jerry Muro unakuja na Balaah Blaah za kipuuzi eti CHADEMA wanakusanya Pesa kwa kusingizia kua wana mgonjwa anayeitaw Petter kama kisingizio.

Achana na roho ya Kishetani Jery Muogope Mungu wako. Petter Tamael Mtinangi aliyepigwa na Kingu 2020 yupo kwao Mighughe Kitandani hali yake ni mbaya sana hana msaada wowote. Kama huamini washa gari ya Umma nenda Minyuge kama hujamkutu Petter anakoroma kwa ugonjwa.

Soma: Ukatili na Unyama wa Mbunge wa CCM Singida Magharibi, Elibariki Kingu wailiza jamii



IGP Simon Sirro agiza RPC wa mkoa wa Singida aende akafanye uchungu ndio mtakua upotoshwaji wa maakusudi unaofanywa na DC huyu ambaye sasa ameonekana mtu wa hovyo kabisa.

Kingu anakuja na ngonjera zake za kijinga kabisa eti Petter alikuwa na matatizo yake, ujinga mtupu. Mnaelewa trauma za kwenye kichwa madhara yake huja kwa muda gani? Kingu acha ushamba na kuchezea maisha ya watu.

#*Kuna taalifa kwamba kesho unapeleka madaktari wako wa Mchongo kutoka hospitali ya Wilaya ya Makiungu na ofisi ya DMO kwenda kuandaa taarifa za Upotoshaji kuwa Petter haumwi na ugonjwa wake hauhusiani na kupigwa, tunalijua hili na tuwaambie kua hamtabaki salama mbele ya uhai na roho za watu. Ukweli ni kwamba Petter Mtinangi ni mgongwa sana kwa sababu ya ukatili wa ndugu Kingu. Mkificha ripoti umma utawaumbua.

DC Muro umepotoshwa na Kama huamini pitia taarifa hii na kushauri kesho mtembelee mgonjwa acha kupotosha.
👇👇

ANAHIJI MSAADA WA MATIBABU.
_____________________________________

JINA: PETTER TAMAEL MTINANGI

MAKAZI/ANUANI: MINYUGHE-SINGIDA .

UMRI: MIAKA 43

............................................................
Mtajwa hapo juu ni Petter Tamael Mtinangi, Mkazi wa kijiji cha Minyughe,Kata ya Ikungi mkoani Singida. Mapema machi 2020 alishambuliwa na Kikundi kinachodaiwa kua ni cha mbunge wa jimbo Singida Magharibi Ndg Elibariki Kingu sababu ikitajwa kua ni bwana Petter kunyanyua vidole viwili ikiashiria alama ya Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, hali hiyo ilisababisha ndugu Petter kukamatwa na vijana aliokua Mbunge wakiongozwa na Katibu wake aitwaye Abubakary Muna pamoja na Mwenyekiti UVCCM kata ya Puma ajulikanaye kwa jina la Hangida na kisha kumuingiza kwenye gari aina ya Noah ambayo iliwabeba. Kwa madai ya Ndg Petter mwenyewe ni kwamba walianza kumpiga na kumuumiza vibaya pamoja na kumfanyia vitendo viingine vya kumdhalilisha kinyume na maumbile pamoja na utu wake.

Bwana Petter Mtinangi alikua Mwenyekiti wa Baraza la vijana la chadema BAVICHA Wilaya ya Ikungi na baadaye Mwenyekiti wa Chama hicho Kata ya Minyughe mpaka anashambuliwa. Uongozi wake ndani ya chama hicho Petter anautaja kua ulimjengea uadui mkubwa sana wa kisiasa baina yake na Mbunge wa jimbo la Singida Magharibi ndugu Elibariki Kingu huku akisema kua alifikiri wangepoteza uhai wake kutoka na kipigo walichompa pamoja na vitisho.

Bwana Petter baada ya kushambiwa alichukuliwa na Vijana hao wakiongozwa na Mbunge na kisha kumpeleka katika kituo cha polisi Wilaya ya Ikungi. Baada ya hapo ndugu Petter alifunguliwa kesi ya kushambulia Kesi ya Katibu wa Mbunge, baadaye mashtaka yakabadilishwa tena na kusomeka kama kesi ya kushambulia gari ya mbunge, kesi iliendelea bila ya bwana Petter kupata matibabu wa la muda wa kupumzika kutokana kipigo alicho kipata. Kwa maelezo yake Petter alisema kua waliomshtaki walimwambia kua pona yake ni kuhamia CCM na kukanusha vitendo vyote vya kikatili alivyofanyiwa ili aweze kufutiwa mashtaka yake maana dhamira yao ilikua ni kumfunga kabisa.

Petter hakua na wakili wala msaada wowote wa Kisheria aliona ni bora akubali kuhamia CCM kwa muda lakini akifutiwa kesi atarudi tena kwenye Chama chake CHADEMA. Kweli baada ya bwana Petter kuhamia CCM kisha kweli akafutiwa mashtaka, baada ya kufutiwa mashtaka mbele ya mlango wa Mahakama aliikana CCM kwa kauli ya chini na kusema yeye ni CHADEMA damu hawezi kujiunga na CCM, hivyo ndiyo alivyofanya na alirejea CHADEMA na kuendelea na harakati zake za kisiasa pamoja na kua aliathirika vibaya kiakili pamoja na kimwili kwa sababu maskio yake yaliacha kusikia kabisa baada ya kupigwa.

Haikuchukua muda mrefu bwana Petter alianza kujiskia maumivu makali ya kichwa pamoja na mwili kukosa nguvu na baadaye jicho moja la kulia lilianza kua na jini hafifu. Baadaye akaanza kushindwa kutembea hali ilibadilika na kumfanya Mama yake mzazi kuanza kuomba msaada wa pesa kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki lakini baadhi ya wanasingida kupitia magroup ya Mtandao wa Watsap waliamua kumchangia kiasi ambacho kilimwezesha kwenda hospitali ya Benjameni Mkapa mkoani Dodoma kufanya vipimo ambapo nao walimpa rufaa kwenda hospitali ya MOI. Kutokana na mzunguko mrefu wa kupata matibabu hospitali ya MOI huku wakiambiwa wakae wasubiri kwa muda usiojulikana maana hakukua na kifaa cha kufanyia upasuaji,ndugu zake walienda hospitali ya Mloganzila ambapo kule alipatiwa vipimo,matibabu pamoja na dawa. Alifanyiwa Shunt kuyatoa maji yaliyojaa kichwani kwenye ubongo na kisha upasuaji mmoja na aliamriwa kurudi tena kufanya upasuaji wa mara ya pili maana hawakumaliza kwa sababu alithirika kwa kiasi kikubwa sana.

Kutoka na hali duni ya familia hiyo ndugu Petter hakurudi tena hospitalini tangu afanyiwe upasuaji wa kwanza kwa sababu ya kukosa pesa. Hali yake ni mbaya sana, haoni macho yake yote wala hasikii, hawezi kula chakula.

Unahitajika msaada wa dharura na haraka sana wa pesa za matibabu kufanya upasuaji wa Pili ambao kw makadirio ni shilingi million tano(5,000,0000/=) hii inajumuisha upasuaji ambao unaweza usiwe mmoja tena maana ya tatizo kuongezeka kutokana na kukaa muda mrefu nyumbani bila huduma yeyote, dawa pamoja na vipimo.

Chanzo cha taarifa hii ni ndugu Petter Mwenyewe na baadhi ya wanafamilia.

Mtanzania mwenzangu ukiguswa na taarifa hii, msaidie ndugu Petter apate mabibabu.

Ahsante.
 
Pole kwa Ugonjwa.
Ingawa unaumwa ila nakupa kongole kwa kujitahidi kujitetea wewe binafsi kutoka ulipo.

Tumuombe Mungu akupe wepesi wa kupona ndugu yetu.
Tanzania ya sasa sio ile ya JPM.

WAMERUDI Aiseee
@mwananchinewspaper!
 
Ndugu yangu Jerry Muogope Muumba wako na kama wewe ni mkristo nenda katubu achana na roho ya Kinyama kiasi hiki.

Jerry Muro unakuja na Balaah Blaah za kipuuzi eti CHADEMA wanakusanya Pesa kwa kusingizia kua wana mgonjwa anayeitaw Petter kama kisingizio. Achana na roho ya Kishetani Jery Muogope Mungu wako...
Wanateteana

1. DAB
2. Mnyeti
3. Sabaya
4. Hapy
5. Muro
6. gambo
7. Ogundu
8. Bashiri
9. Slowpole
10. etc
 
Pole kwa Ugonjwa.
Ingawa unaumwa ila nakupa kongole kwa kujitahidi kujitetea wewe binafsi kutoka ulipo.

Tumuombe Mungu akupe wepesi wa kupona ndugu yetu.
Tanzania ya sasa sio ile ya JPM.

WAMERUDI Aiseee
@mwananchinewspaper!
Enzi z mwendazake asibgethubutu hata kulalamika.
 
Kila ubaya utalipwa
I feel very sorry for him. Ninashauri kama wewe ni chama tofauti, basi ujongeapo kwenye shughuli ya chama kingine usifanye vitu vinavyoweza kutafsiriwa kama vya kichokozi.

Hakuwa na ulazima wa kuonyesha alama ya vidole viwili kwenye mkutano wa ccm.

Naamini hata chadema wakiwa na shughuli zao ukapeleka uccm wako hawatakuacha salama.
 
I feel very sorry for him. Ninashauri kama wewe ni chama tofauti, basi ujongeapo kwenye shughuli ya chama kingine usifanye vitu vinavyoweza kutafsiriwa kama vya kichokozi.

Hakuwa na ulazima wa kuonyesha alama ya vidole viwili kwenye mkutano wa ccm.

Naamini hata chadema wakiwa na shughuli zao ukapeleka uccm wako hawatakuacha salama.
Wewe huenda una tstizo la uelewa, umeambiwa walikua wanapita kulikua na vijana wa CHADEMA wamekaa kwenye mti wanaonyesha vidole viwili wakawakamata na kuwatia ndani, Petter Kams kiongozi ailipowafuata waliokamatwa akaambiwa wewe ndio tulikua tunakutafuta. Naye walimuingiza kwenye gari na kuanza kumpiga na kumlawiti.
 
I feel very sorry for him. Ninashauri kama wewe ni chama tofauti, basi ujongeapo kwenye shughuli ya chama kingine usifanye vitu vinavyoweza kutafsiriwa kama vya kichokozi.

Hakuwa na ulazima wa kuonyesha alama ya vidole viwili kwenye mkutano wa ccm.

Naamini hata chadema wakiwa na shughuli zao ukapeleka uccm wako hawatakuacha salama.
Huyu naye alifanya nini ?
2183704_IMG_1183.jpg
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom