DC amtaka `Dada wa Kikombe’ asitishe huduma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DC amtaka `Dada wa Kikombe’ asitishe huduma

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Apr 3, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  DC amtaka `Dada wa Kikombe’ asitishe huduma

  Imeandikwa na John Nditi, Morogoro; Tarehe: 2nd April 2011 @ 23:55 Imesomwa na watu: 114; Jumla ya maoni: 0
  WAKATI huduma ya tiba ya kiimani ya `vikombe’ ikizidi kuenea nchini, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu, amemwagiza Fatma Senga (41) wa mjini hapa kusitisha kwa muda huduma ya tiba ya magonjwa sugu anayodai kuitoa baada ya kuoteshwa.

  Mwambungu, alitoa agizo hilo hivi karibuni kwa maelezo kwamba, kutokana na ukweli kuwa anahudumia idadi kubwa ya watu, ni vyema akasitisha kwanza huduma hiyo kwa muda, ili kuwezesha wataalamu kuchukua sampuli ya dawa hiyo ili ifanyiwe kwanza uchunguzi.

  Mwanamke huyo, mzaliwa wa Mzenga, Pwani ambaye kwa sasa anaishi Kata ya Kichangani, mjini hapa amedai kuoteshwa na Mungu kutumia mizizi minne ya miti shamba kutibu wagonjwa kwa kuwatoza Sh 200 kwa kikombe, na sehemu ya fedha hizo kupelekwa msikitini.

  Akizungumza nyumbani kwa ‘Dada wa Kikombe’, Mwambungu alifafanua kuwa, yeye na viongozi wa Manispaa ya Morogoro, hawakwenda kuzuia utoaji huduma hiyo, bali kujiridhisha kwanza.

  Alifuatana na viongozi kadhaa, akiwamo Mganga wa Manispaa ya Morogoro, Ibrahim Mahinzo.

  Aidha, Mwambungu alimtaka kufuata utaratibu wa kusajili huduma hiyo ili ikubalike kisheria sambamba na kupata uhakika wa usalama wa dawa kwa watumiaji.

  “Hili jambo ni kubwa hasa kutokana na kuwapo mkusanyiko hapa nyumbani kwako … Serikali lazima iingilie kati ili kuangalia hali ya usalama sambamba na dawa kuangaliwa iwapo haina madhara kwa watumiaji wake … usalama wa watu wenyewe na wako pia kutokana na idadi ya watu utakaowapata, “ alisema Mkuu wa Wilaya.

  Mwambungu pia alitumia nafasi hiyo kumwagiza Mganga Mkuu kushirikiana na Senga kuwezesha sampuli ya dawa yake kufanyiwa uchunguzi kabla ya kuendelea na tiba ili kujiridhisha kama haina madhara na kusajili shughuli yake hiyo mpya ya kutibu.

  Pamoja na Mkuu wa Wilaya kutoa msimamo huo, akiwa nyumbani kwa Senga, makundi ya watu wenye matatizo mbalimbali walikuwa wakimiminika kupata kikombe kutoka kwa dada huyo, aliyesema kwa siku hiyo alichemsha zaidi ya lita 25 kwa ajili ya wagonjwa.

  Kuibuka kwa Senga kunafanya idadi ya waliojitokeza kutibu kwa ‘kikombe’ kufikia wanne, kinara wao akiwa Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwaisapila wa Kijiji cha Samunge, Loliondo, Ngorongoro ambaye bado anakubalika zaidi ndani na nje ya nchi.

  Wengine waliojitokeza ni Jaffari Willina (17) wa Mbeya, Hillary Kitwai wa Rombo, Kilimanjaro na Margareth Mutalemwa wa Urban Quarter, Uzunguni, Tabora.

  Naye Lucas Raphael, anaripoti kutoka Tabora, kwamba Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Tabora, Mhashamu Paul Ruzoka, amesema Kanisa halina mpango wa kuzuia utoaji tiba ya magonjwa unaofanywa na muumini wake Margareth Nestory.

  Askofu Ruzoka, alitoa kauli hiyo juzi mjini humo, alipozungumzia kuibuka kwa tiba ya magonjwa mbalimbali inayofanywa na mwanamama

  huyo ambayo imevutia mamia ya watu wa ndani na nje ya Tabora. Askofu alisema anachokifanya mama huyo kinaweza kuwa kimetoka kwa Mungu, kwani tiba ya mitishamba ilishawahi kufanywa na manabii ikiwa ni pamoja na Nabii Musa akitumia fimbo (mti) kukata maji baharini na majani kuponya watu.

  Alisema kutokana na karama hizo, hawezi kukataza tiba hiyo ila kuangalia mafanikio yake na
  historia ya mwumini huyo tangu alipozaliwa hadi hatua hiyo, ambayo leo hii inamfanya awe maarufu.

  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk. Leslie Mhina, alisema kinachoweza kufanyika kitaalamu ni kuipima dawa hiyo, kujua kama inafaa kwa matumizi ya binadamu au la na baadaye kujua aina ya kemikali iliyomo na jinsi inavyotibu maradhi mengi katika mwili wa binadamu.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Mwambungualitoa agizo hilo hivi karibuni kwa maelezo kwamba,  kutokana  na ukweli kuwa anahudumia idadi kubwa ya watuni vyema  akasitisha  kwanza huduma hiyo kwa mudaili kuwezesha wataalamu kuchukua  sampuli  ya dawa hiyo ili ifanyiwe kwanza uchunguzi.  
  Hivi masuala ya kiimani kweli tunavyo vipimo vyake? Mbona yule wa Loliondo hawakusitisha ila aliendelea na huduma halafu vipimo vya kiusalama vilifuata baadaye?
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Mwambungualitoa agizo hilo hivi karibuni kwa maelezo kwamba,  kutokana  na ukweli kuwa anahudumia idadi kubwa ya watuni vyema  akasitisha  kwanza huduma hiyo kwa mudaili kuwezesha wataalamu kuchukua  sampuli  ya dawa hiyo ili ifanyiwe kwanza uchunguzi.  
   
  Mwanamke huyomzaliwa wa MzengaPwani ambaye kwa sasa anaishi Kata  ya  Kichanganimjini hapa amedai kuoteshwa na Mungu kutumia mizizi  minne  ya miti shamba kutibu wagonjwa kwa kuwatoza Sh 200 kwa kikombena   sehemu ya fedha hizo kupelekwa msikitini.  
   
  Akizungumza nyumbani kwa ‘Dada wa Kikombe', Mwambungu alifafanua  kuwa,  yeye na viongozi wa Manispaa ya Morogoro, hawakwenda kuzuia utoaji   huduma hiyo, bali kujiridhisha kwanza.  
  Aya ya kwanza naya tatu zinapingana zenyewe.........kama umemsimamisha kwa muda au kwa vyovyote vile ni kuwa umemsimamisha huwezi tena ukasema nia siyo kumzuia asiendelee kutua huduma wakati hawezi tena kuendelea kutoa huduma hadi pale atakaporuhusiwa tena................................Are we not masters of doublespeak?
   
 4. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mwaka wa vikombe huu jamani,

  eti askofu ruzoka naye kaamua kutoka kama askofu laizer! hahah..duh! viongozi wa makanisa wageuka vipofu wakuu, na kipofu akimwongoza kipofu mwingine sote tunajua wote wawili huishia shimoni

  tena huyu ruzoka ndiye kipofu mkubwa kabisa. hapo kwenye red anasema "atangalia mafanikio yake na historia ya mwumini huyo tangu alipozaliwa hadi hatua hiyo"! askofu mzima hajui kuwa anapaswa kuangalia neno la Mungu pekee. yaani yeye akishajiridhisha kuwa historia ya muumini wake sio mbaya basi tayari ni karama ya Mungu? tunazipima roho kwa historia za watu au neno la Mungu? kwa kweli kama wachungaji ndio hawa! Mungu na atuhurumie sana!

  tusijidanganye wala kudanganyika kirahisi hivi, ni neno la Mungu pekee ndilo litakalotuweka huru

  mbarikiwe wapendwa

  heri na mtakatifu ni yule mwenye sehemu yake katika ufufuo wa kwanza
  juu yake huyo kuzimu na mauti havina nguvu
   
Loading...