DC Gondwe aagiza Wanafunzi watatu wafukuzwe Shule kwa kujihusisha na vitendo viovu

Ingefanyika social investigation kabla ya kuwafukuza ili kujua sababu iliyowapelekea kufanya hayo. Pengine wanahitali unasihi na ushauri tu wao na familia zao. Unakuta chumba kimoja kimewekwa pazia wazazi na watoto wanalala humohumo.
 
Sasa kuwafukuza shule ndio solution? Hii nchi ina viongozi wa ajabu sana
Ni ushamba huo.. yaani hii inchi bado kuna watu wana mawazo primitive sana.. Akati ndo wanatakiwa wapewe elimu zaidi ili wajue kwamba walichofanya ni makosa..
 
Ni ushamba huo.. yaani hii inchi bado kuna watu wana mawazo primitive sana.. Akati ndo wanatakiwa wapewe elimu zaidi ili wajue kwamba walichofanya ni makosa..
Kweli kabisa. Hao watoto wasaidiwe. Shule hiyo ina watoto 4000. Inabidi igawanywe ziwe shule nne au tano ili waweze kuwamudu hao watoto.
 
Je, wao kama wasimamizi wa taasisi hiyo (shule) na lama viongozi wa serikali katika eneo hilo walioruhusu vichaka kuota na kuwa guest bubu za watoto wetu wamechikuliwa hatua gani?
 
Aidha, Gondwe ameagiza kupigwa kwa kura ya siri kwa kila darasa ili kuwabaini wanafunzi wote wanaojihusisha na vitendo hivyo na baada ya kuwabaini wafanyiwe uchunguzi wa kitabibu kuthibitisha tuhuma hizo na wakithibitika wazazi wao wapewe taarifa na hatua kali za kisheria zichukuliwe ikiwemo kuondolewa shuleni.
Kwanini upime waliopigiwa kura tu?, pima wanafunzi wote wa kike tujue nani hajihusishi na huo mchezo. Kisha viongozi wakiandae kupokea matokeo/majibu😷😷😷😷😷😷😷😷😷
 
DC hapa naona ameponyokwa kidogo. Mwanafunzi wa S/M ni minor, huwezi kumuhukumu kirahisi hivyo. Nitafurahi nikisikia wamerudishwa shule. Ina maana hata viboko vimewashindwa?
 
Namuunga mkono, ngono ni kosa linaloweza mfukuzisha mwanafunzi shule kwa mujibu wa sheria.
 
Badala ya kuamrisha wapelekwe kwa wanasaikolojia wao wanawafukuza shule ili iweje huko mtaani na maisha yao ya baadaye!

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Hivi ukisikia mwanao wa kiume wa darasa la tatu ana lawitiwa na kijana wa darasa la sita kila siku huko vichakani tena anapewa onyo kali asiseme popote, je ukisikia huyu kijana wa darasa la sita anae walawiti watoto wa la tatu kushuka chini amefukuzwa shule utaumia?
 
Mpango wetu wa sasa ni kuwa elimu ya sekondari ni elimu ya lazima. Unafukuza ili iweje?
 
Sasa kuwafukuza shule ndio solution? Hii nchi ina viongozi wa ajabu sana
Atafukuza wangapi, vitoto vingi vimeharibika. Angehangaika na somo la maadili kuanzia walezi hadi waalim.

Kuwafukuza shule ni kuwaharibia maisha tu.

Ukute na waalim wanachangia kuwaharibu watoto.

Kumbe Gondwe naye ana uelewa wa chini hivyo.
 
Back
Top Bottom