DC Iringa Mjini, Richard Kasesela amelazimika kuomba radhi kwa umma baada ya kutoa taarifa feki ya kifo cha Dr. Salim Ahmed Salim

MakinikiA

JF-Expert Member
Jun 7, 2017
5,011
6,542

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Richard Kasesela, amelazimika kuomba radhi kwa umma, baada ya kusambaza taarifa za uongo juu ya kufariki kwa Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Dkt. Salim Ahmed Salim.

Loading...
Hapo jana usiku Kasesela alichapisha taarifa kwenye mtandao wa Twitter, ukieleza kutokea kwa kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt. Salim zilizodai kuwa mauti hayo yamemfika akiwa nchini Uingereza, ambapo baadae alizikanusha.

"Kwa dhati naomba nimuombe radhi, Dr. Salim Ahmed Salim na kwa sasa bado yuko na anaendelea na matibabu nchini Uingereza nimeongea na familia, ni bahati mbaya sana chanzo kilichonipa habari hakikuwa sahihi, ninaomba radhi kwa familia na Watanzania kwa ujumla."ameandika Kasesela.
Mapema jana Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping alimtunuku Waziri Mkuu huyo mstaafu wa Tanzania Dkt Salim, kuwa miongoni mwa watu waliosaidia nchi hiyo kurejeshwa kwenye Jumuiya ya Umoja wa Mataifa.
 
Kulikuwa na haja gani yakukimbilia kutangaza msiba wa watu??? yeye ni msemaji wa familia??? yeye ni msemaji wa serikali??? anastahili kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa udaku
Huyu anatakiwa achukuliwe hatua za kinidhamu haraka iwezekanavyo.yeye ni msemaji Wa serikali?
 
Kulikuwa na haja gani yakukimbilia kutangaza msiba wa watu??? yeye ni msemaji wa familia??? yeye ni msemaji wa serikali??? anastahili kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa udaku
jamaa alikuwa Rastafarian huenda alionja ile makitu yao
 
Endapo kama habari hii ina ukweli, KWA mujibu WA Sheria ya Mawasiliano ya Kimtandao ya huko Tz (EPOCA), anastahili kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria ili apewe haki yake anayostahili kulingana na makosa yake
 
"Kwa dhati naomba nimuombe radhi, Dr. Salim Ahmed Salim na kwa sasa bado yuko na anaendelea na matibabu nchini Uingereza nimeongea na familia"

Ulishindwa kuongea na familia ili kupata uhakika kabla huja_tweet......BWEGE
 
Tatizo la shetani wa kifo huwaga hana siri. Hupenda kuvujisha siri ya kifo cha mtu hasa siku zake zikikarbia ukingoni kwa kuwa yeye tayari huwa ana ratiba kamili.

Husambaza taarifa hizo kupitia ndoto, ziwe za usiku au za mchana.

Taarifa hizo 90% huwa zinanatokeo chanya.
Ref: faarifa za mapema za kifo cha King majuto, hasi mwenyewe zilimfikia na kuzikanusha.

Sasa na hizi, muda ndiyo mwalimu mkuu.
 
wakukurupuka huyo
1569849289611.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom