DC Gondwe atoa wiki 1 barabara ya Keko ifanyiwe marekebisho

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,533
2,000
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe ametoa wiki moja kwa Mkandarasi kuhakikisha anaifanyia marekebisho Barabara ya Keko ili iweze kupitika kiurahisi.

Gondwe ametoa agizo hilo leo alipofanya ziara kukagua barabara hiyo wilayani humo mkoani Dar es Salaam na kubainisha kuwa barabara hiyo imekuwa kero kubwa kwa wakazi wa Temeke.

"Hii ni Barabara ambayo ipo kwenye mpango wa kupita magari yaendayo kasi, moja ya makubaliano katika mkataba ni kufanya marekebisho madogomadogo na tayari TANROADS wamewakabidhi, hatuwezi kukaa kusubiri, nimewapa siku saba Wakandarsi watengeneze ili Wananchi wa Temeke waendelee na kazi zao"amesema Gondwe

Chanzo: HabariLeo
 

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,098
2,000
DC yuko tayari kuwajibika hiyo barabara itakapokamilishwa chini ya kiwango ili tu wawahi muda aliotoa?
 

Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,080
2,000
Anajimwambafayi aaiyyiii!
Matamko.com

Everyday is Saturday............................... :cool:
 

Gilbert A Massawe

Senior Member
Feb 18, 2021
106
225
Keko Ni Balaa ukiwa na kigari cha Chini utachekecha kama mchawi

Kiukweli Ujenzi wa Barabara unafanyika sana dsm naona Barabara Ya Kwa Mwl Nyerere Magomeni nayo imefumuliwa samabamba na Kuelekea Mburahati👏🏿🙏🏿

Kariakoo nako Agrey namwona mkandarasi
 

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
42,666
2,000
Keko ipi hiyo mbona ume generalize?
Kutoka veta hadi njia panda ya taifa, wanajenga mwendokasi ila wakandarasi wanavuruga wanaacha kitimtim kwa watumiaji. Ni kama kilwa road tu wanajenga hapa wanaacha wanahamia pale wanaacha sasa kazi ipo kwa watumiaji. Asubuhi mtapita kushoto,mchana katikati jioni kulia kesho hamna njia!
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
102,079
2,000
Kutoka veta hadi njia panda ya taifa, wanajenga mwendokasi ila wakandarasi wanavuruga wanaacha kitimtim kwa watumiaji. Ni kama kilwa road tu wanajenga hapa wanaacha wanahamia pale wanaacha sasa kazi ipo kwa watumiaji. Asubuhi mtapita kushoto,mchana katikati jioni kulia kesho hamna njia!
Hakika ni kero mkuu
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
57,889
2,000
Gondwe acha kucheza michezo michafu. Usiishie kutoa wiki moja ya ujenzi wa barabara, toa na fungu.
Tunajua una uhasama na mhandisi wa wilaya. Acha maneno mbifumbofu, chunga heshma yako
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom