Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi kwanza nichukue nafasi hii kukupongeza kwa uchapakazi wako. Ni DC usiyependa kukaa ofisini unachapa kazi tu. Niliipenda ile style yako ya kujifanya mgonjwa pale Mwananyamala na juzi juzi ukavalia kimgambo. Big up!
Lakini leo nimeona kwenye vyombo vya habari kuwa katika wilaya yako kuna msako wa madanguro na nyumba za kulala wageni zote ili kuwabaini watu wanaojihusisha na vitendo vya ngono.
Mm nakushauri kuwa uachane na zoezi hili kwa sabb zifuatazo.
1. Ni vigumu kuyabaini madanguro na kuyatolea ushahidi wa kisheria ili kuthibitisha kuwa ni madanguro. Kama ilivyo kwa makahaba. Katika nchi yetu biashara ya ukahaba na madanguro haitambuliwi kisheria na ni batili. Hivyo mhusika aliyemo kwenye danguro anaweza akajitetea kwa kupachika kazi nyingineyo yoyote halali ktk nyumba hiyo. Maana haijasajiliwa kama danguro.
2. Nyumba za kulala wageni nyingi zimesajiliwa na zinatambuliwa kisheria kwa kazi ya kulaza wageni. Watu 2 waliokubaliana kwenda kufanya ngono katika nyumba hiyo ya wageni hawawezi kikubali kunaswa na mkono wa sheria kwa kukubali kuwa walikuwa wakifanya ukahaba. Watahalalisha kwa kujifanya ni wanandoa wasafiri.
Mm nikuombe ushughulike na matatizo makubwa yanayo wakabili wanakinondoni kama vile ukosefu wa ajira, ukosefu wa masoko, uchafu, foleni, n.k.
Naomba utambue kuwa wengi wa watu wanaofanya ukahaba hawafanyi kwa kupenda. Wengi wao ni kutokana na changamoto za kiuchumi.
NAWASILISHA.