DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Huku Mbezi Beach Jogoo, watendaji wa Dawasco (fieldattendants/technicians) wanakula njama na wauza maji kazi yao ni kupiga lock maji yasitufikie....pathetic !
 
Nyie dawasco mnafanya kazi kwa mazoea sana, mm nilibambikiwa bili ya 1.6 mil mwaka jana Nov lkn mpaka leo Nov 2018 nafuatilia warekebishe hakuna linalofanyika ni ahadi tuu mara kesho. Nawaambia kuna watu hapo mtapoteza ajira nikiamua kwenda kwa waziri. Account yangu ni 900343431, rekebisheni kabla sijakasirika zaidi. Luhemeja aone hii!
Nenda ewura dawati la marekebisho. Usipoteze Muda, utaona tu wanakuita wenyewe kwa appointment.
 
INASIKITISHA KUONA KUNA WATU WANAKOSA MAJI MWEZI SASA

NA MBAYA ZAIDI KUNA SEHEMU ZA KARIBU BOMBA ZA MAJI ZIMEPASUKA INAMWAGa MAJI WANAKUJA DAWASCO NA KUGEUKA

HILO ALIPENDEZI HATA KIDOGO TUNAOMBA MUWE NA WHATSUP LINK KAMA HAWA WENZENU TANESCO KMR UKIRUSHA SHIDA DK MBILI WAKO HAPO

TUNAHESHIMU UBUSY WENU NASI TUHESHIMUNI TUNAPOLE shida ZA MAJI

KMR BARUTI KWENDA770 KUNA MABOMBA YAMEPASUKA WANAKUJA BAJAJI WA DAWASCO WANANUNULIWA SODA WANACHAFUKA WANAONDOKA BILA.KUREKEBISHA

KMR BUCHBUCHA UPANDE WA OPP NA THOMAS LYIMO NJIA YA KUINGILIA WAPO WATU WA PIKPIK HAPO WAULIZENI WAPI PANAVUJAA BARABARA IMEARIBIKA SABABU MAJI YA DAWASCO

WANAOPITA WAKIJULISHWA HAKUNA ANAEFANYA KAZI SERIOUS KABISA

IGENI HUU MFANO KAMA WATU WENU WANADANGANYWA MNATUMIWA NA PICHA NA WANANCHI

AHSANTEN
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)

DAWASCO HUDUMA KWA WATEJA 0800110064
DAWASCO ILALA 0743 451879
DAWASCO KAWE 0743 451861
DAWASCO KIBAHA 0743 451875
DAWASCO KIMARA 0743 451865
DAWASCO KINONDONI 0743 451863
DAWASCO BAGAMOYO 0743 451877
DAWASCO MAGOMENI 0743 451862
DAWASCO TEGETA 0743 451881
DAWASCO TABATA 0743 451867
DAWASCO TEMEKE 0743 451866View attachment 721128

HIZI NAMBA ZENU HATA HAZINA KAZO WALA MAANA TENAA

PALE KMR BUCHA OPP NA THOMAS LYIMO KUNA VIJANA WA PIKPIK ULIZIA HAPO GARAGE IKO WAPI MTAONYESHWA AMA KWA JANTHON HIO NJIA KUNA BOMBA LIMEPASUKA MWEZI WATATU WANAKUJA BAJAJI WABAUZA SURA WANAONDOKA UKIULIZA TUTAKUJA TENA

LEO HII BARABARA IMEJAA MAJI INANUKA MAJI MACHAFU YA MIEZI KADHAA JE N KWELI MMESHINDWA LIFUNGA

TUMESHAURI KWAKUWA MIEZI YOTE WAHUSIKA AWAJAFUNGA BOMBA LAO TUNAOMBA MLIKATE AMA MLIFUBGE VIZURI MAJI YASITOKE

HAKUNABTAARIFA AMBAYO AOJAFIKA DAWASCO WANAKUJA KUONYESHA SURA ZAO AIPENDEZO KABISA ..UKWELI ALHAMISI KAMA AWAKUJA NALIPELEKA KWA CEO NA PICHA ZOTE TWENDE SAWA NANI AWAJIBIKE
 
BINAFSI NIMEBAKIMBIWA BILI YA MILION MBILI NIMEHANGAIKA KILA.KONA MWISHO ALIEKUWA AKISOMA MT PALE KAWE MKURIA MREFU ANAKUJA KUULIZA HGAL WANGU BABA ANAONEKANA ANA HELAA HEE KISA KAONA GARI NNE NJE SIKUHIO AKUJUA ZINGINE ZA MAJIRAN NYOKO SANA

NIMEKWENDA KWA MANAGER NKAISHIA KUAMBIWA NIENDE WIKI IJAYO NIMEKWENDA WAMETOKA MIL MBILI MPAKA LAKI TISA..NIMEULIZA HIZI LAKITISA ZIMETOKA AAPI AWAJIBU

BAADA YA WIKIMBILI ANAKUJA MSOMA.MT ANAOMBA NAMBA YANGU..AKAPIGA AKASEMA NKALIPE NUSU AMA ROBO ILIOBAKIA ATAJUA ANAFANYAJE

NKAMWAMBIA UNGESE KAMA MMEZOEA HIZO HELA HUTOPATA..IMAGINE NALIPA KILA.MWEZI 8000-12000NA 1200 NIKIWA NA KUKU..NIMESAFIRI KIDOGO NKARUDI NKALIPA 40K BKAMALIZA NA DENI

LLAKITISA IMETOKA WAPI

GAFLA BAADA YA KUTUKANANA NA MSOMA MTR YULE.MKURIA NALETEWA BIL YA MIL 2 ..AISEE MANAGER WA KAWE WAWILI WAMEPITA WANADAI YAANI SIJUI TUFANYAJE....NASHUKIRI MUNGI SERIKALI HAYAMALIPO KUPITIA BENKI HAO WAHUNI WAMEKULA SANA HELA ZA WATU...NIMEANZA PUNGUZA NA NINALIPA BANK WAKAIBE HUKO

KUNA WASHENZI SANA OFISINI ENGN LAZIMA AWAKAGUE HAWA WAHUNI WA KAWE
 
Hizi mita mpya speed yake mbona kali kuliko ya zamani ? Wiki moja tu familia yangu ya watu wanne tumetumia init 4 (litre 4000 ) imekaaje ? Matumizi ni ya kawaida
 
Hizi mita mpya speed yake mbona kali kuliko ya zamani ? Wiki moja tu familia yangu ya watu wanne tumetumia init 4 (litre 4000 ) imekaaje ? Matumizi ni ya kawaida
...wanajua ! Na wenyewe wanaita 'mwendo kasi' hii huduma ya maji imejaa uhuni uhuni tu. Mie maji yapo getini kwangu lakini ndani hayaingii.....ukifuatialia mazingira ni rushwa tuu ! Tuyawatafutia 'pesa za moto' mlaze watoto wenu njaa ! Shubaaa miit !
 
What’s happening with you Dawasco? Nilikua nalipia bili kwa mpesa lakini safari hii nimejaribu kulipia kwa kutumia utaratibu wa control number lakini Dawasco Hawapo kwenye malipo ya mpesa, nimejaribu kuwasiliana na huduma kwa mteja lakini nao wameshindwa kunisaidia na nimegundua pia hawajui ambalo ni jambo la kushangaza, nauli za hivi nifanyeje ili niwalipe hela yenu nina deni la miezi miwili sasa na kwamujibu wa kazi yangu sipati muda wa kwenda kwa wakala au ofisini zenu na njia rahisi kwangu ilikua kupitia malipo ya simu
 
Kwakweli mimi DAWASA bill zenu huwa sizielewi kabisaaa... sijui mwezi wenu unaanza lini hadi lini na billi haziko updated.
 
IMG_1164.JPG
bomba limepasuka
Mlipokuwa mnachimba mtaro wiki iliyopita
Kimara Tanesco

Maji yanaingia mpaka ndani
 
DAWASCO kitengo hiki humu ndani kapewa mdada muda mwingi anajipodoa tu
Awajibu chochote lakini wanasoma comment zetu..
 
TANGU HUU UZI UMEFUNGULIWA NAKUTA TU KERO, MALALAMIKO, LAWAMA TAARIFA ZA MABOMBA KUPASUKA SEHEMU MBALI MBALI NA KADHIA MBALIMBALI LAKINI SIJAWAHI KUONA MAJIBU HATA MARA MOJA. HIVI HUU UZI ULIFUNGULIWA NA DAWASCO/DAWASA WENYEWE AU NI WATU FULANI TU WALIJISIKIA TU KUFUNGUA UZI KWA KUTUMIA JINA LA DAWASCO/DAWASA?

NI MUDA MUAFAKA SASA HUU UZI KAMA HAUJAFUNGULIWA OFFICIALY NA DAWASCO/DAWASA BASI UFUNGWE/UFUTWE TU KWA SABABU WATEJA WANAWEZA KUACHA KUPELEKA MALALAMIKO SEHEMU HUSIKA WAKAYALETA KWENYE HUU UZI WAKITEGEMEA ZITAWAFIKIA DAWASCO/DAWASA NA KUFANYIWA KAZI WAKATI HAYAFIKI SEHEMU HUSIKA NA KWA WAKATI. MATOKEO YAKE MPAKA TAARIFA ZIFIKE SEHEMU HUSIKA INAWEZEKANA KAMA NI MADHARA YAMETOKEA MAHALI YANAWEZA KUWA HAYAWEZI KUREKEBISHIKA TENA.

