DC Gondwe aagiza Wanafunzi watatu wafukuzwe Shule kwa kujihusisha na vitendo viovu

Watakapokutana na changamoto za maisha wakianza kujitegemea ndio watakumbuka kuwa kuna mtu aliamua kukatiza elimu yake na lawama zake zitabaki kuwa tabu kwa walioamua.

Kwa primary bado wanahitaji kusikilizwa hadi wanafikia hapo changamoto ni nini? Unaweza kuta anachukulia kama jambo / mchezo wa kawaida kutokana na malezi duni anayolelewa.

Kulikuwa na watukutu miaka ya 94 tambaza na azania lkn walitumia mbinu nzuri sana ya kuwatawanyisha shule mbali mbali za boarding huko mikoani na tatizo likaisha kwa asilimia mia.

Kama wale wote wangefukuzwa leo tungeongeza taifa la wajinga. Wakati mwingine tufikiri future ya watu wetu na taifa kwa ujumla kwa ikiwa kuna njia nyepesi za kutatuwa tatizo na sio kufikiri kukomoa kiumbe ambacho kinaweza kubadilika bila kutumia nguvu kubwa.
 
Mkuu wa Wilaya hana mamlaka ya kumfukuza mwanafunzi shule. Bodi ya shule ndio yenye mamlaka ya kumfukuza mwanafunzi shule. Ni tayari kukosolewa
 
Ndiyo maana vijana wanakosa bikra kumbe ilisha tolewa siku nying Sana
Sio jambo la kushangaza maana siku hizi watoto wanapata exposure ya sex katika umri mdogo na vile wasanii wetu siku hizi wanajitahidi kuimba mambo ya chumbani kwa ustadi.. bado hajaingia mtandaoni akayaona mambo live.

Ni lugha gani utatumia hadi mtoto akueleww kuwa sex sio haki yake.
 
ila kiukweli waalimu wana kazi ya ziada..
Hawa watoto wa siku hizi mbona naona kama ni shida maana bora hata kipindi chetu japo ni juzi juzi ila tulikuwa na uoga

siku hizi sasa, better sikuchukua ualimu maana
Changamoto sio ndogo mkuu, yaani ni balaa
 
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe, ameagiza kufukuzwa kwa wanafunzi watatu wa Shule ya Msingi Toangoma iliyopo wilayani Temeke, Dar es Salaam kwa kosa la kujihusisha na vitendo viovu (ngono) ambapo ni kinyume na maadili ya shule...
Amekurupuka tena sana aina hii ya uongozi ni ya ajabu sana he has no qualities.
 
Hivo vitoto vinapigana miti kweli au michezo michezo tu?

Kuwafukuza watoto kama hao shule naona bado sio solution.
 
Nchi ya kusadikika always watawala wake wana maamuzi ya mihemko,huyu DC amewafukuza shule kwa kutumia sheria gani?lini nchi yetu utawala bora utatamalaki?...
Gondwe naona anapotea njia, sheria to a elimu inaeleza vizuri tu makosa yatakayosababisha moto kufukuza shule na taratibu gani zifuatwe.
 
Kwa kweli kuwafukuza shule primary sijui watakuwa wageni wa nani teena hao watoto.
 
wazazi wanakaa chumba kimoja mke, baba na mtoto/watoto, usiku wazazi wanafanya yao watoto wapo macho wanakula deo,mchana wanaenda ku practice na wenzie shule
Wahindi huwa nao wanalala chumba kimoja na double deck kibao,lakini hawana hiyo tabia, hufanya kwichi kwich mchanaa kweupee wakati watoto wao wapo shuleni nao wamefunga maduka mchana kwa ajili ya kwenda kula,sasa sisi miafrika kwichikwich unaanza saa 8 usiku hadi kunakucha
 
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe, ameagiza kufukuzwa kwa wanafunzi watatu wa Shule ya Msingi Toangoma iliyopo wilayani Temeke, Dar es Salaam kwa kosa la kujihusisha na vitendo viovu (ngono) ambapo ni kinyume na maadili ya shule....
DC Gondwe, kuwafukuza shule kutawasaidia nini? Kwanini wasifanyiwe counseling? Kwanini wasitafute namna nzuri ya kuwasaidia? Wengine hao ndio watatubu na kututangulia kwenye ufalme wa Mwenyezi Mungu, kama wakijua ukubwa wa tatizo hilo na kuamua kuliacha.

Ingawa pande zile kule umakonde mwingi sana, khaaaa!!!
 
DC Gondwe, kuwafukuza shule kutawasaidia nini? Kwanini wasifanyiwe counseling? Kwanini wasitafute namna nzuri ya kuwasaidia? Wengine hao ndio watatubu na kututangulia kwenye ufalme wa Mwenyezi Mungu, kama wakijua ukubwa wa tatizo hilo na kuamua kuliacha.

Ingawa pande zile kule umakonde mwingi sana, khaaaa!!!
Baada ya kushindwa kutatua tatizo wao wameamua kuongeza tatizo.
 
Kwa sheria ipi na lini kawaona wanafanya hivyo vitendo. Huyu DC kichwa debe kabisa maamuzi ya kijinga amekaa ofisini anafanyakazi kwa hasira. Wanasheria pambaneni kuwaokoa hao watoto
 
Back
Top Bottom