beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe, ameagiza kufukuzwa kwa wanafunzi watatu wa Shule ya Msingi Toangoma iliyopo wilayani Temeke, Dar es Salaam kwa kosa la kujihusisha na vitendo viovu (ngono) ambapo ni kinyume na maadili ya shule.
Gondwe ametoa agizo hilo leo alipotembelea shule hiyo kwa lengo la kutaka kupata ukweli wa kile kilichoripotiwa na vyombo vya habari siku chache zilizopita kuhusiana na kukithiri kwa vitendo vya ngono katika shule hiyo, huku akiutaka Uongozi wa Shule hiyo pamoja na Uongozi wa Kata, kuchukua hatua za haraka kukomesha vitendo hivyo ambavyo vimeonekana kukithiri shuleni hapo.
Aidha, Gondwe ameagiza kupigwa kwa kura ya siri kwa kila darasa ili kuwabaini wanafunzi wote wanaojihusisha na vitendo hivyo na baada ya kuwabaini wafanyiwe uchunguzi wa kitabibu kuthibitisha tuhuma hizo na wakithibitika wazazi wao wapewe taarifa na hatua kali za kisheria zichukuliwe ikiwemo kuondolewa shuleni.
Gondwe ametoa siku saba kwa uongozi wa shule na wa Kata ikishirikiana na uongozi wa Mtaa kuweka mikakati ya pamoja ili kuangalia njia ya kutokomeza vitendo hivyo.
Chanzo: IPP Media