DAWASCO yamjibu Mnyika, Midalla aeleza kushangazwa na atoa siri ya chanzo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DAWASCO yamjibu Mnyika, Midalla aeleza kushangazwa na atoa siri ya chanzo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Habarindiyohiyo, Feb 24, 2012.

 1. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2012
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  KAMPUNI ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASCO), na Mbunge wa Jimbo la Ubungo John Mnyika, wanatarajia kufanya ziara katika baadhi ya maeneo ya jimbo hilo ili kubaini maeneo yenye matatizo ya upatikanaji wa maji.

  Akizungumza na gazeti hili Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Jackson Midalla, alisema ziara hiyo iliyoombwa na Mnyika itafanyika kati ya Machi mosi hadi Machi 3 mwaka huu katika maeneo ya Kwembe, Saranga, Msigani, Makuburi, Sinza na Makurumla.

  Midalla alisema hayo wakati akijibu taarifa ya Mnyika aliyoitoa kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Facebook dhidi ya Dawasco. Mbunge huyo alisema kampuni hiyo imekiuka mikataba miwili inayoongoza kazi zake na hivyo kusababisha matatizo ya upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar es Salaam.

  Katika taarifa hiyo, Mnyika alisema Dawasco imeshindwa kuchukua hatua za kutatua matatizo ya maji katika maeneo mbalimbali sambamba na kutozingatia ratiba ya mgawo wa maji.

  Alisema mara ya kwanza alitumia taratibu kwa kuiandikia barua Dawasco kuhusu tatizo la upatikanaji wa maji Septemba mwaka jana na mara ya pili ni Februari 14 mwaka huu. Kwa mujibu wa Mnyika, majibu ya matatizo hayo hayajapatiwa ufumbuzi.

  Mbunge huyo aliitaka Dawasco ifanye ukaguzi wa mtandao wa maji, kurekebisha kasoro zilizopo na kutoa taarifa kwa umma kuhusu matatizo ya maji yanayoendelea katika maeneo mengi ya Jiji la Dar es Salaam ikiwemo Jimbo la Ubungo.


  Alitaja baadhi ya maeneo yanayopaswa kutembelewa kuwa yapo kata za Makuburi, Kimara, Saranga, Mbezi Luis, Msigani, Kwembe, Goba, Kibamba, Sinza, Makurumla, Mabibo, Manzese, Ubungo na Mburahati Hata hivyo akiendelea kutoa ufafanuzi juu ya taarifa hiyo ya Mnyika, Midalla alihoj.i

  “Nimeshangazwa na maneno ya Mnyika, alituletea barua kuomba sisi na yeye tufanye ziara hiyo, leo amesema kuwa ametupa siku tatu kutoa majibu ya tatizo la maji, kauli ipi ni ipi ?” alihoji Midalla.

  Aidha alisema matatizo ya maji yanayoyakabili baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam yanatokana na kuharibika kwa pampu moja kati ya tatu za kusukumia maji iliyopo Ruvu na kuongeza kuwa mafundi wapo katika matengenezo na wakati wowote hali inaweza kutengamaa.

  HabariLeo | Mnyika, Dawasco kutembelea jimboni Ubungo
   
 2. M

  MWananyati Senior Member

  #2
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 155
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Nafikiri wote wawili Mbunge na Afisa wa DAWASCO mpo sahihi. Maji ni kero kubwa sana kwa baadhi ya maeneo hapa dar japokua na kisingizo cha kuharibika kwa mashine.

  Mfano kwa maeneo yetu ya Golani-Msewe, maji ya DAWASCO ni historia. pamoja na kuweka mtandao wa mabomba ya wachina, hakuna lolote wala chochote kwa zaidi ya mwaka mzima.
  Hii lakini inachangiwa pia na hujuma zinazofanywa na wafanyakazi wa dawasco kwenye kitengo cha mgawanyo wa maji. wamehongwa na wafanyabiashara wa kuuza maji kwa ma-boza.hivyo maji yanafungwa kwa makusudi ili kunufaisha biashara zao za maji. Ni ushenzi huu, twaomba ukomeshwe sababu dawasco wenyewe wanahusika katika mchezo huu.

  TWASUBIRI MATOKEO YA HIO ZIARA AMBAYO MMEIPANGA MBAAALI WAKATI MNAJUA TATIZO LA MAJI NI KUBWA NA WATU TUNATAABIKA.
   
 3. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo la maji Dar es Salaam ni sugu, na huwezi leo kusema eti ni kwa sababu ya uhalibifu wa pump ambao pengine umetokea siku mbili tatu zilizopita. Hapa uhalisia ni kwamba hakuna uwajibikaji kuanzia uongozi wa juu wa serikali hadi wa DAWASCO. Hakuna nia njema ya kutatua kero ya maji siyo Dar es Salaam tu bali pia katika sehemu zingine za nchi.
   
 4. s

  shujaa Member

  #4
  Feb 24, 2012
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Dar Haijawahi kuwa na maji waache kuongopea watu, ila baadhi tu ya maeneo kama Mikocheni Kawe nk
   
 5. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ufisadi ndo unafanya miundo mbinu imara ya kukidhi Demand ya DAR isitengenezwe.Hakuna kipaumbele katika masuala ya maji toka serikalini kama ilivo kwa sekta nyingine.Lawama ziende kwa serikali
   
 6. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #6
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Nadhani haisaidii kufanya ziara tu aende na maji kabisa
   
 7. p

  plawala JF-Expert Member

  #7
  Feb 24, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kufanya ziara kunasaidia kupata taarifa sahihi kuhusiana na changamoto na matatizo yaliyopo
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Feb 24, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mnafikiri ela za kuleta maji zitatoka wapi wakati nyie wahishimiwa wabunge mwakinga vitita vya mishahara na marupurupu ya ubunge pasipo na tangible output yeyote? Mtakula mlipopeleka mboga.
   
 9. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #9
  Feb 24, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  DAWASCO my hair
   
Loading...