DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Hivi utaratibu wa kusoma mita ukoje? Mi ni mteja mpya ila bado sijaelewa maana sijaona mhusika yeyote akikatiza hapa home
 
Dawasa nataka kufahamu...je kifuru ya kinyerezi ipo kwenye mpango wa kuunganishwa maji mwaja huu au tuendelee kunywa matope tu?
 
Zungukeni mitaani mfanye utafiti ni nyumba ngapi hazina huduma ya maji,wafungieni wateja mabomba ya maji hukohuko majumbani mwao sio waje maofisini kwenu kuomba huduma ya maji
 
Hivi DAWASA lini mtatuunganishia maji kule Mbezi Makabe?

Au inatakiwa nini cha kufanya ili tuweze kuunganishiwa maji kwa uharaka kama sehem zingine?
 
Haina haja ya kuwepo hii DAWASA special thread kama tunajiuiza na kujijibu wenyewe
 
DAWASA KIBAHA NI TATIZO!!
Mimi ni mteja mzuri sana wa DAWASA na huwa najitahidi sana kila mwezi kulipia Ankara kwa wakati. Tatizo linakuja pale maji yanapokatwa bila mteja kupewa hata taarifa, kwamba kuna ukarabati unafanyika hivyo huduma haitapatikana kwa muda.Tatizo lingine nililoliona kwa DAWASA Kibaha ni kutokujali mabomba mengi yanavujisha maji tena mengi sio kidogo,lakini they don't care maji yanapotea sana kwa kuvuja barabarani, mabomba yanapasuka repair haifanyiki kwa wakati, Uongozi umeshindwa kabisa kazi ni vyema Waziri mwenye dhamana Mh Makame Mbarawa akatembelea Pwani ajionee madudu yanayofanyika huku. Tatizo lingine kuna kubambikiana bill, mimi nina SIMTANK lenye ujazo wa LTR 3000 ninapolijaza lile huwa situmii tena maji ya bomba,mpaka niliyojaza kwenye SIMTANK yanapoisha na kwa mwezi najaza TANK mara mbili ikizidi sana mara tatu lakini inapokuja bill inakuwa kubwa mno kuliko matumizi nimejaribu kuhoji baadhi ya watu wanasema bill inaongezwa ili kufidia maji yanayopotea njiani. Huyu Engineer sina hakika kama anadeserve position aliyonayo kwa sababu hatuwezi kupata maji kwa wiki mfululizo bila kukatika na mbaya zaidi hakuna Taarifa yoyote inayotolewa. Tunaomba Mamlaka husika ifanye mabadiliko kwa Uongozi mzima wa DAWASA Mkoa wa Pwani. Nawasilisha
 
Pole sana za bingwa..tupatie maelezo yako binafsi yaan kituo ulichoomba,fomu namba pamoja na namba yako ya simu kwenye mesage nasi tutaufanyia kazi
Yaani DAWASA Kazi zenu mnafanya polepole sana. Naishi Madale. Nimeomba maji tangu 2017 mpaka leo. No message. Nothing
 
Dawasa acheni dharau nimeuliza maji mnatuunganisha lini kifuru ni mwezi sasa hamnipi majibu.... jibuni maswali ya wateja wenu ndio maana ya kuwepo hii thread!
 
Mnaniletea Bili 3M matumizi ya nyumbani nawauliza mnaniambia eti ni pamoja na deni la nyuma kwa kuwa mlikuwa mnaleta bill zenye makadirio ya chini sana kwa mwaka na nusu. Kwa uzembe wenu kwa nini tusigawane hili deni?
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)

DAWASCO HUDUMA KWA WATEJA 0800110064
DAWASCO ILALA 0743 451879
DAWASCO KAWE 0743 451861
DAWASCO KIBAHA 0743 451875
DAWASCO KIMARA 0743 451865
DAWASCO KINONDONI 0743 451863
DAWASCO BAGAMOYO 0743 451877
DAWASCO MAGOMENI 0743 451862
DAWASCO TEGETA 0743 451881
DAWASCO TABATA 0743 451867
DAWASCO TEMEKE 0743 451866View attachment 721128
Mmetufungia Mtaani kwetu Maji.
Mmetumia Mambomba madogo kwenye Main lines,as a result pressure kila mkifungua inapasua Maji yanamwagika.
Tokea mtufungie zaidi ya Mwezi Maji yametoka si zaidi ya Mara tatu.
Muje Mng'oe basi Mabomba yenu,Maana Kama hayana Maana kabisa
 
Bomba lenu lilipasuka. Mlipokuja kutengeneza mliwarushia watu eote maji ila mimi. Nimetoa taarifa nikapewa namba ya rejea Mkasema ili kufuatilia ni quote hiyo ref number. nimepiga simu mara tatu kufuatilia kila siku mnasema mmepokea taarifa. Hivi tatizo dogo kama hili inawachukua muda gani kulirekebisha. Nipo Kibaha. Kongowe. Msoma mita wetu anataarifa hii kwa zaidi ya siku 7 sasa.
 
Hivi dawasa kwa nini mnakata maji kabla ya mwezi kuisha hamjui wengine tunapokea pesa tarehe thelathini
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom