DC Hawa Ngulume apata wakati mgumu na sera mbovu za huduma ya afya za CCM

mchakachuaji192

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
362
225
Aliyewahi kuwa mkuu wa Wilaya ya Mbarali, bi Hawa Ngulume yuko katika hali mbaya nyumbani kwake, Goba Kinzudi jijini Dar es Salaam akisumbuliwa na ugonjwa wa vichomi na mapafu.

"Nimeona nitumie chombo cha habari kufikisha ujumbe (wa ugonjwa) kabla sijafa,” alisema mkuu huyo wa zamani wa alipoongea na Mwananchi.


6003571.jpg
Bi. Hawa Ngulume​
Akizungumza na gazeti la Mwananchi nyumbani kwake jana, Ngulume alisema kwa miezi mitatu sasa yuko hoi na hawezi kutembea bila kusaidiwa na hivyo anaiomba serikali imsaidie aweze kwenda kutibiwa nje ya nchi. Alisema ameamua kutumia gazeti la Mwananchi kufikisha ujumbe kwa serikali na CCM kuhusu maradhi yanayomsumbua baada ya njia nyingine kushindikana.

“Nilipeleka taarifa kwenye chama changu kwamba ninaumwa nahitaji msaada, lakini sikujibiwa; pia nimefanya juhudi za kutaka kumwona Waziri Mkuu ili anisaidie, lakini juhudi hazikuzaa matunda. Nimeona nitumie chombo cha habari kufikisha ujumbe kabla sijafa,” alisema.

Ngulume, ambaye ni kada maarufu wa CCM aliyetumikia nafasi ya ukuu wa wilaya kwa miaka 18, alisema maradhi hayo yalianza kumsumbua baada ya kumalizika kwa mchakato wa kura za maoni za chama hicho. Alisema aliomba ridhaa ya chama hicho kimsimamishe kuwa mgombea ubunge katika Jimbo la Singida Mjini.

“Katika mchakato ule Mohammed Dewji alishinda, na mimi nikawa mshindi wa pili. Niliporudi Dar es Salaam nikaanza kujiandaa kwenda kumpigia debe mshindi kama ulivyo utaratibu wa chama chetu, ndipo nikaanza kuumwa ghafla,” alisema.

Mkuu huyo wa zamani wa wilaya ambaye amewahi kushika wadhifa huo kwenye wilaya mbalimbali zikiwemo za Bagamoyo, Ilala na Kibaha, alisema amekuwa akitibiwa katika hospitali za Lugalo, IMTU na Ocean Road.

“Kuna kipimo ambacho nilitakiwa kuwekewa kwenye kinywa katika Hospitali ya Ocean Road ili kiweze kubaini kama kwenye mapafu kuna maji au la, lakini ilishindikana kwa sababu ya kukosa pumzi, na hawana kipimo cha aina nyingine,” alisema.

Alishauriwa kwamba aende India ambako kuna vipimo vya aina nyingi ambavyo havihitaji kuwekwa katika kinywa na kwamba vipimo hivyo vingemfaa kutokana na matatizo yake ya pumzi. Alisema katika kuhangaika alifika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, lakini cha kushangaza alikaa kuanzia saa 8.00 mchana hadi saa 11.00 jioni bila kuhudumiwa.

“Ndipo mtu mmoja anayenifahamu aliyekuwa akipita nilipoketi, akanisalimia kwa kuniita mheshimiwa. Muuguzi mmoja jina ninalihifadhi akaja kutaka kunihudumia, nikamwambia ina maana siwezi kupata huduma hadi niwe mheshimiwa, nikaondoka kwa hasira," alisema.

Alisema baada ya kutelekezwa na kunyanyapaliwa Muhimbili, amekuwa akipata matibabu kwenye hospitali za binafsi kwa ajili ya kutuliza maumivu.

“Maumivu ninayoyapata ni makali sana, nina vichomi utadhani kuna msumemo unaokata viungo vyangu ndani ya tumbo. Ninalia usiku kuchwa kwa maumivu, wanaonisaidia ni majirani tu ambao hufika kila mara kunijulia hali,” alisema.

Hii ndio serikali ya Jakaya iliyojaa ubinafsi na kusahau watumishi wake, je tunawezaje kumsaidia huyu mama yetu jamani?
 

ChiefmTz

JF-Expert Member
Apr 15, 2008
2,833
2,000
Kwa kuzingatia jinsi kampeni zilivyokuwa, c vizuri kuhukumu viongozi wa kisiasa. Bali ni muda wa kujitazama kama taifa hasa suala la roho mbaya miongoni mwa watz.
 

Keykey

JF-Expert Member
Dec 1, 2006
3,254
2,000
Huyu Mama ni majeruhi wa uchaguzi wa mwaka huu, tena wapo wengi kila anayeanguka kwenye kura anaishia kitandani, na wote wanadai serikali amewatelekeza! Viongozi wetu wengi wanaishi kwenye dunia ya 'KUFIKIRIKA' na kujifanya hawajui hali halisi ya huduma katika hospitali zetu; pole sana Mama Ngulume hayo ndio maisha halisi huku uraiani.
 

Kunta Kinte

JF-Expert Member
May 18, 2009
3,689
2,000
Huyu mama analalamika nini sasa wakati alikuwepo serekalini katika ngazi za juu za kufanya maamuzi hawakufanya lolote sasa ndio anapiga kelele eti hakuhudumiwa hospitali! Yeye hajahudumiwa mara moja tu tayari amekimbilia kwenye magazeti! Ajue hayo ndio maisha yetu ya kila siku na kwa kuwa naye system imemtupa ndio yatakuwa yake pia. Aidha namkumbuka alikuwa arrogant sana kipindi akiwa dc kinondoni, nafurahi sana nikisikia watu wa aina hii nao wanapata watu wa kuwanyanyasa kama walivyonyanyasa wenzao
 

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,213
2,000
Pia akiwa dc-Kibaha aliwahi kupiga watu makofi sana!
Lakini alifanyiwa advertize ya hatari baada ya kufanyiwa shambulizi la ghafla na watu wasiojulikana, ambapo walimjeruhi ikiwa ni pamoja na kukatwa masikio kwa panga!

BTW, POLE MAMA, WAKUBWA WATASIKIA.
 

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
14,183
2,000
Mama Hawa Ngulume anastahili kupata huduma aliyopata Muhimbili kwani ni sehemu ya matunda ya uongozi wake anavuna alichopanda.Huduma za afya nchini zimekuwa za hovyo sana kwasababu sera ya CCM badala ya kuboresha huduma za afya wamekuwa wakitoa nafasi za matibabu kwa viongozi wake waandamizi.
 

Joo Wane

JF-Expert Member
Mar 14, 2007
629
1,000
Pole sana mama. Hujafa hujaumbika. Ila wakumbushe wakubwa wenzako uliowaacha madarakani kuwa huduma za afya ni janga kwa walalahoi wa nchi hii. Haya uliyokutana nayo muhimbili mara moja kwetu sisi walalahoi ni adha ya kila siku kwa maisha yetu yote
. Ila kama sikosei miaka si mingi sana ulimnasa kibao mwanakijiji kule mbarali aliyekuwa anapigania haki yake kwenye mashamba ya mpunga.
 

Edson

JF-Expert Member
Mar 7, 2009
9,455
2,000
kuna dawa aina ya mlonge

aitafute then atumie hivyo vichomi vitaisha

atumimie magome ya mti huo aina ya mlonge
 

Kichakoro

JF-Expert Member
Sep 10, 2008
2,363
2,000
Huyu Mama ndio alikataa kutujazia form za mikopo wakati akiwa DC kindononi 2000/2001. Kama
angekuwa mtu mzuri hizi shida asingezipata. What goes around comes round...... malipo hapa hapa.

Anyway ugua pole Mungu akujalie upone na uje kuwatumikia watu wake.
 

sosoliso

JF-Expert Member
May 6, 2009
8,497
2,000
tumezoea kuona wale wasiojiweza wakitoa maombi katika magazeti na radio..kuomba msaada toka kwa wasamaria wema..bt hii ya kiongozi wa serikali kuomba msaada halafu kutoka serikalini..ina walakini..inawezekana alijaribu kujiingiza ndani ya system..bt ikashindikana..so ametoswa kijumla..nadhani ni muda muafaka wa yeye kutafakari kwa kina..yale yote mazuri aliyofanya..then yale yote mabaya aliyoyafanya..then amuombe Mungu amsamehe..halafu auze ile nyumba yake moja pale mtaa wa kitomondo b..ili apate hela ya kujitibia...
 

