Jumaaly
Member
- Sep 5, 2015
- 74
- 21
Mkuu wa wilaya ya Kinononi na Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa kiusalama wa Kinondoni Mh. Ally Hapi leo akiambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama, maafisa afya na biashara wa manispaa wameendelea na operesheni ya kusaka stoo Na magodauni bubu yasiyozingatia sheria za nchi, kukwepa kodi na kuvunja kanuni za afya.
Leo hii viongozi hao wametembelea na kukagua godauni bubu Manzese, Clabu bubu ya usiku cha Rombo ambayo imekua kitovu cha vibaka, danguro na kipindupindu kutokana na kanuni za usafi kutozingatiwa. Katika club hiyo ukaguzi ulifanikiwa kubaini ujenzi na upanuzi usio n vibali, chemba za vyoo kuwa zimejaa hadi kutapika, chemba za vyoo kumwagwa kwenye mtaro unaopita kwenye vyumba vya kulala na kwenda barabarani pamoja na chemba iliyojaa kuwa karibu na sehemu ya jiko na vinywaji.
Mh. Mkuu wa Wilaya ameagiza Mkurugenzi wa manispaa kukagua leseni zote za biashara za maeneo hayo kama zina uhalali na kufunga club hiyo mara moja. Aidha Hapi aliagiza vyombo vya dola kuwachukulia hatua za kisheria wamiliki wa maeneo hayo watakaobainika kuvunja masharti au kutokua na leseni.
Wananchi wa Manzese wakiwa wanaimba "Hapa Kazi tu" walimpeleka Mh DC Hapi katika Danguro lingine maarufu kwa jina la "Double A" ambapo watoto wadogo wanatajwa kuuzwa kingono.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na kamati ya Ulinzi na Usalama wameendelea na ukaguzi wa miradi ya maendeleo itakayofunguliwa na mwenge.