Egnecious
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 875
- 960
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ally Salum Hapi Leo Jumatatu ya 30/05/2015 ameanza Ziara Kutembelea Hospitali 48 za Serikali zilizoko Wilaya ya Kinondoni. Ziara hii ataifanya kwa Zaidi ya siku Saba (7) ambapo atatembelea Zahanati na Vituo vya Afya ili Kujionea Huduma na Changamoto mbalimbali zinazo kabili Hospitali Hizi.
Mh DC Leo ametembelea Vituo Vifuatavyo.
1. ZAHANATI YA WAZO
2. ZAHANATI YA MADALE
3. DISPENSALI YA MBOPO
4. ZAHANATI YA TEGETA.
5. ZAHANATI YA KUNDUCHI
6. DISPENSALI YA SALASALA.
7. DISPENSALI YA NDUNBWI.
Kote huku Mkuu wa Wilaya amezungumza na Waganga Wafawidhi wa Hospitali, Manesi, Pamoja na Baadhi ya Wagonjwa.
Mkuu wa Wilaya kamaliza Ziara yake Saa 12:00 Jioni Hii Nakurejea Ofisini Kuendelea na Majukumu Mengine.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ally Salum Hapi Kesho Saa 5 asubui ataendelea na Ziara yake.