DC Arusha akonga nyoyo za wamachinga soko la Samunge lililoungua

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Serikali imewahakikishia wamachinga kuendelea kufanyabiashara kwenye soko la Samunge lililoungua moto na kuwaondolea hofu iliyojengeka kwamba ina mpango wa kuwaondoa katika soko hilo.

Akiongea na maelfu ya wafanyabiashara hao zaidi ya 5000 Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro ameigiza halmashauri ya jiji la Arusha kuhakikisha wanaharakisha kujenga miundombinu ya soko hilo ili kuwapa nafasi wafanyabiashara kuendelea na shughuli zao.

Ameeleza kuwa hakuna mfanyabiashara mdogo aliyekuwa anafanyabiashara katika soko hilo atakayeondolewa bali serikali inahitaji kuweka sawa hali ya ufanyaji wa biashara ndani ya soko hilo.

"Niwatoe hofu hakuna mtu atakayeondolewa ndani ya soko hilo kama maneno yanavyopita chini chini msiyasikilize kwa kuwa serikali inahitaji kuweka mazingira rafiki ya ufanyaji wa biashara ndani ya siku saba itakuwa teyari"Amesema Daqarro

Amebainisha kuwa halmashauri itaendelea kufanya tathmini ya miundombinu rafiki kwa majanga ili kuondoa changamoto iliyojitokea wakati wa kuzima moto ikiwemo kuweka nafasi za kuweza kupitika ndani ya soko hilo.

Awali wafanyabiashara hao wadogo walikuwa na hofu ya kuondolewa katika soko hilo jambo lililowalazimu kukusanyika kwa wingi eneo hilo ili kujua hatima yao,suala ambalo Mkuu huyo wa wilaya aliwahakikishia kuendelea kufanya biashara zao na kwamba hakuna atakayewaondoa.

Katika hatua nyingine Daqarro ameagiza kufungwa kwa barabara mojawapo iliyo kando ya soko hilo ilikutoa fursa kwa baadhi ya wafanyabiashara ambao bidhaa zao hazikuunguliwa na moto kuendelea na biashara zao hadi miundombinu ya soko hilo itakapokuwa tiyari.

Hata hivyo aliwataka wafanyabiashara waliounguliwa kufanya usafi na kutoa mabaki ya mabati ili kupisha soko hilo kufanyiwa marekebisho, tathmini na miundo mbinu .

Awali aliyekuwa mstahiki meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro ametoa pole kwa wafanyabiashara hao huku akipongeza uamuzi wa serikali kwa kuruhusu wafanyabiashara hao wadogo kuendelea na shughuli zao katika soko hilo mara baada ya marekebisho kukamilika.

Naye Mwenyekiti wa wamachinga Mkoa wa Arusha Amina Njoka ameishukuru serikali kwa hatua kuweza kuwaruhusu kuendelea kufanya biashara katika soko hilo kwani walikuwa gizani hawajui hatma yao ambapo alitoa angalizo kwa serikali kuendelea kuwasimamia ili kila moja aweze kupata eneo lake la biashara na kuondoa wavamizi.

Mwisho.

IMG_20200330_125449.jpeg
IMG_20200330_120253.jpeg
IMG_20200330_115645.jpeg
IMG_20200330_105352.jpeg
IMG_20200330_125412.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
RC Gambo anaweza kuja na yeye akatoa tamko la kupingana na DC
Kama kawaida yao wanavyopenda kuoshena. Tena ataita watu wakusanyike halafu aseme DC alikusanya watu wakati kuna CORONA.
Hawa watu huwa wananifanya niache kuhuzunika nianze kufurahi tu maana hakuna jinsi.
 
RC Gambo anaweza kuja na yeye akatoa tamko la kupingana na DC
Alafu mkulu akifanya ziara naye anatoa tamko la kuwapinga wote. Ndio maisha yetu.

Kipindi wakurugenzi wa majiji wanazuia machinga wasifanye biashara hovyo mkulu akawaambia uzieni mnapotaka. Siku hizi jioni watu wana meza soko kuu lakini wanatoa bidhaa zao wanakuja kupanga barabarani ukipita vibaya lazima ukanyage nyanya za watu.
 
Back
Top Bottom