DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Kwanza niwape pongezi kwa kutengeneze hii thread ili muweze kuwasikiliza na kuwa karibu wateja wenu..Nina viwanja vyangu maeneo ya Goba...ila nimekuwa nikisita kuyaendeleza kutokana na kutokuwa na uhakika wa maji ya Dawasco. Katika maeneo yenye shida ya maji kwa Dar Goba ni eneo mojawapo. Mna mpango gani wa karibu na wa muda mrefu kusupply maji ya bomba kwa wakazi wa maeneo hayo
 
ndugu mteja mbona bili nyingine mnalipa kwa wakati ?kwanini bili ya Maji inakuwa na malalamiko mengi. tafadhali kama unatumia Maji jitahidi kuyalipia kwa wakati. Maji ni uhai

Bili zote zinalipwa kwa wakati Mwisho wa Mwezi. Hasa kwa wafanyabiashara wakubwa. Ni usumbufu sana uende bank katikati ya Mwezi kulipia bili ya maji na mwisho wa mwezi uende tena. Infact kwa majengo yaliyomjini watu hatuna jinsi inabidi tukubali ila kwa nje ya Mji mnapoteza wateja wengi sana.

Kama kweli mnataka kufanya biashara ya Maji serious msijifikirie nyinyi tu na lengo lenu la kukusanya Mapato au ku meet target.

Jaribuni kuwafikiria pia na wateja wenu maana bila wao nyinyi hamtakuwepo.
 
huyo msomaji wa mita hasomi vizuri manake mita yangu sshv inasoma 5540 wao wameleta bili inasema kutoka 5446 mpk 5496 nimetumia unit 50 yani wanakisia tu hiyo hotel tu nadhani hawatumii Lita 1666!!
 
Bili zote zinalipwa kwa wakati Mwisho wa Mwezi. Hasa kwa wafanyabiashara wakubwa. Ni usumbufu sana uende bank katikati ya Mwezi kulipia bili ya maji na mwisho wa mwezi uende tena. Infact kwa majengo yaliyomjini watu hatuna jinsi inabidi tukubali ila kwa nje ya Mji mnapoteza wateja wengi sana.

Kama kweli mnataka kufanya biashara ya Maji serious msijifikirie nyinyi tu na lengo lenu la kukusanya Mapato au ku meet target.

Jaribuni kuwafikiria pia na wateja wenu maana bila wao nyinyi hamtakuwepo.
sio lazima kwenda kulipa bili bank. lipia sasa kupitia Mpesa..Tigopesa..Airtel Money popote ulipo
 
inamaana mm natumia kwa siku Lita 1666? nyumba ya kawaida ina tank la Lita 500 tu yenye familia mbili? mnk bili inaonesha nimetumia unit 50
matumizi yako ndio yanayoakisiwa kwenye mita zetu. angalia upya matumizi yako na familia yako hususani yale yasiyo ya lazima kama kunyeshea bustani kila siku..kuflash choo kila wakati...uoshaji wa gari...na mengine mengi.
 
lita 1000
Safi, naomba muendelee na huu ushirikiano nasi, maana kuna mida huwa mnatukimbia tukiwauliza maswali!
Big up!
Mimi nina swali la ziada, ni mgeni ktk mita zenu, nilikuwaga natumia kisima cha pump sasa hivi niko dawasco, kuhusu hizi mita, unit ndo zile namba 1,2,3,4 ambazo hubadilika taratibu kadri unavyotumia maji? Nimeuliza hivi ili kuwa rahisi kwangu kujua bili nayotakiwa kulipa kwa kuisoma mita, au mita zenu hizi mpya ndogo nazisomaje kujua unit nilizotumia??
 
tutajie eneo husika. maelezo yako bado hayajajitosheleza
habari, mimi ni mteja wenu nipo wazo hill, nimeunganishiwa maji tokea mwaka jana ila sijawahi kutumiwa bili, nimejaribu kufuatilia dawasco ofisi za boko wakasema niwape meter namba nikafanya ivo ila hadi leo hamna kilichofanyika, sasa sielewi lengo lenu ni nini!
 
sio lazima kwenda kulipa bili bank. lipia sasa kupitia Mpesa..Tigopesa..Airtel Money popote ulipo
linapokuja swala la wafanyabiashara wakubwa zikiwemo ofisi kubwa mfumo wa malipo uboreshwe kuwa tofauti, ikiwa ninalipa kwa check inabidi niletewe bill yangu ya maandishi siku 14 kabla ili niweze ku-process malipo ktk utaratibu mzuri, utaratibu wenu mnatuma msg kitu ambacho si kithibitisho kizuri. nashauri utaratibu wa msg ufanyike kwa wateja wadogo wadogo.
 
matumizi yako ndio yanayoakisiwa kwenye mita zetu. angalia upya matumizi yako na familia yako hususani yale yasiyo ya lazima kama kunyeshea bustani kila siku..kuflash choo kila wakati...uoshaji wa gari...na mengine mengi.
sina gari wala bustani istoshe mita yangu inasoma 5590 wao wanasema Mita yangu inasoma 5496 hii dalili tosha ya kuwa mita hazisomwi kabisa wanakisia tu wala sina leakege yyte kwny nyumba yangu
 
Hongereni sana Dawasco kwa huu uzi,mimi nlikua na maswali kadhaa ambayo kama tukipata majibu yake itasaidia sana.
1.Maeneo ya mbezi juu tuliwekewa mabomba kwenye mradi al maarufu kama mabomba ya wachina,ila tangu wayaweke hayo mabomba hayajawahi kutoa hata upepo,ila ni hapa jirani tuu maeneo ya Africana maji yapo mengi sana,ni kwa nini Dawasco wasiongeze pressure ya maji ili na sisi tuweze kupata huduma hii??

Asanteni.natumai tutapata majibu mubashara hapa jamvini.
 
habari, mimi ni mteja wenu nipo wazo hill, nimeunganishiwa maji tokea mwaka jana ila sijawahi kutumiwa bili, nimejaribu kufuatilia dawasco ofisi za boko wakasema niwape meter namba nikafanya ivo ila hadi leo hamna kilichofanyika, sasa sielewi lengo lenu ni nini!
tunaomba meter namba tukusaidie kukusajili. pole kwa usumbufu
 
linapokuja swala la wafanyabiashara wakubwa zikiwemo ofisi kubwa mfumo wa malipo uboreshwe kuwa tofauti, ikiwa ninalipa kwa check inabidi niletewe bill yangu ya maandishi siku 14 kabla ili niweze ku-process malipo ktk utaratibu mzuri, utaratibu wenu mnatuma msg kitu ambacho si kithibitisho kizuri. nashauri utaratibu wa msg ufanyike kwa wateja wadogo wadogo.
asante kwa ushauri, tutaufanyia kazi!
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)
Maji Taka yanatiririka Dar nzima, na nyie huwa mnakusanya malipo kwa huduma hiyo. Why, kwanini?
 
Back
Top Bottom