DC IGUNGA KAJIDHALILISHA MWENYEWE: Mwisho wa ubaya ni Aibu!

LENGEJU BOB

Member
Nov 1, 2010
53
29
Wamejisahau sana hawa... Bado wanaishi katika ulimwengu wa chama kushika hatamu...wanalewa divai ya ukada mpaka kwenye nyumba za ibada!.. Wanasahau kuwa ulevi nooma!! Haya tuliyajua muda mrefu, tulikuwa tunakosa ushahidi tu... sasa yamejidhihirisha mchana kweupe, kulikuwa hakuna namna nyingine ya kuanika uzandiki ule pasipo kumuumbua mhusika... Ingefanywa siri wakekanusha hao,, si mnawajua walivyo mahodari wa kukana?

Ni aibu sana lakini ya kujitakia, hebu angalia Mama wanao wanakuona umeminywa kama mwizi wa maembe, watu wa ukoo wako wanaficha uso kwa ajili yako, badala ya kuwa Alama ya ushujaa katika kutetea uhai na haki unakuwa kinara wa mikakati ya kuua democrasia... Likiisha hili jirekebishe na warekebishe na wenzioo......watu wanang'angana kupigana na wakati!....Ujumbe umefika, kama wezi wa simu za kichina wanachomwa moto tufanyeje kwa wezi wa Haki na Democrasia?....

Safari ndo kwanza imeanza, wala si suala la Chadema, ni ishu ya Wananchi tunaoimua, very soon tutaanza kuwashikisha adabu wanaouza chakula cha msaada, tutawaburuta wanaokula pesa sa miradi ya maendeleo na tutawakimbiza mchakamchana wanaozika utu wetu kwa propaganda dhaifu....very soon tutawafunga kengele na kuwazungusha nchi nzima, msiaminike tena, mtengwe mpaka na nafsi zetu wenyewe, maana mmekuwa makatili wa miili yenu na wasaliti wakubwa wa mioyo yenu..mnatenda yanayoumiza hata dhamiri zetu, halafu mnataka tuwashangilie tu, tuwasifie tu, tuwanyenyekee na kuwalambalamba.....Not this time, not today, not Igunga! Be ware.....Mwisho wa ubaya ni Aibu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom