DAWASCO, ni aibu mabomba mengi mjini yamepasuka yanamwaga maji

kapuchi

JF-Expert Member
Oct 8, 2008
268
163
iInasikitisha kuona maeneo mengi ya mji wa dares salaam mabomba yakiwa yanamwaga maji hovyo barabara ni wakati wakazi wa Bunju b juu njia ya kuelekea Mabwepande hakuna maji kabisa

Tumeshapiga kelele za kutosha kwa wadau wa Dawasco ya kuwa eneo hili lote ambalo liko mkabala na Mradi wa Nyumba za watumishi wa serikali (TBA) watanzania hatuna maji ,tunafanya kununua kwenye maboza ya watu binafsi ,ambao wanayauza kwa bei ghali sana

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa,na Mbunge wetu machachari Mh Halima Mdee hebu mtusaidie msikie kilio chetu maana Dawasco wameshindwa na hili jambo
 
Ukipita jangwani utaona maji mengi utadhani mvua zinaendelea kunyesha kumbe bomba limepasuka na sidhani kama wanajua!!!!
 
Dawasco ibinafsishwe tuu, wameshindwa kazi. Maji shida mjini kama tupo kijijini? Hivi hili shirika lina viongozi kweli? Basi kama wapo wanajijali wenyewe na sio maslahi ya taifa.
 
Wanatoa namaba ya kuwapigia kuwaeleza tatizo hawa dawasco na hawaji. Fake tupu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom