DAWASCO kulipisha pesa kwa kisima ulichochimba mwenyewe ni sawa?

Akilimali22

Senior Member
Jun 7, 2015
168
90
Wanajamii, mimi naishi mjini katika jengo lenye gorofa naneSasa hapa kwenye jengo kuna kisima katika hali ambayo sijaielewa Dawasco wametoa agizo kuwa watakusanya pesa kama kibali na usajili pesa ambayo itakuwa inalipwa kila mwaka kuanzia leo hii.

Najiuliza hii ni sawa kama si sawa naomba mnieleweshe kwanini tunafikia hapa?

Sababu ya kuchimba kisima ni kuwa na tatizo la maji sasa mtu unajitahidi mwenyewe bado unatozwa pesa ambazo hazieleweki za nini katika maendeleo ya nchi.
 
wanajamii mm naishi mjin katika jengo lenye gorofa nane..sasa hapa kwenye jengo kuna kisima katika hali ambayo sijaielewa Dawasco wametoa agizo kuwa watakusanya pesa kama kibali na usajili pesa ambayo itakua inalipwa kila mwaka kuanzia leo hii,hv najiuliza hii ni sawa kama si sawa naomba mnieleweshe kwa nn tunafikia hapa ..sababu ya kuchimba kisima ni kuwa na tatiz la maji Ss mtu unajitahid mwenyewe bado unatozwa pesa ambazo hazielewek hiz za nn katika maendeleo ya nchi...
MKUU NAWEZA NIKAKUSAIDIA ILA NAOMBA UNYOOSHE MAELEZO...ILI NIJUE NITAANZIA WAPI KUKUSAIDIA ILA KWA MUANDIKO HUO ATA WACHANGIAJI WENGINE WATASHINDWA CHAKUKUSAIDIA
 
ok mkuu ni kwamba Dawasco wanatoza pesa kama vile unavolipa kodi ya majengo au pesa ya fire kila mwaka ..ila hii ni kwa kisima ulichokichimba mwenyewe napenda kufahamu hii ni halali au
 
hapana mkuu hiyo si halali...ata kidogo je kisima hicho kinafaidisha hapo kwako tuu au ata nyumba zininezo?
 
wanajamii mm naishi mjin katika jengo lenye gorofa nane..sasa hapa kwenye jengo kuna kisima katika hali ambayo sijaielewa Dawasco wametoa agizo kuwa watakusanya pesa kama kibali na usajili pesa ambayo itakua inalipwa kila mwaka kuanzia leo hii,hv najiuliza hii ni sawa kama si sawa naomba mnieleweshe kwa nn tunafikia hapa ..sababu ya kuchimba kisima ni kuwa na tatiz la maji Ss mtu unajitahid mwenyewe bado unatozwa pesa ambazo hazielewek hiz za nn katika maendeleo ya nchi...
Ukielewa kuwa dawasco ni shirika la maji safi na maji taka Dar es salaam, ikiwa kweli gorofa lako lipo mjini kati city centre basi inatakiwa uwe mpole, na uwalipe tu bill yako.

Mimi wa huku goba kweli naweza kugoma kuwalipa kama nina kisima changu na sina maji yao.

Mkuu hapa sijakielewa kabisa, ni sheria ipi ambayo inaipa mamlaka dawasco kufanya hilo unalodai endapo nyumba ina kisima chake kwa kuwa ipo katikati ya jiji?
 
hapana mkuu hiyo si halali...ata kidogo je kisima hicho kinafaidisha hapo kwako tuu au ata nyumba zininezo?
ni hapa tu, ila jengo lina .gorofa nane ina lazimu kila apartment itoe 50,000/-ili kuifikia figure wanayotaka walipwe na ni kila mwaka kuanzia sasa.
 
hapana aisee hawana mamlaka hayo ata kidogo...ikiwezekana nenda mahakamani/waandikie barua ya kuwataka wakuambie mamlaka ya kuchukua huo ushuru wameupata wapi?...maana yake watu wanaotumia solar wanatakiwa walipe ushuru kwa tanesco...
 
Shukran Mkuu kwa ushaur
 
Mkuu hii inaonesha wewe mwenye kisima unawauzia hao wenzako majo ya kisima,
na wakishayatumia hawana pa kuyapeleka mnaingia katika sewarege ya DAWASCO
hapo ndipo wanapopiga ile % ya maji taka.
lm alivyosema aliuetangulia kuwa yeye anakaa Goba huko chimba kisima chako uza na maji taka yatafutie namna na kuyachota
Km sijakuelewa, ina maana ile system ya maji taka ya DAWASCO hutumii basi usiwalipe, nenda Jiji kakate leseni lipa service levy TRA nk
 
Usipende pende mahakama, unapoteza muda
 
Shukran Mkuu kwa ushaur
anza kwanza kwa kuwaandikia barua, barua yako iadress kwa meneja wa tawi la dawasco eneo ulilopo...ukiweza siku ya kupeleka barua kabla hujaifikisha pale mapokezi waombe kuonana na meneja kisha ukiwa unampa barua yako muhoji hayoma maswali...ila usisahau kuwa unatakiwa uwe na barua mbili yani moja ubaki nayo ambayo itapigwa muhuri na dawasco kuwa wamepokea barua yako...orginal utawapa copy utabaki nayo sasa hiyo copy hakikisha dawasco wanaipiga muhuri wa received. incase meneja hayupo unaweza kuiacha barua yako pale mapokezi lakini hakikisha copy ya barua yako inapigwa muhuri....hii itakusaidia sana pindi utakapoenda ngazi za mbele
 
Mkuu hii inaonesha wewe mwenye kisima unawauzia hao wenzako majo ya kisima,
na wakishayatumia hawana pa kuyapeleka mnaingia katika sewarege ya DAWASCO
hapo ndipo wanapopiga ile % ya maji taka.
lm alivyosema aliuetangulia kuwa yeye anakaa Goba huko chimba kisima chako uza na maji taka yatafutie namna na kuyachota
Km sijakuelewa, ina maana ile system ya maji taka ya DAWASCO hutumii basi usiwalipe, nenda Jiji kakate leseni lipa service levy TRA nk
Mkuu kwanza mm siuzi maji ya kisima ila hichi kisima ni kwa ajili ya jengo zima kwa kuwa maji ya Dawasco ni tabu hilo linaeleweka kwa kila mkazi wa maeneo ya mjini na kuhusu sewarage system hz bill zinakuja na tunalipa kila mwez kwa huku kwetu tunalipa 18,000/-kila mwez
 
Mkuu hapa sijakielewa kabisa, ni sheria ipi ambayo inaipa mamlaka dawasco kufanya hilo unalodai endapo nyumba ina kisima chake kwa kuwa ipo katikati ya jiji?
Mkuu huyo jamaa mwenzetu atanatakiwa kulipia bill ya maji machafu na si bill ya maji masafi.

Sababu ni kwamba, watu wa city centre huwa hawana makaro ya maji machafu, kwa maana maji machafu yao yote yanaingia kwenye mtandao wa dawasco, ndio maana nimesema sisi watu wa boko ama goba hatuwezi kudaiwa maji machafu.
Mkuu hapa sijakielewa kabisa, ni sheria ipi ambayo inaipa mamlaka dawasco kufanya hilo unalodai endapo nyumba ina kisima chake kwa kuwa ipo katikati ya jiji?
 
Anaandika Manager wa Mkoa wa Ilala

Kwa Mtoa Mada hapo Juu naomba nikupe Darasa kidogo kuhusu visima, Kisima ni Mali ya Mtu na hakina Mamlaka yoyote na DAWASCO, hakuna tozo yoyote ya Kisima kwa DAWASCO, visima vyote kuanzia usajili, umiliki hadi ukaguzi unafanywa chini ya Taasisi ya Serikali iliyopo chini ya Wizara (BONDE), hawa ndiyo wenye kutoa vibali, hawa ndiyo wenye kusimamia visima, kwahiyo hilo la kusema kuna tozo ya Dawasco juu ya Kisima si Kweli...! Dawasco kwa Sasa tupo kwenye zoezi maalumu la kuwashawishi watu warudi kwenye huduma yetu kama mwazo, Tuna Maji ya Kutosha, ningependa kutoa Rai kwa Wananchi wa Mkoa wa Ilala ambao mtoa Mada inaonekana ndipo anapoishi kuwa Maji yetu ni hakika na salama na nafuu, Karibu tukuunganishe kwenye Maji yetu, pia ukisikia mtu yoyote anadai tozo au hela yoyote ya kwenye kisima tafadhali usisite kumtolea taarifa Ofisi zetu, kwa maelezo zaidi nitakutumia Number husika DM
 
wanajamii mm naishi mjin katika jengo lenye gorofa nane..sasa hapa kwenye jengo kuna kisima katika hali ambayo sijaielewa Dawasco wametoa agizo kuwa watakusanya pesa kama kibali na usajili pesa ambayo itakua inalipwa kila mwaka kuanzia leo hii,hv najiuliza hii ni sawa kama si sawa naomba mnieleweshe kwa nn tunafikia hapa ..sababu ya kuchimba kisima ni kuwa na tatiz la maji Ss mtu unajitahid mwenyewe bado unatozwa pesa ambazo hazielewek hiz za nn katika maendeleo ya nchi...
Kabla sijakusaidia kujibu ni vyema nikuulize maswali machache:-

1;Kisima hicho kimechimbwa kwa njia gani ( Mkono au Mashine na kina urefu gani kwenda chini)
2:Kisima hicho kabla ya kukichimba ulifanya/kufuata taratibu gani za Kiserikali? au
3:Ulichukuwa drilling permit na water user permit?
 
Back
Top Bottom