DC Arusha ambaye aliwahi kutoa 'Singo' ya kumsifia Magufuli kuwa ni jembe adai kuwa Magufuli alikuwa ni fisadi

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
39,901
95,404
Katika hali ya kustaajabisha, DC wa Arusha Kenani Kihongosi ambae aliwahi kutoa 'Singo' niliyoambatanisha hapo chini ya kumsifia Magufuli kwa kudai kuwa Magufuli alikuwa ni jembe la kila kitu aibuka na kudai kuwa Magufuli alikuwa ni fisadi.

Anadai kuwa katika awamu hiyo Serikali ilikuwa haiweki wazi kuwa imekopa nini na kwa matumizi gani.

Kilichonifanya nilete huu uzi siyo tu kumshangaa Bwana huyu bali nataka niweke wazi kuwa Tanzania hatuendelei kwa sababu ya kuwa na viongozi wanafiki.

Anachomaanisha huyu Bwana ni kwamba alikuwa anajua kabisa kuwa Magufuli alikuwa ni fisadi lakini hakusema kipindi Magufuli akiwa hai ili kulinda ugali wake.

Katika Mataifa yaliyo serious viongozi huweka misimamo yao mbele kwa maendeleo ya Taifa.Viongozi huwa wapo tayari kujiuzulu au kufukuzwa kazi kwa maslahi mapana ya Taifa.

Lakini huku kwetu ni tofauti.Viongozi wapo tayari kutetea ujinga,ufisadi,wizi,mauaji,ukandamizaji wa wananchi na kadhalika ili kulinda ugali wao.Hapa Tanzania viongozi wapo tayari kumtetea kiongozi aliebadilika kuwa kichaa au mwendawazimu ili kulinda nyadhifa zao.

Katika hali kama hii usitegemee Taifa kuendelea kamwe.Hii ni kwa sababu pale kiongozi anapoamua kubadilika kuwa fisadi,mwizi,mkandamizaji au hata kichaa basi hulindwa na chama chake pamoja na viongozi wengine waliopo madarakani ambao lengo lao ni kulinda nyadhifa zao na wala siyo kutetea maslahi mapana ya Taifa.

CCM kwa miaka mingi imekuwa ikitoa viongozi wa aina ya huyu Bwana na ndiyo maana Tanzania miaka nenda haiendelei.Ni muda muafaka sasa CCM kukaa pembeni ili kupisha vyama vingine vya siasa ambavyo vina maono pamoja na nia ya dhati ya kulikomboa Taifa hili.

VD.jpg
16410193477180.jpg
 
Nilichogundua kwa hasa wachumia tumbo wa lumumba ni kua kwanza wanamsoma kiongozi wao ni mtu wa namna gani.

Kwa jinsi wanaojitokeza wengi kumtupia lawama mwendazake ilhali zamani walikua wanamsifia ni dhahili kua mama haukua anaelewana na mwendazake kwa namna moja au nyingine na watu wa karibu huenda walijua hicho kitu.

Ndio maana sio viongozi wa chini yake tu ila hata yeye alishwahi kukiri huko nyuma hakukua sawa kwa kutupa madongo utawala uliopita.
 
Mkuu mbona unakuwa kama unaishi ughaibuni?

Kwa mkaazi wa Tanzania haya mambo ya kubadilika kama kinyonga kwa viongozi wetu ni jambo la kawaida.

Wanachojali ni kujaza matumbo yao na watoto wao kusoma shule za uhakika habari za kujuheshimu hawajali kabisa wanakuwa kama ndumila kuwili.
 
Ningekuwa ni mimi, kiongozi yeyote anayenisifia hata pale ninapokuwa nimechemka, NAMTUMBUA mara moja.

Au ili kuwajua wanafiki ndani ya serikali yangu naweza nikaamua kutoa wazo la kipuuzi/ kipumbavu kwa kusudi ili niwatambue wanafiki watakaosifia wazo/jambo hilo wakati wakijua ni la kipuuzi.
 
Kama rais Samia hawezi kujifunza kitu kutoka kwa hawa njaa kali basi itakuwa ajabu sana. Ingekuwa mimi kila anayenisifia kupita inavyostahili ningemtumbua niwaache wale wanaonikosoa tu.

Nakuunga Mkono””TATIZO VIONGOZI WETU WANAPENDA SIFA ATA KM WAJUA HAKIKA KUA HAWASTAILI WANACHOSIFIWA NACHO,,Wanajenga KIZAZI CHA OVYO KABISA,,
 
Back
Top Bottom