DAWASCO Geita fungeni mita za maji safi

Jorochere

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
1,000
2,000
Habarini ndugu,

Ni takribani miezi 6 tangu mradi wa Maji safi uzinduliwe mjini Geita. Kwanza natoa shukrani kwa mamlaka husika kwa kujizatiti kusogeza hii huduma kwa wananchi na kuwaondolea ghadhabu ya muda mrefu ya uhaba wa Maji.

Changamoto na kero kubwa ni ukosefu wa mita kwa ajili ya kubaini matumizi ya huduma hii muhimu ya Maji ambapo wenye nyumba sasa "wanapiga hela"kwa wapangaji kwa kuwatoza kuanzia Tsh: 4,000 kila kichwa bila kujali umetumia au hujatumia! Ukihoji inakuwaje unaonekana mchochezi! Hivi inawezekana kweli, kwa mfano mji mmoja kuna wapangaji 20×4,000=80,000 ikakusanywa halaf yote ikapelekwa DAWASCO tena bila kutolewa risiti?

DAWASCO kama mliweza kutumia gharama kununua mabomba na kulipa mafundi mitambo na wataalamu kwa ajili ya kufanikisha utoaji wa Huduma ya Maji, mtashindwaje kufunga mita kwa ajili ya kuthibiti na kubaini matumizi? Sasa ni wakati wa kumalizia mkia ng'ombe mlishamla! Au ndio mwanya wa "kupiga dili?"

Ushauri kwa wenye nyumba; kuweni wastaarabu, acheni kuwanyonya wapangaji wenu kwa kutumia huo mwanya wa kukosekana mita. Nitalipiaje huduma ambayo sijatumia? Au tuseme mlishaingia ubia na DAWASCO au? Tuambieni tujue maana mnakera sana.

Mamlaka husika fuatilieni hili swala.haiwezekani wananchi kuendelea kutozwa bili za Maji na wenye nyumba bila utaratibu wa kubaini matumizi ya kila mmoja.
 
johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
38,404

Dawasco Geita?!
 
CHIEF MGALULA

JF-Expert Member
Sep 11, 2009
903
500
Swala Sio Gharama Halisi, Kumbuka Na Yeye Anapoteza Muda Wake Kwenda Kusimama Foleni, Muda Ambao Angeutumia Kufanya Mambo Mengine
 
kizaizai

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
3,712
2,000
Ndio walewale anakwambia nipo Shell nakusubiri kumbe yupo Total au GAPCO petrol station.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom