DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Inakuaje wajenzi wa barabara wanakata miundo mbinu yenu hamuwachukulii hatua kurejesha mapema iwezekanavyo na bado mnawapelekea madai ya malipo wateja wenu?
Jitihada zinaendelea kuhakikisha mawasiliano yanakuwepo kabla wajenzi wa barabara hawajaanza kazi ili tuwajulishe maeneo yenye miundombinu yetu kuepusha usumbufu usio wa lazima
 
Dawasa mnakera
Nimepeleka maombi ya kufungiwa maji
Mwezi wa pili huu
Kuja kufanyiwa tathimini tu nishakuja ofisini kwenu tabata mara 3
Ofisi za serikali urasimu mwingi...kila siku saundi tu...hapo ni utathimini tu....daah
Pole sana za bingwa..tupatie maelezo yako binafsi yaan kituo ulichoomba,fomu namba pamoja na namba yako ya simu kwenye mesage nasi tutaufanyia kazi
 
Wasoma meter na wakata maji wa DAWASA hivi wana kiwango gani cha elimu. Maana ni wabishi na wasiotaka kuelewa. Mfano wamekata maji na kutoa notification ambapo bill ya notification ilishalipwa. Sasa waje kurudisha maji, wamekuja wamerudisha maji sasa pale walipofunga kwa kukunja panavuja, wanakuambia funga na mpira wewe mteja wakati wao ndio wameharibu. Naomba kujua kiwango cha elimu cha watu hawa.
Tumelipokea na tunaahidi kuwaelimisha zaidi ili tatizo lisijitokeze tena
 
Habari, naona upo online. Mie ni mnifaika wa maji ya mkopo Kibamba. Toka nimefungiwa yale maji sijapewa invoice yoyote ya kuomyesha ni kiasi gani nadaiwa. Mmeanza kunitumia bili mwezi wa pili mwaka huu. Nahitaji kulipa ila niko nje ya mkoa, naomba muongozo
Tusaidie account namba yako
 
Sawa tupatie mawasiliano yako na account namba mafundi wetu watafika hapo haraka
NILILIPA SHS.462,000 KWA AJILI YA KUUNGANISHIWA MAJI KIMARA BARUTI BAADA YA SURVEYOR KUFANYA SURVEY. IMEFUNGWA METER KWENYE LILE ENEO LAKINI TANGU ILIPOFUNGWA HALIJATOKA HATA TONE MOJA LA MAJI. MAJIRANI WOTE WANAPATA MAJI LAKINI KWANGU HAKUNA. NIMEAMBIWA ILE METER ILIFUNGWA KWENYE BOMBA LA MAJI LA ZAMANI AMBALO HALINA MAJI. NIMETUMA MALALAMIKO DAWASA NA HADI WIZARANI LAKINI HAKUNA ANAECHUKUA HATUA.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taarifa zote za DAWASA sasa kiganjani mwako..piga *152*00# sasa
IMG-20190517-WA0197.jpeg
 
HIVI DAWASCO MTATUTATULIA LINI TATIZO LA MITA.TUNAKUWA WA WAPANGAJI WENGI NA TUNAHITAJI METER KWENYE ENEO MOJA.MFANO UNA JENGO LINA APARTMENT 3 KILA MTU ALIPE KADRI YA MATUMIZI YAKE
Utaratibu unaotakiwa kufuatwa ni mmiliki wa nyumba kuomba extra meter ambayo itajumuishwa kwenye mita kuu yake na ndio atakuwa anapokea bili zote extra alizoomba kupitia bili kuu yake
 
Naomba ufafanuzi wa mradi wa kuunganishiwa maji maeneo ya bagamoyo au namba ya mhusika na taratibu kwa ujumla. Thnc
 
Jambo kubwa nina ugomvi na nyie hasa kwenye malipo ya bill zangu hamjaingiza kwenye mfumo mpaka mnaniletea madeni niliyolipa tayari ila mmekataa kukubali kuwa nililipa ingawa receipt zote zipo.
 
Ni Dawasa...Dawasco haipo tena
Nadhan mgeacha DAWASCO Mkuu mana wao kidogo walikuwa na unafuu kuliko nyinyi.....Nimelipa bill ya kufungiwa maji mwezi Wa NNE sasa sjaona cha suvyer wala kishoka..Nini hili mnatufanyia wateja wenu?
 
Dawasa ( Kimara )
Tunaomba mtujuze nini kinaendelea kwenu wakazi wa maeneo ya V8 hatuna maji yapata wiki sasa na hakuna taarifa yoyote


Please tunaomba mtufungulie hata kwa masaa 3 tu hali ni mbaya
 
Dawasa ( Kimara )

Tunaomba mtujuze nini kinaendelea sisi wakazi wa maeneo ya Kimara Vyumba 8 hatuna maji yapata wiki sasa na hakuna taarifa yoyote.


Please tunaomba mtufungulie hata kwa masaa 3 tu hali ni mbaya
 
Jambo kubwa nina ugomvi na nyie hasa kwenye malipo ya bill zangu hamjaingiza kwenye mfumo mpaka mnaniletea madeni niliyolipa tayari ila mmekataa kukubali kuwa nililipa ingawa receipt zote zipo.
Mkuu hata mimi nikienda kudai naambiwa bado hawajafungulia account ya bomba langu sasa sielewi
 
DAWASA shida ni nini mbona MAJI hatupati karibia wiki la pili hili,maeneo ya KIMARA.Hakuna TAARIFA yoyote ya kupasuka kwa BOMBA wala MATENGENEZO kwa umma.

Je? mnataka wakazi wa DAR tuanze kutumia maji ya mitaroni na hali ya KIPINDUPINDU ndo hii,je mkilaumiwa kwa kuchochoea matumizi ya maji yasiyo salama ilihali bili zinalipwa mtakuwa na cha kujitetea???.
 
Dawasa Pwani acheni ubabaishaji, mnatuumiza na bill hewa tunalipia upepo maji hayatoki mita zinazunguka upepo ukipita, mnatulipisha bili kubwa tofauti na matumizi yetu ya maji, mfano unakuta kwa mwezi unaambiwa umetumia unit 75 za maji na maji hayajatoka wk takriban 2 au 3, ukienda kutoa hiyo shida hapa dawasa pwani unapewa majibu ya kuudhi na watoa huduma.
Halafu tulichogundua sisi wakaazi wa Mwanalugali tuliokuwa kwenye mradi wa maji wa wachina baadae dawasa wakauchukua huo mradi hawakufanya tathimini mfumo mzima wa maji hao wachina, ni kwamba mfumo mzima hawkufunga air valve kwenye mabomba yao kwa hiyo maji yakikatika yanaporudi huwa hewa inaanza kupita kwenye mabomba na mwisho inaishia kwenye mita zetu, kinachouma zaidi upepo ukipita kwenye mita huwa inazunguka kwa kasi ya ajabu sana na mita inasoma unit nyingi kwa muda mfupi na bili ikija huwezi amini utakoambiwa unakuta bili inasoma unit 120 au zaid kwa mwezi inauma sana kuona unaibiwa hivi na watu wamekaa oficn ukiwaeleza shida yako wanakununia sijui tuwaeleweje nyie dawasa?
Tumeshaliripotia sana hili tatizo lakini hakuna ufumbuzi wowote ule.
Tunazidi kuumia kwa kweli.
Na hadi navyo andika hii taarifa huku leo ni siku ya tano hakuna maji na hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kwa msg au radio, zaid mtakachokumbuka kutuma meseji ni kuhusu kulipa bili na sio kutatua matatizo yetu wateja.
Ama kweli nimeamini mteja wa dawasa kibaha hana thamani.
ASANTENI
 
DAWASA shida ni nini mbona MAJI hatupati karibia wiki la pili hili,maeneo ya KIMARA.Hakuna TAARIFA yoyote ya kupasuka kwa BOMBA wala MATENGENEZO kwa umma.

Je? mnataka wakazi wa DAR tuanze kutumia maji ya mitaroni na hali ya KIPINDUPINDU ndo hii,je mkilaumiwa kwa kuchochoea matumizi ya maji yasiyo salama ilihali bili zinalipwa mtakuwa na cha kujitetea???.

Sms za bili zinatumwa kwa wakati na usumbufu wa kukumbusha mara kwa mara kuwa kalipe au utakatiwa huduma
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom