DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Tangu december nimekuwa nikipata bill sizielewi elewi. Lakini kwa kawaida bill ina range 15,000 - 25/30,000 kulingana na watu ninaoishi nao ndani. Sasa nashangaa leo nimeletewa bill 79,000? tena watu wamepungua sana kwangu kwa lipi? namba ni 90071710 KAwe
Sijui hili haliwahusu. Mbona sipati jibi?
 
Chanika hamna maji na sijasikia kama mna mpango wowote ule wa kuleta maji.Tunaomba mtujuze lini mtatuletea maji?
 
Zamani hapa Tandale Yemen bombs limepasuka linamwaga maji hovyo
Mmefunga barabara ya Tandale- Chama na Mwananyamala Manjunju miaka miwili sasa kwa mabomba yenuChakavu
Mnataka tufanyeje?
 
Dawasco mnakera. Eneo la Mikocheni B mbele ya 5 Star Apartment kuna shimo limechimbwa na Dawasco na lina zaidi ya mwaka na ni chanzo cha ajali usiku. Kwa nini wachimbe mashimo kwa ajili ya kurekebisha mifumo ya maji na kujisahaulisha? Mimi nina mwaka wa pili sipati tena sms ya bill ya maji, why Dawasco?
 
Ni lini mtaanza kuingiza maji majumbani kwetu huku kwa msuguli? Bomba kubwa lishawekwa ardhini kuanzia morogoro road mpaka msingwa. Maji yanavuja tu. Mtatupa lini?
 
Mbona mnabambikia wateja wenu bill za maji ......kuna kuna malalamiko hayo

Ova
 
Kimara stop over King'ongo hatuna maji ni zaidi ya wiki sasa.....nini tatizo? Tunaona wafanyakaxi wenu wakisoma meter bila kutupa jawabu lolote
 
Kisukuru maeneo Kilimanjaro bar TUMESHACHOKA ,maana yakitoa Leo SAA saba usiku ndio zitapita wiki mbili kama sio tatu ndio yatoke tena saa7 usiku, in SHIDA!
 
Nawapongeza Dawasco kwa kazi kubwa , kuna mabadiliko ktk utendaji ila kuna mambo ya kuboresha mengi kadiri ya maoni mbalimbali ya wadau .
Mimi langu ni kuhusu bills za maji . Inavyoelekea wasoma mita hawazungukii wateja wote kusoma mita ; matokeo yake sasa :-
1 . Units zinazokuja kutumwa ni nyingi kuliko zilizo ktk mita .
Madhara yake ni mateso ya kisaikolojia kwa mteja na mteja ana uwezo akiamua kuwashitaki kwa usumbufu .
2 . Mteja anaweza kukatiwa maji kwa ankara isiyo halisi na kumletea usumbufu.
3 . Inampotezea muda mteja kuja ofisini kwenu kuripoti kosa lilelile lisilofanyiwa kazi na linalojirudia.
Mara kadhaa nimefika ofisini kwenu kuripoti huu usumbufu bila mafanikio na mwezi huu mmerudia kosa lile lile . Kama hamtajirekebisha nitajiaandaa kuchukua hatua za kisheria na nitahakikisha haki inapatikana hata kama itachukua muda mrefu . Najua wenye kesi kama yangu ni wengi na hao nd'o watakuwa mashahidi muhimu mahakamani
 
Na mie nindo shid yangu hii. units tofauti na meter reading. nimeandika hapa no response. Nimewapigia hawajaleta mhakiki.
 
Habari ya asubuhi,
Mimi ni mkazi wa Mbezi juu - Jogoo, karibu na Kerai Construction ltd. Tuna mfumo/mtandao wa mabomba uliowekwa na mradi wa Mchina. Kwa muda wote hatuna maji. Nilifika Dawasco Kawe - Nov. 2017 kuomba kuunganishwa kwenye mtandao. Niliambiwa nisubiri mradi wa matanki yanayojengwa Salasala/Tegeta ambao utakamilika January 2018. Hata hivyo mpaka sasa bado kimya.
Tafadhali naomba kujua kinacho endelea, ili niweze kutuma maombi ya kuunganishiwa maji.
Nawasilisha.
DAWASCO
 
Kwanini bado Watanzania wote hawapati maji ya kutosha ni kitendawili cha Dunia!
Africa: Water surpluses persist in East Africa

DcCK2HzW4AABHJR.jpg large.jpg
 
Inawezekana kuna leakage ndani ya mfumo wako wa Maji hivyo kupelekea upotevu mkubwa wa Maji na bili kubwa
Bila mita kusoma hivyo? leakage kabla ya mita? Maana last reading mita ilisoma unit 811, next bill naambiwa nimetumia 49 units lakini mita inasoma 825?????? Anyway, naona baada ya kupigiwa simu wamerekebisha nimeletewa bill nyingine. Naomba mrudishe utaratibu wa kusema last meter reading zilikuwa units ngapi. Inasaidia sana kutobambikiwa bill.
 
Back
Top Bottom