DC akabidhi hundi ya Mil. 626 kwa vikundi 100 Arusha, ampigia Debe Rais Magufuli

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
MKUU wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro amekabidhi hundi ya zaidi ya Sh.milioni 626 kwa vikundi 100 vya watu wenye ulemavu,wanawake na vijana ili waendelee kufanya biashara zao bila kukwama

Akikabidhi hundi hiyo mapema leo jijini Arusha,alisema fedha hizo zinatokana na mapato ya fedha za ndani za jiji la Arusha na kuwataka wanavikundi kutomsahau Rais John Magufuli katika uchaguzi ujao kwani mambo haya makubwa anayafanya kwa ajili yenu

"Uchaguzi ujao naomba tushikamane na Rais Magufuli tumuunge mkono na wakati wa kupiga kura angalia nguo ya kijani weka tiki" amesema Dagarro

"Mikopo hii zamani watu walikuwa hawazipati lakini kutokana na Rais John magufuli kusema asilimia hii ipelekwe kwa watu wake ndio maana halmashuri zinatenga na kuwapa wahusika hao,"alisema

Aidha alisema fedha hizo ziliombwa na vikundi 109, lakini tisa kati ya hivyo hazijapata sababu wamekosa sifa, hivyo aliomba wahusika wa mikopo waelekeze vikundi hivyo ili waendelee kufanya vizuri na awamu ijayo vipewe kipaumbele.

Aliwataka wanakopeshwa fedha hizo ziwasaidie kukua kiuchumi kwa kupiga hatua katika biashara zao na kuepuka kuzipeleka kwenye matumizi yasiokusudiwa.

Pia aliwataka Maofisa Maendeleo Kata kusimamia vizuri vikundi hivyo pamoja na kuelekeza aina za biashara za kufanya amabzao zitawazalishia fedha badala ya kuvitelekeza.

"Naomba pia awamu ijayo tuone vikundi vingi zaidi vya watu wenye ulemavu na tusiwabague ili nao wanufaike na mikopo hiyo na wengi wakisaidiwa wanaachana na omba omba na wanauwezo wa kufanya biashara,"alisema.

Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Mwanamsiu Dossi, alisema fedha hizo zimetokana na urejeshaji wa zaidi ya Sh.milioni 122.2 wa vikundi vilivyokopeshwa na zaidi ya Sh.milioni 504.6 zimetokana na fedha za mapato ya ndani.

Alisema mikopo hiyo iliyotolewa zaidi ya Sh.milioni 626.8 kati ya hizo Sh.milioni 377 zimetolewa kwa vikundi 65 vya wanawake,Sh.milioni 234.866 vikundi 32 vya vijana na Sh.milioni 15 vikundi vitatu vya watu wenye ulemavu.

Alisema halmashauri itaendelea kutoa mikopo hiyo kadiri itakavyokuwa ikitolewa maombi kutoka kwenye vikundi kulingana na fedha zitavyopatikana kutokana na makusanyo ya mapato ya ndani na marejesho ya mikopo ya nyuma.

Mkurugenzi wa Halmashuri ya Jiji la Arusha Dk.Maulid Madeni amemwomba Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro kuongeza kiwango cha fedha za kukopesha kwa walengwa hao ili ziwasaidie kufanya biashara.

"Sio lazima tuwape fedha tunawezabkuboresha kwa kununua mashine za kufyatulia tofauti vijana na akna mama wapewe mashine za kushona nguo wakaongeza kipato kwa bidhaa watakazozalisha,"alisema.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Denisi Zakaria amevitaka vikundi vya wanawake,vijana na walemavu wanaokopeshwa fedha na serikali wazirejeshe kwa wakati ili wenzao wapate.

Alipongeza Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa kuhakikisha asilimia kumi ya mapato yake ya ndani wanawapa makundi hayo tofauti na halmashutinzingine nchini wanazitenga na kuzifanyia kazi zingine nje ya ilivyokudiwa.

"Lakini sababu sisi CCM tuwakuna kwa kuwapa fedha za mikopo nanyi mtukune wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu,"alisema.

Ends...


IMG_20200609_114122.jpeg
 
"Lakini sababu sisi CCM tuwakuna kwa kuwapa fedha za mikopo nanyi mtukune wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu,"alisema.

Kumbe ndiyo lengo la mkopo!!?
 
Lakini sababu sisi CCM tuwakuna kwa kuwapa fedha za mikopo nanyi mtukune wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu,"alisema.
Ngoja mkunane ila hii pia Ni kampeni mmeanza. Muwe makini na kampeni zenu hizi za kuwalagai wananchi huku wanaolipa mapato ya halmashauri na wananchi wote.
 
Back
Top Bottom