DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)

DAWASCO HUDUMA KWA WATEJA 0800110064
DAWASCO ILALA 0743 451879
DAWASCO KAWE 0743 451861
DAWASCO KIBAHA 0743 451875
DAWASCO KIMARA 0743 451865
DAWASCO KINONDONI 0743 451863
DAWASCO BAGAMOYO 0743 451877
DAWASCO MAGOMENI 0743 451862
DAWASCO TEGETA 0743 451881
DAWASCO TABATA 0743 451867
DAWASCO TEMEKE 0743 451866View attachment 721128
NAOMBA DAWASA MTUJULISHE SISI WAKAZI WA KIFURU LINI MTATULETEA MAJI ILI TUACHE KUISHI MAISHA YA KIZANDIKI NAMNA HII?
 
DAWASA MAENEO YA MAGETI HAPA GOBA MAJI HAKUNA TUNATUMIA MAJI YA CHUMVI CHA KUSHANGAZA MABOMBA YAMEKUJA MPAKA MTAA WA MUHIMBILI INAKUWAJE MAENEO YA MAGETI HAYO MABOMBA KUCHIMBIWA BADO NA KUNA BAADHI YA WATU HUKU WANACHEZA MICHEZO MICHAFU HILI MAJI YA DAWASCO YASIJE JE HILI SUALA MNALIJUA? KARNE HII KWELI WATU TUNATIA MAJI YA CHUMVI KWELI
 
Dawasa kifuru tunapara lini maji naombeni mnijibu swali hili nimeuliza sana
 
MIMI , NAULIZIA ZILE NAFASI ZA KAZI ZA KUCHIMBA MITALO/NJIA KWA AJILI YA KUFUKIA MABOMBA YA MAJI JE HUWA ZINAPATIKANAJE , MAANA NATAFUTA KAZI HIZO ZA KUTUMIA NGUVU .

DAWASA
 
Mimi ni mkazi wa Boko mnemela njia panda ya mpiji kiukweli tunapata tabu sana kuhusu swala la maji tushatoa 5,000 zetu na kupewa form kuwa Dawasa survey atakuja yapata mwaka sasa hakuna aliyepita tunakaa na form mpaka zinapauka hebu fanyeni utaratibu mtuunganishie maji maana mara ya kwanza mlisema mradi hamjakabidhiwa je mpaka leo hamjatuunganishia maji tatizo liko wapi muwe mnatupa taarifa basi maana namba zetu mnazo
 
Naandika uzi huu kwa masikitiko makubwa sana hapa keko wanga karibu mkabala na kiwanda cha dawa cha gulin, kuna bomba lenu limekatika sasa ni miezi minne maji yanamwagika na wahuni wanachota wanauza. tumeita fundi wadawasa kaja mpaka leo hajarudi, n hasara kubwa sana na sisi wakazi wa hapa maji hatupati. sina majina ila namba zawale tuliokuwa tunawapigia zipo. cha ajabu juzi mmekuja kudai bill ya maji wakati maji yaishia hapo na huku hayafiki mwezi wa 4 sasa
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)

DAWASCO HUDUMA KWA WATEJA 0800110064
DAWASCO ILALA 0743 451879
DAWASCO KAWE 0743 451861
DAWASCO KIBAHA 0743 451875
DAWASCO KIMARA 0743 451865
DAWASCO KINONDONI 0743 451863
DAWASCO BAGAMOYO 0743 451877
DAWASCO MAGOMENI 0743 451862
DAWASCO TEGETA 0743 451881
DAWASCO TABATA 0743 451867
DAWASCO TEMEKE 0743 451866View attachment 721128
DAWASCO
KWANINI MMEKUWA.MNABIMBIKIZA SANA BILL ZISIZO ZA WATU
TUNA BILLS ZA MILLION 2 TOKA 85000

BAADA YA KELELE ZIKARUDISHWA TO 1" 060" 000

KAWEBRANCH KUNA SHIDA GANI NA BAADA YA KELELE ALIEKUWA ANABAMBIKIZA MKAMWONDOA UPANDE WA TANKIBOVU

WAHUSIKA WAKALALAMIKA SANA HAKUKUWA NA MSAADA WOWOTE MKAISHIA KUSISITIZA ZILIPWE WAKATI HUO WANAKWENDA DAWASCO BAADHI YA WAFANYAKAZI WANATAKA WALIPWE NUSU WACLEAR DENI

MAMAMOJA MZAZI AKAJIOLEA KUPUNGUZA DENI LIKAISHIA 270000
MKAENDA KUONDOA MTR HUKU MANAGER AKISISITIZA ZILIPWE ZOTE
MAJUZI MMEKUJA NA BILL YA 500'000 TOLA 270000 AMBAYOO MLISAINI WENYEWE NA KILA.MAKATO MNATOA RESIT

LEO HII AFISA WENU JAMAL ANAULIZWA HII BILL IMETOKA WAPI ANASEMA WALIBADILISHA MTR WAKAKUTA HILO DENI

TUNAULIZA TOKA NOV HAWANA HUDUMA DADANGU MKATOAA NA MITA
JE LEO HIII HIO 500'000 INATOKEA WAPI

AFISA ANASISITIZA ANDIKENI BARUA ELSE INACHUKUA MUDA MPAKA HUDUMA ZIRUDISHWE ELSE LIPEN 170000 MMALIZIE HIZO BAKI NDANI YA MIEZI MITATU HIZO PESA ZINATOKA WAPI NA HIZOO BILI N ZA NANII NA HUU UPUUZI UNAISHAA LINI

MMLIBAMBIKIZA BILI TOKA 85000 MPAKA MIL MBILI
MKARUDISHA MOAKA MIL MOJA
HIKO N KIWANDA NA STATEMENTS ZOTE ZIPO HAYA MAMBOO YALISHAISHAA MNAYAANZISHA HATA ENZI ZA MAGUFULII AIPENDZI

CONT +255 658 2155
0718 2426 60
cc
CYPRIAN.L
 
JMOSI MNAPIGA SIMU KUTOKA AFISA WA MAKAO.MAKUU OMARY MTU AENDE TEGETA ..TEGETA WANASEMA TWENDE KAWE ..KAWE NDIKO HIO.MICHEZO.MICHAFU INAYOFANYIKA GAFLA AFISA ANASEMA BILL 500'000
NA SIO 270" 000
ANAULIZWA HIZI RESIT MMETOA NINYI AMA ZA KUGUUSHI ANASISITIZA TUKIANDIKA MALALAMIKO INACHUKUA HATA MIEZI SITA KURUDISHIWA HUDUMA NYIE KALIPENI HIZO 170000
INAYOBAKIA MLIPE NDANI YA MIEZI MITATU HUU UPUUZI UNATOKEA WAPI NA BADO HAYA MAMBOO YAPO KWELI??

MH ANAYAJUA KWELI..NAKUMBUKA YALIKUWA ENZI ZILE ZA UMEME LAKINI NA HUMU MNAYAACHA LINI???UNAMTISHAJE MTEJA ATI UKIANDIKA MALALAMIKO UTARUDISHIWA NDAN YA MIEZI SITA

WAKAT HUOHUO ALIELETA RESIT BAADA YA KULIPA JTATU ANASEMA ILIPWE 150000 120" 000 MLIPE POLEPOLE NAWAZA HUYO JAMAL NA HAO WANAOPITA MAJUMBANI NA KAMPUNI MOJA AMA TOFAUTI..LEO ANAKUJA NA BILL YA 500" 000
 
Dawasa Dawasa. Fuatilieni uunganishaji bomba jipya Makuburi DSM. Ni majanga matupu. Watu wenu waliweka bomba jipya vizuri tu kuanzia A - Z. Sasa kuunganisha ni mtihani. Wanatoka A wanakwenda F wanarudi B wanakwenda Z nk. Ni mazingira ya rushwa na si cuostomer friendly, jeuri sana. jambo lingine wanawaambia wateja wachimbe wenyewe. Wachimbaji wanataka elfu 10. Bado wao watakuzunguusha uwape chochote na ni mwezi sasa tunanunua maji ndoo sh 500. Lakini je, hao wachimbaji tunaotafuta wakikata hilo bomba jipya na masururu yao nani wa kulaumiwa? Maana tunawajua vichwa vyao hawa wachimbaji. Meneja tunajua unavyopokea simu zetu na kuwapigia vijana wako. Tafadhali toka ofisini fuatilia....
 
Safi sana, Maji mtaani kwetu tunapata na yenye spidi kali mpaka bomba zinaachia.Mjitahidi kwenye kutoa taarifa za marekebisho mapema tu ili mnapokata tuwe na akiba ya kutosha.
 
MATENGENEZO MTAMBO WA RUVU JUU LEO (17.06.2019) KUTOKANA NA HITILAFU YA UMEMEView attachment 1129769
Wengi wa watumishi Dawasa mnafanya kazi vizuri isipokuwa wachache wanaoendekeza "kitu mazoea" na hii tabia imekomaa Sana kwa senior officers hasa kitengo Cha ufundi/matengenezo na biashara, kwa kifupi uchafu wa mambo yao ni mengi hivyo naomba email ya CEO moja kwa moja nimpe A-Z ya DAWASA na hii ni kutokana na email account yenu haifanyi kazi wala email za zamani DAWASCO nazo hazipo hewani
 
Dear *DAWASA* Kimara
Ni lini sisi wakazi wa kuanzia V8 kwenda Kwamrema hadi Kwamashaka tutapata huduma ya kuaminika

Tunavyoongea ni wiki ya pili sasa hatuna maji
 
Mrejesho
Maji yanatoka huku V8 ahsanteni kwa kuskia kilio changu
----------------
Hapa Kimara V8 Mskitini mtaa kama unaelekea kwa Mama Nunuu kuna bomba limevujisha maji kwa sababu ya magari yakipita na mpira upo juu juu

Watu wanajichotea maji tu hii pipe line inaenda kwa mteja wenu
IMG_20190831_065005.jpeg
 
Mrejesho
Maji yanatoka huku V8 ahsanteni kwa kuskia kilio changu
----------------
Hapa Kimara V8 Mskitini mtaa kama unaelekea kwa Mama Nunuu kuna bomba limevujisha maji kwa sababu ya magari yakipita na mpira upo juu juu

Watu wanajichotea maji tu hii pipe line inaenda kwa mteja wenuView attachment 1193898

Ukweli DAWASA kuna mambo mnayoyafanya kwa kuwa mumezoea uzembe wa toka enzi za NUWA mpaka DAWASCO sasa inabidi mbadilike ili muende na wakati, Mteja wenu anaomba maji na nyie mnafanya survey/mnatoa budget na baadae mnakuja kuchimba mfereji juujuu tu ambayo haidumu, kwanini msiruhusu vifaa vyote vinavyohitajika na kazi ya kuchimba mtaro ambayo sasa hivi mnaruhusu wanachimba vishoka wenye connection na DAWASA (kuna jamaa ameuliza tenda zenu za kuchimba mtaro mnazitoaje na mmeshindwa kumjibu) Ili kuwe na quality nzuri ya mtaro ni bora kazi hii ikafanywa na mteja na nyie mkabaki na kazi ya kuunga tu kwenye bomba lenu na ku certify kazi yote aliyofanya huyo mteja wenu na endapo hapo baadae bomba litatoboka na kuwa na leakage basi mwenye bomba ndie awajibike na akishindwa basi kupitia close supervision yenu mnakata service yake na anailipia pale atakapohitaji kuunganishiwa na hii itasaidia kuepusha upotevu wa maji kwa sababu mtakuwa mmegawa madaraka ya usimamizi wa bomba direct kwa mteja na sio nyie kwani utaratibu wa sasa hivi watu tunatoa taarifa za upotevu wa maji au bomba kupasuka kwa watumishi wenu hasa wasoma mita na ofisini kwenu na hakuna mwitikio wa haraka kama vile hakuna hasara na inapotokea wakaja basi watumishi wenu wanakuwa kwenye operation maalumu na ndipo wanapokata bila maelezo yoyote na kutaka chochote kitu ili waunganishe maji, DAWASA kama kweli mnataka kunyoosha utendaji wa kazi na kuweka mazingira mazuri ya huduma ya maji basi sasa ni wakati muafaka wa kuweka mkataba kati yenu na mteja ili atakayeuvunja awajibike kwa kuvunja mkataba na sio kuendesha shirika kama lilivyo hivi sasa, Mwisho naomba ICT afanye review ya website kwani tunashindwa kujua kama ni dawasco au dawasa...www.dawasa.go.tz haijawahi kufunguka wakati nayo email account info@dawasa.go.tz inagoma kufanya kazi, Watendaji wenu from top to down hawana official email account? zamani mkiwa Dawasco CEO alikuwa na official email account siku hizi akiwa Dawasa hana? wekeni milango ya watendaji wakuu wenu wazi ili kuzuia umangimeza wa watendaji wabovu walio chini yao kwani hizo namba mlizotoa tukipiga simu zinapokelewa na mabinti wa reception ambao wao na watu wa field ni kitu kimoja nasema hivi kwa sababu ilinipata siku moja nilikuwa nashida yakumwona engineer tu basi nilizungushwa kama nataka kumwona JPM na mungu bariki yule bwana alitoka nje ya ofisi akiwa anaelekea site na ndipo aliponisaidia tatizo langu kwa kutumia dakika chache tu tena tukiwa tumesimama nje ya ofisi, Jambo jingine jamani katika mashirika ya umma nafikiri nyie mna overstaff, kwa mfano inakuwaje reception office mnakuwa na mabinti zaidi ya mmoja wakati computer wanayoitumia ni moja?
 
Back
Top Bottom