DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Sms za bili zinatumwa kwa wakati na usumbufu wa kukumbusha mara kwa mara kuwa kalipe au utakatiwa huduma
Hawa DAWASA hawako serious kabisaa.....maana hata majibu ya malalamiko yetu hakuna anayejishughulisha kuyajibu na lithread lao la DAWASA...wako kimya kama vile hawana taarifa ya haya yaliyowasilishwa hapa.
ONENI AIBU NYIE DAWASA.....BILI ZETU NDO ZINALIPA MISHAHARA YENU.
 
Makongo juu wanakuja kuziba maji yanayovuja barabarani wakukuta bomba LA MTU karibu na hapo wanapoziba wanakata maji na shimo wanafukia hivi hawa watu wanalipwaje?nahisi mshahara wa dawasco ni ruzuku sio bill tunazolipa.ji
 
Mamlaka ya Majisafi na Majitaka jijini Dar(DAWASA) imetangaza kuwa uzalishaji wa maji katika mtambo wa Ruvu Juu umesimamishwa kwa muda ili kuruhusu mafundi wa TANESCO na DAWASA kufanya maboresho kwenye mtambo huo

Maboresho hayo ni kutokana na hitilafu ya umeme katika njia ya kuingizia umeme katika mtambo huo na hivyo mtambo utawashwa mara baada ya hitilafu kurekevishwa

Baadhi ya maeneo yatakayokosha maji kutokana na kuzimwa kwa mtambo ni pamoja na Mji wa Mlandizi, Ruvu Darajani, Kwa Mathias, Mkuza, Maili Moja, Kibamba, Mbezi, Kimara, Changanyikeni, Ubungo na maeneo ya Tabata
IMG-20190617-WA0002.jpeg
 
MATENGENEZO MTAMBO WA RUVU JUU LEO (17.06.2019) KUTOKANA NA HITILAFU YA UMEME
IMG-20190617-WA0087.jpeg
 
Bomba linavujisha maji uwanja wa mnada kunduchi mecco mnapigiwa simu hamji kuziba
 
Jamani maeneo ya Ubungo Msewe(Golani kwa Muya), maji hayajatoka wiki ya tatu sasa, watu wanaishi kwa taabu sana na kuna ujumbe unatumwa kwa wateja wawe wavumilivu eti umeme mdogo. Mnataka watu wafe kwa kipindupindu? Mbona maeneo mengine ya jiji maji yanatoka kila siku, ikiwezekana wafungieni nao ili na sisi tupate maji.
 
Naomba kujua bado mnahudima ya kuwafungia maji wateja kwa mkop0? Nipo kimara mwisho milenia shule ya msingi
 
Naomba mje kurekebisha bomba linaloviluja Mbezi njia ya mpigi majoe... Ni la muda mrefu Sana. Mita Kama 100 kutoka get la Mbezi high School
 
Maeneo ya mpigi magoe Mbezi yataletewa maji lini? Kuna mabomba yamelazwa chini zaidi ya mwaka sasa
 
Mimi ni Mteja wenu tangu 2016,ninaishi Kibaha P/Ndege.Mwanzoni wakati naanza kutumia huduma yenu nilikuwa naletewa bill ya Tshs 8,000/= hadi Tshs 12,000/= kwa mwezi.Lakini kadri siku zinavyozidi kwenda naona naletewa bill kubwa wakati matumizi yangu ni yale yale.Sina bustani nnayonyweshea kusema imeongeza matumizi ya maji,kwangu hakuna leakage maungio yote yamekaguliwa,isitoshe pipe zilizotandazwa kwa ajili ya kusafirisha maji sehemu mbali mbali kwenye nyumba ni ile ya Class "C"haipasuki kirahisi hata pressure ya maji ikiwa kubwa.Mwezi May 2019 nililetewa bill ya Tshs 30,000/= na mwezi huu June 2019 nimeletewa bill ya Tshs 50,000/=.Mpaka sasa hivi sijalipa nataka J'3 nikaonane na Meneja wa Dawasa Mkoa wa Pwani, akishindwa kusolve tatizo langu nitakwenda ngazi ya juu zaidi ili kupatiwa ufumbuzi wa hili tatizo. Kuna haja ya kufanya Vetting kwa hawa wasoma mita kuna uwezekano mkubwa baadhi sio waaminifu badala ya kusoma na kurekodi Units sahihi zilizotumika anaongeza units na hivyo kupotosha mahesabu.Silipi hii bill mpaka nipatiwe maelezo ni kwa nini bill yangu inakuwa kubwa ilhali matumizi yangu ni ya kawaida kabisa. Nilimwambia rafiki yangu mmoja akashangaa sana bill niliyoletewa.Anasema yeye ana wapangaji Sita na wote wanatumia maji kwa shughuli zote za nyumbani lakini analipa kila mwezi Tshs 12,000/= ikizidi sana analipa Tshs 15,000/=.Nawauliza hao wanaohusika kwa nini kunakuwa na Double standard?
 
DAWASA kuna bomba linavuja barabarani muda mrefu kidogo hapo Makuburi External kwenye mataa. Na lingine barabara hiyo hiyo kuelekea Maji Chumvi kwenye kona kabla haujafika kwenye Yard ya magari ya Raphael Logistics.
 
Ndugu wadau tuwasaidie DAWASA kuwajulisha maeneo yote yanayovuja maji. Nimegundua kuwa maji mengi yanapotea kutokana na uvujaji bila kutufikia wananchi. Naamini DAWASA kadri watakavyokuwa wanazuia huu uvujaji basi idadi ya wanaopata maji nayo itaongezeka.
 
Dawasco huduma yenu ni mbovu Sana. Hata customer care yenu pamoja na watumishi wenu. Nyumbani kimara kunatatizo la leakage kwenye mita nimereport Mara kibao lakini Hakuna suluhu. Bill imezidi kija kubwa tu.
 
Dawasco huduma yenu ni mbovu Sana. Hata customer care yenu pamoja na watumishi wenu. Nyumbani kimara kunatatizo la leakage kwenye mita nimereport Mara kibao lakini Hakuna suluhu. Bill imezidi kija kubwa tu.
Ni kweli hawa jamaa wana mapuuza sana unaporipoti kwao tatizo hawawi serious kutatua tatizo hilo kazi yao ni kutuma msg kwenye simu LIPIA BILI YAKO OPERESHENI KATA MAJI IKO MTAANI KWAKO!
 
Back
Top Bottom