Reyes

Senior Member
Sep 1, 2010
188
0
Anataka kwenda nje eti kwa vile ni kiongozi

Mimi mtoto wa kabwela ntapelekwa nje nikiugua?

Uzoefu wa matatizo ya huyu mama utumike kuboresha hospitali zetu ili kusiwe na suala la kutaka kwenda nje

Najisikia faraja kuchagua CHADEMA hata kama hatujashinda
 
Sep 15, 2010
53
0
Mama Hawa Ngulume anastahili kupata huduma aliyopata Muhimbili kwani ni sehemu ya matunda ya uongozi wake anavuna alichopanda.Huduma za afya nchini zimekuwa za hovyo sana kwasababu sera ya CCM badala ya kuboresha huduma za afya wamekuwa wakitoa nafasi za matibabu kwa viongozi wake waandamizi.

Pole sana mama tumuombe Bwana wa majeshi akujalie afya njema kwa kuzibariki dawa unazotumia
 

Henge

JF-Expert Member
May 14, 2009
6,939
2,000
Jamani ccm pesa za kuhonga mnazo ila hizi za kumtibia huyu mama hakuna!
Pole sana haya ndo maisha a TZ!
 

RayB

JF-Expert Member
Nov 27, 2009
2,752
1,250
Karibu aktika ulimwengu wetu mama hayo ndo maisha ya mdangayika wa kawaida kila siku
 

Henge

JF-Expert Member
May 14, 2009
6,939
2,000
Ndipo mtu mmoja anayenifahamu aliyekuwa akipita nilipoketi, akanisalimia kwa kuniita mheshimiwa. Muuguzi mmoja jina ninalihifadhi akaja kutaka kunihudumia, nikamwambia ina maana siwezi kupata huduma hadi niwe mheshimiwa, nikaondoka kwa hasira," alisema.

Rushwa zinatupeleka wapi jamani!
 

Kichakoro

JF-Expert Member
Sep 10, 2008
2,363
2,000
Nimepata wazo moja WANAMAGEUZI wote tuanzishe mfuko tumchangie huyu mama aende kutibiwa Maaana CCM wameshindwa
pamoja na kuweka mabango nchi nzima
 

Gurtu

JF-Expert Member
May 15, 2010
1,231
1,500
Aulizwe kama alimpigia kura Dr. Slaa, maana Dr. alisema huduma ya Afya bure kwa kila Mtanzania. Kwa vile Dr. amenyimwa uongozi kwa wizi wa CCM, huyo mama imekula kwake wala hakuna namna ya kumsaidia.

Hata hivyo, chama gani hicho anachozungumzia? Kama ni CCM watu walikuwa busy kuchakachua na vile vile mama huyo si mtaji tena katka chama hicho.
 

coby

JF-Expert Member
Nov 28, 2008
342
195
Huyu mama kawasumbua sana wafugaji na wakulima kule wilayani Mbarali - Mbeya, alikua anatembea na ulinzi wa kutosha then anatoa amri yoyote tena kwa jeuri hadi kuwanasa vibao hadi wanaume. Yaani wafugaji walikua wakimuogopa balaa. Eti analalamika huduma? Ndio maisha yetu ya kila siku watamcheka watu kama halijui hilo! Anyway namuombea apone ili aendelee kujifunza namna ya kuishi na watu hata ukiwa kibosile
 

Power to the People

JF-Expert Member
Jul 11, 2007
1,199
2,000
ningekuwa na uwezo wa kuonana na huyu mama ningekuwa na maswali ya kumuuliza.
1. amejihusisha katika shady deals ngapi tangu awe kiongozi wa katika serikali?
2. yale magari aliyokuwa akitembelea akiwa DC gharama ya 1 tu isingetosha kununua kifaa kitumike kufanya kipimo anachohitaji?

What goes around comes around.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom