DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Leo ndio nimejua wizi wenu nyie jamaa
Nina mita 2
1 imetumia unit 8 inadaiwa 20elfu
2 imetumia unit 24 inadaiwa 40elfu

Unit 1 mnauza Shilingi ngapi???
 
Leo ndio nimejua wizi wenu nyie jamaa
Nina mita 2
1 imetumia unit 8 inadaiwa 20elfu
2 imetumia unit 24 inadaiwa 40elfu

Unit 1 mnauza Shilingi ngapi???
....watakujibu basii !? Anae'endesha hii account yumo kwenye likizo ya uzazi.
 
Huku Kimara tunakereka sana kuhuhusu huduma ya maji na sijui kama wahusika wanalifahamu hill.
Sasa nj wiki takribani mbili hatupati maji, tunateseka tunapata shida kupata maji...!
Tunaomba mtusaidie kuhusu hiyi shida maana haiwezekani tunalipa bili halafu maji hayatoki.
Fanyeni hima kabla hatujafikisha kero hizi sehemu husika!!!
 
Mbezi madukani maeneo ya msikitini jabal nur hatuna maji na kila tukija ofisini kwenu mnatuambia mtaleta lakin hakuna lolote maji wanapata wenzetu tu kwann mnatutesa
 
Dawasco/Dawasa Maeneo ya mwenge mmekuwa na tabia ya kukata maji kwa siku tatu mfululizo bila taarifa yoyote,na hii inatokea every week, tatizo ni nn?
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)

DAWASCO HUDUMA KWA WATEJA 0800110064
DAWASCO ILALA 0743 451879
DAWASCO KAWE 0743 451861
DAWASCO KIBAHA 0743 451875
DAWASCO KIMARA 0743 451865
DAWASCO KINONDONI 0743 451863
DAWASCO BAGAMOYO 0743 451877
DAWASCO MAGOMENI 0743 451862
DAWASCO TEGETA 0743 451881
DAWASCO TABATA 0743 451867
DAWASCO TEMEKE 0743 451866View attachment 721128
Ununio mnara wa Tigo hatuna maji siku ya 4 leo tatizo ni nini? Sisi tunahudumiwa na ofisi ya Boko!
 
Nyie dawasco mnafanya kazi kwa mazoea sana, mm nilibambikiwa bili ya 1.6 mil mwaka jana Nov lkn mpaka leo Nov 2018 nafuatilia warekebishe hakuna linalofanyika ni ahadi tuu mara kesho. Nawaambia kuna watu hapo mtapoteza ajira nikiamua kwenda kwa waziri. Account yangu ni 900343431, rekebisheni kabla sijakasirika zaidi. Luhemeja aone hii!
 
MM bado nataka kufahamu hapa kwetu mbezi madukani msikitini njia ya makabe maji tutaunganishiwa lini bomba kubwa limepita zaidi ya mwaka sasa hakuna maji tunasikia kwa wenzetu tu wa mshikamano kontena GR na kwa mzungu
 
Mnajisikiaje mko maofisini huku maeneo mengi ya jiji hasa wilaya ya Ilala na Temeke hakuna miundo mbinu yenu tokea uhuru?
 
Mimi nakaa mbweni. Tatizo langu ni kwamba huku kwetu tunapata maji machafu (kama ya mtaroni) kila siku. Huku haipiti siku 2 hujamwaga ndoo tatu hadi 5 kisa maji machafu.

Hii imetokea muda mrefu. Kulikoni?
 
NI LINI MTASAMBAZA MAJI MAENEO YA KUANZIA MBEZI MWISHO KUPITIA BARABARA YA MALAMBA MAWILI MPAKA KINYEREZI, TUNAPATA SHIDA SANA JAMANI TUNANUNUA MAJI KWA BEI GHARI SANA NA SOMETIME WAUZAJI WANATUUZIA MAJI MACHAFU NA YENYE CHUMVI KILIO CHET MTAKIMALIZA LINI. MAANA TUNASIKIA TU MNA MAJI MENGI SASA HIVI LAKINI HAMTUSAMBAZII
 
Dawasco kibaha kuna wakazi wa miembe saba kitongoji kinaitwa ngungwa tumeomba maji huu ni mwaka wa tano. tunaomba kujua shida ni nini. mnawapa ujiko viongozi wa mtaa kuombea kura au kuna makubaliano yenu na wao. Na uchaguzi wa serikali za mitaa ni mwakani watakuja kuomba kura tena kutumia huo mradi. Hebu tusaidieni kujua shida ipo wapi
 
Pamoja na kuharakisha mradi wa upanuzi wa huduma za maji katika maeneo ya GOBa, tunaomba menejimenti iutupie macho uratibu wa mgao wa maji kupitia viosk na nyumba chache zilizounganishwa. inaonekana kuna kamchezo.
 
Dawasco
Mbezi Juu barabara ya kwenda St Marr’s wiki ya pili sasa maji hayatoki ndani tunachota barabarani kwny bomba lililopasuka tena kwa kujificha/Mmefunga mabomba mapya mpk leo hamjayaunganisha sijui sisi tuishije ili hali mnajua wengi wetu tunatumia vyoo vya ndani ambavyo vinahitaji usafi wa maji mengi
 
Pongezi kwa serikali kufuta ada ya huduma a.k.a service charge, hii itapunguza bei za Ankara za maji na kumnufaisha mwananchi. Kweli awamu ya tano imedhamiria kuboresha huduma kwa gharama nafuu, Elimu bure, tutafikia maji bure na umeme Bure, Tubane zaidi mianya ya kodi
 
Mnajisikiaje mko maofisini huku maeneo mengi ya jiji hasa wilaya ya Ilala na Temeke hakuna miundo mbinu yenu tokea uhuru?
...wanashinda jamii forum na insta, wanafuatilia issue ya ambaruti !
 
Nyie dawasco mnafanya kazi kwa mazoea sana, mm nilibambikiwa bili ya 1.6 mil mwaka jana Nov lkn mpaka leo Nov 2018 nafuatilia warekebishe hakuna linalofanyika ni ahadi tuu mara kesho. Nawaambia kuna watu hapo mtapoteza ajira nikiamua kwenda kwa waziri. Account yangu ni 900343431, rekebisheni kabla sijakasirika zaidi. Luhemeja aone hii!
...walime memo ya mwanasheria wako, kisha ibaki kama ushahidi wako.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom