DC aendesha ibada ya mazishi ya polisii!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DC aendesha ibada ya mazishi ya polisii!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ms Judith, Apr 24, 2011.

 1. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  IGP Mwema atema cheche

  [​IMG] Makamanda wa wilaya zote kufundwa
  [​IMG] Serikali za mitaa wakae `mkao wa kula`
  [​IMG] DC ajitosa kuendesha ibada ya mazishi  [​IMG]
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema, akitoa heshima za mwisho mbele ya mwili wa ofisa wa Polisi, Joseph, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwake wilayani Nkasi mkoani Rukwa jana.


  Siku chache baada ya wananchi wa kijiji cha Mwakashahala kata ya Puge wilayani Nzega, mkoani Tabora, kumuua askari polisi mwenye namba E6530 Joseph Millinga.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi, Jenerali Said Mwema, ametema cheche na kusema kuwa makamanda wa polisi wa wilaya zote nchini wanakutana mjini Dodoma kuandaa mkakati wa kuimarisha ushirikiano baina yake na wananchi.
  Alisema lengo ni kujenga ushirikiano wa dhati baina ya jeshi hilo, serikali za mitaa na wananchi kwa ujumla ili kujenga uwanja mpana wa upatikanaji wa haki pindi wananchi wanapokwenda polisi.
  Akizungumza baada ya mazishi ya marehemu Millinga yaliyofanyika katika kisiwa cha Manda Kerenge kilichopo katika kata ya Kirando wilayani Nkasi mkoani Rukwa, IGP Mwema alisema hatua hiyo inakusudia pia kupunguza kasumba ya baadhi ya wananchi kujichukulia sheria mkononi.
  Aliongeza kwamba jeshi la polisi limeweka mikakati endelevu ya kulinda maisha ya wananchi na mali zao ikiwa ni pamoja na kupambana na vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na baadhi ya watu wanaojifanya kuwa na hasira kali na kuvunja sheria za nchi.
  Alisema kuwa "ni kifo cha kusikitisha kilichomkumba kijana wetu akiwa katika kulinda usalama wa wananchi kutokana na madhara makubwa yanayowapata wananchi wengi mara baada ya kutumia madawa hayo ya kulevya aina ya bangi sasa jeshi likitaka kuokoa maisha ya wananchi na wananchi wenyewe wanakatisha uhai wa askari wetu jamani tutafika wapi kwa hali hii?...juzi tu nimepata habari juu ya msiba mwingine uliotokea katika kijiji cha Miombo katika wilaya yenu ya Nkasi huku Tabora nako wakamuua askari wetu."
  Alikumbusha kwamba "hakuna jambo lolote linaloshindikana katika sheria hivyo kama kuna mtu anaona hakufuata utaratibu basi jitahidini kufuata utaratibu wa kisheria kuanzia ngazi ya mtaa, kijiji kata wilaya mkoa na hata taifa na si kujichukulia sheria mikononi."
  Hata hivyo, katika hali isiyokuwa ya kawaida, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Joyce Mgana, amelazimika kuendesha ibada ya mazishi, baada ya Kanisa Katoliki kukataa kumzika marehemu huyo kwa maelezo kwamba hakuwa anatimiza masharti ya kikanisa wakati wa uhai wake.
  Mgana na mbunge wa jimbo la Nkasi Kaskazini, Ally Keisy nao walitoa hisia zao juu vitendo vya uhalifu vinavyoendelea kutokea katika maeneo mbalimbali nchini na hususani katika wilaya hiyo ya Nkasi, huku msemaji wa familia akiomba nafasi zaidi ya ajira kwa vijana waliobakia katika kisiwa hicho cha Manda Kerenge.
  Marehemu Milinga aliuawa Aprili 20, mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi baada ya wananchi wa kijiji cha Mwakashanhala kata ya Puge wilayani Nzega mkoani Tabora, kuwashambulia askari waliokuwa wakifanya msako wa kuwakamata watu wanaolima bangi.
  Jeshi la polisi limetuma kikosi maalum cha Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU) zaidi ya 60 kinachoongozwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Liberatus Barlow, kwenda kijijini hapo kuwasaka watu waliohusika katika mauaji hayo.
  Marehemu Millinga ameacha mjane na watoto watatu.


  http://www.ippmedia.com/
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Poleni sana makamanda wetu mimi naangalia upande wa pili wa jeshi,nadhani askari wetu watakuwa wana bima ya maisha kwa kazi wanazofanya kama bado naomba sana vyombo husika wawasaidie maana najua hawana vyama vya wafanyakazi!!!watakaoteseka ni wajane na watoto wao!!!!inauma sanaaa
   
 3. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Skills4ever....Kweni Askari anayetoroka kituo chake cha kazi na kwenda kuomba rushwa toka kwa mkulima wa Bangi ni halali kulipwa Bima? Oparation gani ya polisi isiyoandikwa au kuratibiwa na wakubwa wa Polisi? Kwa nini askari wa Nzega walihusika na sio askari wa kituo cha Puge? hivi siku hizi Oparation za Polisi hutumia pikipiki na sio gari? je kweli ni kawaida kwenda mkamata mjasiriamali wa shamba la Bange mkiwa wachache hivyo tena nasikia bila ? kwanini askari hao hao inasemekana walionekana mara kadhaa (frequency ilizidi karibia ya Pasaka) kijijini hapo na hakukuwa na tukio baya hapo nyuma? kwa nini viongozi wa kijiji hawakupewa taarifa ili wajulikanike ujio wao? IGP Mwema jaribu kututendea haki kwa kutupatia sababu ya msingi kuhusiana na kifo kile ili askari wengine wasije tumbukia katika janga kama lile, kule mwakashahala na iwe shule kwa wengine pia kumbukeni kuwa binaadamu wengi ni wapole kama paka lakini binaadamu huyo huyo anapoona sasa hamna jinsi basi huamua kujinasua kwa namna yoyote ile kama vile paka anavyofanya anapozidiwa,
   
 4. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Ni muda mfupi sana umepita tokea tukio la askari wawili kuuawa kwa kile kilichoitwa "uzembe" ktk kituo kidogo cha Kabongwa Kahama...iliniuma sana..si kwa kua mmoja wa Marehemu hao alikua kaka yangu (Salimu Mwanakatwe) bali kwa kua walikua na haki ya kuishi na kifo chao kilitokea ghafla mno katika mfumo ambao ni wa kusikitisha sana!...Naam na sasa wameuawa wengine Nzega! Kuna maswali marahisi najiuliza hapa....

  • Jeshi la polisi linajifunza nini katika matukio haya?
  • Kuonesha itifaki (ya mavazi) wakati wa msiba inatosha kuwafariji ndugu wa wapendwa wetu?
  • Kwanini askari wenye sifa za kushughulikia uhalifu mikoa korofi wapulizwe tu na viyoyozi ofisini kwa vyeo vya kupeana ilihali ndugu zetu 'wasio na watu" juu huko wakiendelea kupoteza maisha kila kukicha?
  • Ni funzo gani wanapata vijana wadogo wenye moyo wa kuitumikia nchi yao ilihali kila siku wanaona na kusikia tukio la askari kuuawa ambapo reward yake ni kupigiwa tu saluti na uliokua unawapigia enzi za uhai wako?
   
 5. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  HII KALI KUMBE madc nao wanaujua uchungaji, kama kweli mtu yuko nje ya usharika au hajumuiki na wakristo wenzake huwa hawamziki lkn mungu ndio anaejua matendo yake huyu marehemu.
   
 6. chipanga

  chipanga JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 661
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 60
  Hiyo imekaa vby, judge not... i hope sk 1 kanisa litabadika.
   
 7. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #7
  Apr 27, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  People!
  Anagalieni outcry ilivyokuwa kubwa baada ya kifo cha askari! Na hii si mara ya kwanza. Pale askari anapo/wanapokufa kwa kuuwawa kelele zinazotoka kwa Makamanda wao na viongozi wengine ni balaa! Maana wao kuuwawa ni mwiko ingawa hata kazi zao zinawaweka katika mazingira ya hatari ya kuuwawa. Ni lini mlisikia hao Makamanda wakilaani vikali mauaji ya raia wa kawaida? Watu wema tu huuwawa kila kesho kutokana naubovu wa usalama wa raia ambalo ni jukumu la jeshi la mapolisi lakini hilo huchukuliwa kama jambo la kawaida tu. Huo ndio mukuki kwa nguruwe!
  Sitetei mauaji yawe ya raia au askari lakini napata kichefuchefu ninapomwona kiongozi wa Jeshi la Polisi eti anatema cheche baada ya kufa askari wake! Awaulize wananachi wa maeneo mbalimbali waliopoteza ndugu na marafiki kwa mauaji ya uonevu tu kama yale ya uwekezaji kwenye migodi n.k., uchungu walio nao na kama huyo Kamanda alitoa hata salaam tu za pole kama sio kuahidi kufuatilia kwa juhudi zote uovu wa aina hiyo!
  Ni aina ya watu kama hawa huyo KAMANDA na watu wake ambao upeo wao wa kutafakari umezibwa na ubinafsi kiasi cha kusahau kuwa watu wote ni sawa na wanastahili ulinzi wa askari wanaolipwa kwa kodi ya Watanzania!
  Watuondokee na ubaguzi wao!
   
 8. B

  BENTA Member

  #8
  Apr 27, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nakubaliana na Mavumbi raia wengi wasio na hatia wamefia mikononi mwa polisi sehemu mbalimbali lakini hakuna hatua madhubuti zilizochukuliwa hivyo iwe ni somo kwa yeyote kwani wananchi wanaanza kuchoka na hii ni mwanzo tu.
   
 9. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Poleni wafiwa, rip marehemu, hasira iliyojengeka kwenye jamii inazalishwa na wavunja katiba (chama tawala na serikali yake) kwa kuwalipa watumishi wa serikali malipo yasiyostahili(hayakidhi mahitaji ya mwezi) kwa masikio yangu nilimsikia mwajiriwa mkuu wa mwananchi(rais) akituambia hatalipa mishahara inayostahili, watakaoshinikiza wajiandae kupigwa risasi, tusishangae sana kwani viongozi wetu hawajui wanawajibika kwa nani, wamewaacha watumishi wa umma kujitafutia mapato kuziba nakisi ya bajeti zao kama kuku wa kienyeji. Tuna safari ndefu
   
Loading...