Dawasco wazindua mfumo wa LUKU kwenye maji

neema shamuhenya

JF-Expert Member
May 24, 2018
312
216
Shirika la Maji safi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco) limezindua mita mpya za maji ambazo malipo yake yatafanyika kabla ya matumizi (prepaid meters).

Mita hizo zinafanya kazi kama ilivyo kwenye mita za LUKU ambapo mtumiaji atatakiwa kulipia kiasi anachotaka. Baada ya kufunga mita hizo, Dawasco watakuwa wanazifuatilia kupitia mfumo maalum wakiwa ofisini kwao hivyo hakutakuwa na ufuatiliaji wa wateja nyumbani.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Prof. Makame Mbarawa amesema mita hizo za malipo ya kabla zitasaidia kuleta nidhamu katika matumizi ya maji na kuliongezea shirika mapato.

Mita za mfumo wa LUKU kwenye maji zimeanza kwa mkoa wa Dar Es Salaam na kisha zitasambaa katika maeneo mengine ya nchi.
 
Kwenye nyumba za kupanga ni majanga kuna wapangaji wanapenda maji kama. Samaki.... Sasa wewe bachela unaoga asbh unawahi kazini kurudi kuoga tena ndoo moja wakati wenzako mchana washakichafua ndoo 100 bili inakuangukia.
Any way italeta displine ya matumizi ya maji kama kwenye umeme
 
Hamna picha yoyote?
safe_image.jpg
 
Safi sana mfumo huu uenee haraka kupunguza usumbufu wa kubambikiwa bili za maji. Mimi juzi nimeenda DAWASCO mita inasoma unit 83 toka wamefunga naambiwa nadaiwa unit 525
 
duuu inasikitisha sana lakini dawa yao ndio hiyo imefika
Unit moja ni 1679 sasa ukipigwa mara 525 maana yake unalipa 881,475 wakati hizo 83 zenyewe nilishalipia unit 58 na bili nilikuwa nazo. Yaani wale ukienda bila kusoma mita yako umeumia sasa huu mfumo utamaliza malalamiko yote kama ilivyokuwa kwa Tanesco
 
Mkuu kwani wanepandisha bei ya Unit ?
Nijuavyo mimi unit moja inacheza kwenye 1390/= hivi
 
Duuuh pole, ivi na unit moja hua Bei gan kwakwel maana wengine hua tunaletewa tu bili na kulipa tu bila kujua kiasi Cha bei ya unit moja
 
Duuuh pole, ivi na unit moja hua Bei gan kwakwel maana wengine hua tunaletewa tu bili na kulipa tu bila kujua kiasi Cha bei ya unit moja
Chukua bili upige hesabu
Jela gawanya kwa unit ulizotumia
 
Waweke nidhamu kwanza kwenye mabomba yao yanayovuja vuja barabarani. Nafikiri wanapoteza pesa nyingi zaidi.
 
Back
Top Bottom