DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

DAWASA

Official Account
Oct 7, 2010
132
79
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)

DAWASCO HUDUMA KWA WATEJA 0800110064
DAWASCO ILALA 0743 451879
DAWASCO KAWE 0743 451861
DAWASCO KIBAHA 0743 451875
DAWASCO KIMARA 0743 451865
DAWASCO KINONDONI 0743 451863
DAWASCO BAGAMOYO 0743 451877
DAWASCO MAGOMENI 0743 451862
DAWASCO TEGETA 0743 451881
DAWASCO TABATA 0743 451867
DAWASCO TEMEKE 0743 451866

IMG-20180321-WA0058.jpg
 
Je kwa nini DAWASCO hailengi kuongeza wateja wapya na badala yake inahangaika na wale wale wa siku zote? Hamuoni kuwa kuna fedha nyingi mnaziacha kwa potential customers ambao wanashindwa kupata huduma zenu kwa vile tu hamuendi kwa wananchi?

Fikiria maeneo kama Mbagala Gongolamboto, Kigamboni nk sidhani kama mmeyafikia maeneo hayo
 
Safi sana, unaona faida za mitandao ya kijamii habari kama hii mungeiweka TBC au gazeti la uhuru mimi nisingeiona, lakini kupitia JF nimeiona, hongera sana.

Sasa, muwe mna toa ushuhuda kwa viongozi wa kisiasa kuwa mitandao ya kijamii na hasa JF inasaidia sana kufikisha ujumbe kwa wananchi wengi
 
KUNA BOMBA JIPYA AMBALO LILILOPITA PEMBEZONI KWA NGUZO ZA TANESCO, LITAANZA KUTOA HUDUMA LINI KWA WANAINCHI WALIO KARINU NA BOMBA HILO?
 
asante kwa taarifa..tunaomba utuelekeze ni maeneo gani kwa pale Ubungo Terminal

Ubungo Terminal, nyuma ya stand ya mkoa kuna eneo la barabara inayotoka legho kwenda darajani kuna mabomba yanavuja. Na pale unapoanzia ukuta wa Stand ya mkoa kama unatoka legho pana bomba linamwaga maji. Pia hapo hapo ukishuka hicho kinjia chini ya Sanches Lodge kuna kimtalo kinakata kulia kunabomba kubwa limeungwa vibaya linavuja maji.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom