Waziri2025
Senior Member
- Sep 2, 2019
- 148
- 379
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro amemfanyia umafya wa hali ya juu mwanasheria Msomi na wakili wa kujitegemea, Edmund Ngemela kwa kosa la kumtetea mwajiri sakata la wafanyakazi wa Hotel ya Ngurdoto.
DC Muro alifika katika hotel hiyo na kuzungumza na wafanyakazi ambao baadhi yao walipatiwa barua ya kupunguzwa kazi,na baada ya kuwasikiliza alimtaka wakili huyo kueleza undani wa sakata hilo.
Hata hivyo Muro alionyesha kutoridhika na maelezo ya wakili huyo na baada ya kumalizika kwa kikao hicho alimwamuru wakili huyo kuongozana naye hadi kituo cha polisi USA River.
Baada ya kufika DC Muro alimpeleke kaunta ya Polisi na kumwagiza askari waliokuwepo hapo kumweka ndani hadi hapo atakapojisikia kumtoa.
Hata hivyo wakili huyo baadaye aliwasiliana na wanasheria wenzake na kuweza kutoka mahabusu baada ya Masaa kadhaa kusota Lukapu .
DC Muro alimtaka mwanasheria huyo kusitisha barua za kuwafukuza kazi wafanyakazi 50 wa hotel hiyo ,huku Wakili Ngemela akimwambia DC huyo kwamba hana mamlaka ya kisheria ya kuamuru mwajiri kutomfukuza mfanyakazi wake ila mwenye mamlaka ni tume ya usuluhishi (CMA) ama mahakama.
Wakili Ngemela anaitetea kampuni ya Ngurdoto katika kesi ya madai ya wafanyakazi walioipeleka mahakamani hotel hiyo wakidai malimbikizo ya mshahara.