Dawasco Hoi.

rutashobya

Member
May 2, 2008
6
0
Mamlaka ya maji safi na maji taka (DAWASCO) sasa inachungulia kaburi. Kampuni hii sasa imefikia hatua ya kushindwa kununua mafuta ya magari kwa ajili ya shughuli zake za kawaida za kila siku.Leo asubuhi mida ya saa nne na nusu nilienda katika ofisi za makao makuu ya Kampuni hiyo ili kulipa bili yangu ya maji ambapo nimeshuhudia magari mengi ya Kampuni hiyo yenye rangi nyeupe na blue yakiwa yamepaki ndani ya yard ya Kampuni hiyo.Nimejaribu kudadisi nikaambiwa kwamba magari yote ya Kampuni hiyo yapo hapo tangu siku ya Ijumaa kutokana na kukosa mafuta kwani MZABUNI (SUPPER DOLL) ambaye amekuwa akitoa huduma hiyo amesitisha zoezi kutokana na kuidai kampuni hiyo zaidi ya milioni 800, ambazo kwa hali ya sasa ya shirika hilo ni vigumu kuzipata.

Nimedokezwa pia kwamba katika hali ya kutapatapa, Kampuni hiyo inafanya mpango wa kupeleka magari yote kwa foleni ili kununua mafuta kwa CASH katika kituo kingine.

Tafadhali waandishi wa habari fuatilia suala hili na mliweke wazi maana kama Kampuni hii inalegalega namna hii tutaanza kukosa huduma ya maji na hasa ukizingatia kwamba siku chache zilizopita hata wafanyakazi walionyesha kumkataa kiongozi wao mkuu Mhandisi Alex Kaaya.
 
This is sad. City water walishindwa kazi. We thought DAWASCO will be ok. So mchawi ni nani?
 
Back
Top Bottom