MWISHO NAMSHAURI MHESHIMIWA LUHEMEJA ATUSAIDIE WANANCHI WA DAR TUPELEKE WAPI KERO ZETU KWANI CUSTOMER CARE NUMBER HUWA ZINAIITA HATA SIKU NZIMA HAKUNA MPOKEAJI SIO ZA MAKAO MAKUU AU ZA HUKU TABATA. KWA MFANO SIKU CHACHE ZILIZOPITA KULIKUWA NA TAARIFA YA UHABA WA MAJI BAADA YA KUPASUKA BOMBA LINALOTOKA RUVU. LAKINI BAADA YA HAPO HAKUNA UPDATE NA WATU HATUNA MAJI WIKI SASA MABOMBA YAMEBAKIA MAPAMBO NA HATUJUI MAJI YANARUDI LINI.
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)

DAWASCO HUDUMA KWA WATEJA 0800110064
DAWASCO ILALA 0743 451879
DAWASCO KAWE 0743 451861
DAWASCO KIBAHA 0743 451875
DAWASCO KIMARA 0743 451865
DAWASCO KINONDONI 0743 451863
DAWASCO BAGAMOYO 0743 451877
DAWASCO MAGOMENI 0743 451862
DAWASCO TEGETA 0743 451881
DAWASCO TABATA 0743 451867
DAWASCO TEMEKE 0743 451866View attachment 721128

Dawasco eneo la kwa Msuguri maji yanavuja utafikiri mto watu wanayatumia kumwagilia miti na mboga. Kuweni makini
 
Napenda kutoa taarifa za kuhujumiwa kwa DAWASCO maeneo ya Mwananyamala Mchangani, mtaa wa Juhudi.

Mimi ni raia mwema nimeamua kutoa taarifa kwa mamlaka zinazohusika kuhusu kijana maarufu kwa jina la Mudi Chavi ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa akijishughurisha na uuzaji maji maeneo ya Mwananyamala Mchangani mtaa wa Juhudi.

MBINU ANAZOTUMIA KUJIPATIA MAJI.

Amekuwa akiihujumu DAWASCO kwa muda mrefu sana. Na mbinu anazotumia kujipatia maji ni kukata mipira ya maji ntakati za usiku na kuunganisha kwenye mipira yake ambayo inakwenda kujaza matank ya maji anayomiliki na baadae kuuza kwa wananchi.

HASARA ANAZOSABABISHA.

Licha ya kuwa anaharibu miundombinu ya DAWASCO lakini pia amekuwa akichangia upotevu mkubwa wa maji, kwani mara nyingi anapokuwa amekata mipira hushindwa kuifunga na kuacha maji yakitiririka muda mrefu sana all night long. Maji nyakati za usiku huwa na presha kubwa kitu ambacho kinamuwia vigumu kurejeshea mpira anaokuwa ameukata. Mpaka naandika taarifa hii leo asubuhi wakati naenda mihangaukoni nimekutana na madimbwi makubwa ya maji huku moja ya mpira ukiwa unatirirsha maji kwa kasi ya ajabu. Ninaposema madimbwi naomba nieleweke ni madimbwi kweli kweli just like public swimming pool.

MAJI YANAYOPOTEA KIMAHESABU.

Ndugu zangu ipo hivi, kwa presha ya maji nyakati za usiku makadirio ya haraka kwa mipira hii midogo ya kawaida inaweza ikatiririsha lita moja za maji kwa kila sekunde, maana yake hapa ni kwamba kila anapoacha mipira ikimwaga maji usiku hupoteza lita sitini (60) kwa kwa kila dakika moja, ni lita 3600 kwa kila saa moja, ni lita 18,000 kwa saa tano kutoka saa tisa usiku mpaka saa moja asubuhi pale wasamalia wema wanapoamua kufunga mpira wanapokuta inamwagika. Ndugu zangu ni lita 90,000 kama kitendo hicho kitatokea mara tano kwa wiki.

Unaweza ukaona ni kiasi gani cha maji kinaweza kupotezwa na huyu mtu mmoja pekee, na kama wapo watu mia moja wanaofanya vitendo hivi wanauwezo wa kupoteza lita 9,000,000 za maji kwa siku tano tu za wiki ambazo ni sawa na lita 36,000,000 za maji ndani ya siku ishirini za mwezi.

Ndugu zangu hakuna asiyejua jutihada zilizofanywa na serikali ya awamu ya tano katika upande wa maji na maeneo mengine. Pamoja na jitihada zote hizi zinazoongozwa na muheshimiwa rais Magufuli bado wanatokea watu wachache kuhujumu jitihada zote hizi. Kinachotokea hapa ni kuwa maji yanayotarajiwa yawafikie wananchi hayafiki tena, yanakuwa machache, uhaba wa maji unatokea katika vyanzo vya maji na maji kukatika katika kila wakati.

Ndugu zangu uzalendo ni pamoja na kuwa kama watch dog kuangalia mahala popote ambapo nchi inahujumiwa huu ndiyo uzalendo, uzalendo ni kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumiwa ipasavyo na kuripoti vitendo vya hujuma kama hivi.

Muheshimiwa rais anahangaika kila siku kutuletea maendeleo badala yake wanatokea wachache kama hawa kutukwamisha.

Napenda kuomba mamlaka husika zifuatilie swala hili na wahusika wachukuliwe hatua kali ili iwe fundisho kwa wote wenye vitendo vya namna hii.

Naomba kuwasilisha,

Ni mimi mtanzania mzalendo ninaeipenda nchi yangu.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom