DC amfukuza kazi Mganga wa zamu kwa uzembe kazini baada ya kukataa kumtibu Mtoto wa miezi 6

BADO MMOJA

JF-Expert Member
Jul 19, 2012
2,196
1,338
Habari kutoka wilaya ya Bukombe zinaeleza kuwa Tabibu wa zamu Johaness Makobwe katika hospitali ya wilaya ya Bukombe amekataa kumtibu mgonjwa aliyefika hospitalini hapo usiku wa kuamkia leo kwa madai kuwa amechoka hivyo mgonjwa huyo aje asubuhi.

Bila kujali ana hali gani, habari zaidi zinaeleza kuwa ndugu wa mgonjwa walimpigia simu mkuu wa wilaya usiku huo huo na DC alikwenda kumuamsha Medical Officer Incharge wakaenda naye hospitalini hapo na kuthibitisha madai ya ndugu wa mgonjwa kisha DC akamfukuza kazi palepale.

Mara baada ya kumfukuza, MO i/c alianza kumtetea Tabibu yule mpaka sasa haijajulikana kama kweli tamko la DC litatekelezwa au DC atashindwa nguvu na MO I/C. Ngoja tusubiri

==================

MKUU wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, Amani Mwenegoha, amemfukuza kazi Dkt. Johanes Makobwe, aliyekuwa zamu wa Hospitali ya Wilaya ya Mjini Ushirombo mkoani Geita usiku wa kuamkia leo kwa uzembe na kukataa kumtibu mtoto mwenye umri wa miezi 6.

Mwenegoha ameiambia FikraPevu amechukua hatua hiyo ili iwe funzo kwa waganga na wauguzi wengine wanaofanya manyanyaso ya kupokea rushwa na kunyanyapaa wagonjwa Hospitalini hapo.

Mkuu huyo amesema alipofika Hospitalini hapo saa kumi na mbili asubuhi alimkuta mganga huyo akiwa amelala ndipo akampigia simu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dkt. Maja Susuma, aliyefika na kumpatia matibabu mtoto huyo mwenye umri wa miezi 6.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari ndani ya hospitali hiyo vinaeleza kuwa Mkuu huyo wa wilaya amechukua hatua hizo baada ya kupigiwa simu na wazazi wa mtoto aliyefikishwa Hospitalini hapo saa kumi za usiku ili kupatiwa matibabu lakini mganga wa zamu alikataa kumtibu.

Sababu zinazotajwa kuwa ndizo zilizosababisha mganga huyo kutomtibu mgonjwa huyo ni madai aliyoyatoa kuwa Mganga ambaye angeingia zamu asubuhi ndiye ambaye angepaswa kumhudumia mtoto huyo.

Chanzo chetu cha habari kimedokeza kuwa, mhudumu huyo wa afya anatuhumiwa kwamba alikuwa amekwenda kuangalia mpira wa mechi ya ligi kuu kati ya Real Madrid C.F na F.C Barcelona iliyochezwa jana usiku Novemba 21, 2015.

Soma zaidi =>Mganga wa zamu afukuzwa kazi kwa uzembe, Ni baada ya kukataa kumtibu Mtoto wa miezi 6
 
Kazi hii si wito tena ni wajibu wa mfanyakazi! Hata waalimu nako watawajibika ila mishahara yao iongezwe
 
Wangempa nafasi hy Tabibu kujitetea maana ninavyojua kama mtu mwenye fani hy akiwa amechoka basi kutibu kwake kuna mashaka na kunaweza leta athari kwa mgonjwa, pia sijui.ni sheria ipi inampa mamlaka mkuu wa wilaya kumfukuza kazi mtumishi wa serikali. Maana hy tabibu ni mwajiriwa wa mkurugenzi
 
Walipoambiwa hapa kazi basi watatoa amri ambazo hazitekelezeki ili mradi waonekane na wao wamo kwenye msafara wa mamba
 
Habari kutoka wilaya ya Bukombe zinaeleza kuwa Tabibu wa zamu Johaness Makobwe
katika hospitali ya wilaya ya Bukombe amekataa kumtibu mgonjwa aliyefika hospitalini hapo usiku wa kuamkia leo kwa madai kuwa amechoka hivyo mgonjwa huyo aje asubuhi, bila kujali ana hali gani, habari zaidi zinaeleza kuwa ndugu wa mgonjwa walimpigia simu mkuu wa wilaya usiku huohuo na DC alikwenda kumuamsha Medical Officer Incharge wakaenda naye hospitalini hapo na kuthibitisha madai ya ndugu wa mgonjwa kisha DC akamfukuza kazi palepale lakini MO i/c alianza kumtetea Tabibu yule mpaka sasa haijajulikana kama kweli tamko la DC litatekelezwa au Dc atashindwa nguvu na MO I/C. Ngoja tusubiri CHANZO: MFANYAKAZI WA HOSPITALI WILAYA YA BUKOMBE

Atimuliwe tu na faili lake lipelekwe kwa DPP kuona kama kuna jinai apandishwe kizimbani haraka.
 
Kuna MD(Medical Officers) wengi tu mtaani hadi leo, serikali inaendelea kuchezea afya za wananchi na Clinical Officers, kwanini wasipate viburi na kujiona miungu?
 
Maadili!! Maadili!! Hii kada ya C/O kwenye tiba ni shida. Hawana maadili,ni ngumu sana kushtakiwa kwani hicho cheo haitambuliki W.H.O. Hawa jamaa hawana kiapo cha kazi yao,wanapitwa na wauguzi ambao huapa,na kuahidi kuishi kiapo chao. Wengi wao wamesaidia Sana kutibu vijijini(miaka ya 90 kurudi nyuma),ila hawa wa BRN ni shida tupu. Huyo aliyekataa kumtibu mgonjwa huenda alikuwa tungi.
 
Hiyo issue imejaa utata sana, kwa sababu.
1/Mkuu wa wilaya hana haki wala mamlaka ya kumfukuza kazi mtumishi yoyote yule wa serikali. Mkuu wa wilaya hana mamlaka ya kuajiri hivyo hana mamlaka ya kumfukuza kazi mtu ambaye hajamwajiri yeye.

2/Kimaadili Daktari haruhusiwi kukataa kumtibu mtu lakini pia halazimishwi kumtibu mtu.

3/Kama Daktari amechoka hapaswi kumtibu mtu kwa sababu ni hatari sana. Ni sawa na Dereva anasinzia alazimishwe kuendesha gari barabarani.

4/Kanuni za Afya zinatamka kuwa mhudumu yoyote wa Afya anapotuhumiwa kukiuka masharti ya taaluma yake basi Shauri hilo lipelekwe kwenye baraza la taaluma yake husika na huko ni lazima asikilizwe kabla ya kuhukumiwa.
 
Huyo DC ni mjinga tu.

Tabibu ana idadi ya watu anaotakiwa kutibu kwa siku.

Bongo hii misaada wanatotoa wataalam wetu kutibu hovyo imewapumbaza sana watu ona sasa DC analeta siasa kwenye taaluma.

Utamfukuzaje kazi mtu hujamwajiri?

Dc hajui kwamba kuna bodi na ofisi za kupeleka malalamiko yake..
 
Wangempa nafasi hy Tabibu kujitetea maana ninavyojua kama mtu mwenye fani hy akiwa amechoka basi kutibu kwake kuna mashaka na kunaweza leta athari kwa mgonjwa, pia sijui.ni sheria ipi inampa mamlaka mkuu wa wilaya kumfukuza kazi mtumishi wa serikali. Maana hy tabibu ni mwajiriwa wa mkurugenzi

Keli mkuu umeongea vyema. Mtu kasema kachoka we unalazimisha, akitibu jicho badala ya tumbo tunakuja kujadili uzembe. Binafsi namuunga mkono kukataa.
 
Huyo DC ni mjinga tu.

Tabibu ana idadi ya watu anaotakiwa kutibu kwa siku.

Bongo hii misaada wanatotoa wataalam wetu kutibu hovyo imewapumbaza sana watu ona sasa DC analeta siasa kwenye taaluma.

Utamfukuzaje kazi mtu hujamwajiri?

Dc hajui kwamba kuna bodi na ofisi za kupeleka malalamiko yake..

DC ana mamlaka ya kumsimamisha kazi mtumishi wa umma wakati hatua za kinidhamu zikichukuliwa, na mara nyingi utapigwa chini tu.
 
Hata hivyo hospitali nyingi za wilaya ma CO's ndio wanapiga sana kazi na MD Ni kuzunguka tu wakishasaini wanaenda kufanya yao,na hilo nalo liangaliwe sio lawama tu
 
Tuna Mwaka mzima wa majungu na fitna,kama MTU ana bifu na wewe sasa hivi anakupikia maneno
 
Wangempa nafasi hy Tabibu kujitetea maana ninavyojua kama mtu mwenye fani hy akiwa amechoka basi kutibu kwake kuna mashaka na kunaweza leta athari kwa mgonjwa, pia sijui.ni sheria ipi inampa mamlaka mkuu wa wilaya kumfukuza kazi mtumishi wa serikali. Maana hy tabibu ni mwajiriwa wa mkurugenzi

Good idea,ni kweli kabisa kazi km Utabibu,ualimu,Engineering,Urubani,n.k.zinahitaji sana Utulivu wa akili vinginevyo unaweza ukakoroga mambo.
 
MO asitutanie huyo tabibu Hana jipya tuliposema hapa kazivhatukuwa na Utani akatulie na familia yake tuajili mwingine mwenyewe kupenda Kazi
 
Back
Top Bottom