Dc geita amwekea mizengwe kamanda mawazo dhidi ya m4c . | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dc geita amwekea mizengwe kamanda mawazo dhidi ya m4c .

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OMUSILANGA, Oct 1, 2012.

 1. O

  OMUSILANGA JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 384
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndiyo wakuu! Nitaanza na nukuu zifuatazo :- 1. Mwl Nyerere ktk kitabu chake cha Binadamu na Maendeleo alipata kusema "TANZANIA NI YA WATANZANIA WOTE, HAKUNA MTU MWENYE HAKI YA KUSEMA MIMI NDIYE WATU,WALA HAKUNA MTANZANIA MWENYE HAKI YA KUSEMA NAJUA LINALO WAFAA WATANZANIA NA WENGINE NI LAZIMA WAFUATE.WATANZANIA WOTE LAZIMA WAAMUE MAMBO YA TANZANIA." 2. Rais wa zamani wa marekani, Abraham Lincolin May 29,1849 alipata kusema "UNAWEZA KUWAPUMBAZA WATU WACHACHE KWA KIPINDI CHOTE,NA WATU WOTE KWA KIPINDI FULANI, ILA HUWEZI UKAWAPUMBAZA WATU WOTE KATIKA NYAKATI ZOTE." Ni wazi kuwa uteuzi wa wakuu wa wilaya na mikoa kwa kipindi haujalenga kuwasaidia wananchi kutatua kero zinazo wasumbua bali ni kupunguza nguvu za vugu vugu la mabadiliko. Napenda nithibitishe hili kwa DC wa geita, ndgu Mackenzie. Tangu aje hapa, yeye kazi yake ni kuamrisha wenyeviti wa mitaa kushusha bendera za cdm .Pia ameshirikiana mkurugenzi wa halimashauri wilaya kuzuia mgodi wa GGM kulipa fidia kwa wakazi wa kijiji cha Katoma. Jana kwenye mkutano mkubwa wa uzinduzi wa M4C mkoani geita ulioongozwa na Mb Wenje, Kamanda Mawazo na Kamanda Rogerz,mbunge kivuli jimbo la geita walitoa matamko mazito kwa DC na RC Geita waachane na shughuli za ukada wa ccm ambazo hazina tija kwa wana geita na taifa kwa ujumla bali wawatumikie wananchi na kushughulikia utatuzi wa kero zao. Baada ya mkutano huo Kamanda Rogerz aliitwa polisi na OCD lakini baadae ali achiwa ila akawa ana shinikizwa asaini maelezo kuwa Kamanda Mawazo alitoa lugha ya matusi kwa DC.Kwa ushahidi ili kuonesha kuwa nafasi hizi za DC na RC hazina tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla, plz soma sms hii iliyotoka kwa DC geita kwenda kwa Valence Robert, reporter wa RFA geita baada ya kumuuliza maswali juu ya shutuma zilizo tolewa na cdm kwenye mkutano wa hadhara tarehe 30.9.2012. "SASA NDUGU YANGU HIYO NDO SIASA. MIMI KAMA KADA WA CCM NI WAJIBU WANGU KUUSAMBARATISHA UCHADEMA.HAO WA KATOMA JIBU UNALO. HIVI MIMI NITASABABISHAJE WATU WASILIPWE?" Kwa kifupi hiyo ndo sintofahamu iliyopo hapa geita mjini.
   
 2. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,590
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Laana za watanzania zitawapata watendaji wengi wa ccm.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kwa msaada tu, anaitwa Ndg Manzie Mangochie!....Kabla ya kuja Geita alikuwa Mafia, ambako alipata skendali mbaya sana ya Kupiga marufuku wavuvi wadogowadogo kuvua kwenye maeneo ya mazalia, na badala yake akaweka mitumbwi yake binafsi ili ifanye kazi ya kuvua eneo hilohilo, na wananchi walipoona wakamlipua kwenye vyombo vya habari, akazima soo kwa ujanjaujanja na vitisho!
  Jamaa ana asili ya ubabe sana huyu, na niliposikia ishu ya Kijiji cha Katoma nilijua wazi kuwa lazima atakuwa amekula fungu toka GGM!
   
 4. mathewa

  mathewa JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 5, 2012
  Messages: 420
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 80
  mkuki hauwezi kuzuiwa kwa mikoni. hiyo ni kazi bure. mda wa mabadiliko ni sasa. hawawezi kuzuia mabadiliko watu wanayoyahitaji
   
Loading...