DC Hapi atoa siku saba kwa wanaochimba kokoto machimbo ya Boko kuondoka

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ametoa siku saba kwa wanaochimba kokoto kinyume cha sheria katika machimbo ya Boko kuondoka, kwakuwa shughuli zao zinazidi kuharibu mazin gira na kuhatarisha usalama wa wananchi hususan katika kipindi hiki cha msimu wa mvua.

Hapi ametoa maagizo hayo leo katika ziara yake kwenye Kata ya Bunju ambapo alitembelea katika machimbo hayo na kukuta uharibifu mkubwa wa mazingira uliotokana na shughuli za uchimbaji kokoto.

“Msiendelee kuchimba kokoto katika machimbo haya sababu mnahatarisha maisha ya wananchi, natoa siku saba za kuondoa vitu vyenu pamoja na kokoto mlizochimba. Ila msiitumie nafasi hiyo kuendelea kuchimba,” amesema.

Sambamba na hilo, Hapi amewaagiza Afisa Mazingira wa Manispaa ya Kinondoni , Mohamed Msangi pamoja na Afisa Mipango Miji,Respicius Mathew kuangalia jinsi ya kubadilisha matumizi ya machimbo hayo kwa kulikarabati ili liwe dampo la manispaa.

Amesema kama machimbo hayo yatatengenezwa kuwa dampo, itasaidia kuondoa changamoto ya mlundikano wa taka pamoja na kuliingizia manispaa mapato kupitia tozo za ushuru wa taka.

“Kwa nini ili eneo msiweke mradi wa dampo kupitia miradi ya mazingira. Na kama mkitaka kulijenga msilifanye kiholela, mfanye liwe la kisasa ili mmomomyoko usitokee. Huu mradi ni mzuri na utaliingizia mapato manispaa pamoja na kuondoa mlundikano wa taka,” amesema.

Kwa upande wa Afisa Mazingira wa Manispaa, Mohamed Msangi amesema litasaidia kurahisisha usafirishaji wa taka hasa kwa wakazi wa Bunju, Mabwepande, Boko, Kawe na Mwenge.


Chanzo: Dewji Blog
 
Tamko la ngapi vile huyu kijana nae ameanza kulewa madaraka kisa anatembea V8 kaona watu wote wanatembekea V8
 
Back
Top Bottom