DAWASA na DAWASCO ziwajibike kuondoa kero ya maji

John Mnyika

JF-Expert Member
Jun 16, 2006
712
1,240
Pamoja na mafanikio ambayo yamepatikana kwa baadhi ya maeneo ambayo hapo awali yalikuwa hayatoki maji kuanza kupata maji; yamekuwepo pia malalamiko ikiwemo kupitia JF kuhusu kero ya maji katika maeneo kadhaa ya jimbo la Ubungo.

Naomba kuwajulisha hatua ambazo tumefikia kwenye ufuatiliaji kwa kuzingatia maamuzi ambayo tuliyafanya kwenye Kongamano la Maji Jimbo la Ubungo tarehe 31 Januari 2011 ambalo nimeambatanisha taarifa yake.
Kufuatia malalamiko hayo mwezi Juni 2011 nimeiandikia barua Kampuni ya Maji Safi na Maji taka Dar es salaam (DAWASCO) kuwataka kutoa maelezo kuhusu hatua ambazo wamezichukua katika kushughulikia matatizo ya upatikanaji wa maji katika kata mbalimbali za jimbo letu.

Nimedokeza kwamba iwapo DAWASCO haitatoa maelezo mapema nitaeleza hatua za kibunge ambazo nizichukua ili kuhakikisha kampuni hiyo inatimiza wajibu wa kushughulikia kero ya maji katika kata mbalimbali. Naomba pia kuchukua fursa hii kueleza hatua zingine ambazo tumezichukua kuhusiana na maeneo ambayo yanahudumiwa na DAWASCO:

Tarehe 19 Januari 2011 niliiandikia barua ofisi yako yenye kumbu. Na. OMU/ MJ/004/2011 kuwaalika DAWASCO kuja kushiriki na kutoa mada katika Kongamano la Maji Jimbo la Ubungo; hata hivyo hakuna mtendaji yoyote toka ofisi yako aliyefika kutimiza wajibu husika wala barua tajwa kujibiwa.

Tarehe 15 Machi 2011 niliandika tena barua kwa ofisi yako kuwasilisha Ripoti ya Kongamano husika na kutoa mwito kwa hatua kuchukuliwa; hata hivyo ofisi yako mpaka sasa haijaeleza hatua ambazo imechukua au walau kutambua kupokea ripoti husika.

Tarehe 27 Februari 2011 na tarehe 6 Machi 2011 nilifanya mikutano na wananchi katika kata ya Goba kuhusu maji; pamoja na kuwa mradi katika eneo hilo uko chini ya wananchi vielelezo vilitolewa vya malalamiko ya muda mrefu kutaka hatua kuchukuliwa na DAWASCO kuhusu uharibifu wa mita na pia mapendekezo ya kutaka huduma katika eneo husika kutolewa na DAWASCO moja kwa moja.

Tarehe 26 Machi 2011 nilifanya ziara kata Kata ya Makuburi katika Mitaa ya Makoka, Muongozo na Kibangu na kubaini kwamba wananchi wa maeneo husika wamekuwa na ukosefu wa maji kwa miezi kadhaa hata katika maeneo ambayo hapo awali yalikuwa yakipata maji na hivyo kutoa mwito kwa DAWASCO kuchukua hatua za haraka.

Tarehe 7 Mei 2011 nilifanya ziara kata ya Kimara na kubaini kwamba ujenzi wa visima katika mitaa iliyoanishwa na DAWASCO kwa mujibu wa ahadi ya Rais Kikwete ya tarehe 24 Mei 2010 haujakamilika kwa maeneo mengi.

Tarehe 8 Mei 2011 nilifanya ziara katika kata za Mbezi na kubaini upungufu mkubwa wa maji wakati kukiwa na upotevu wa maji katika maeneo ya Msigani.

Tarehe 22 Mei 2011 nilifanya ziara katika kata za Mabibo na Manzese na kubaini ukosefu wa maji katika maeneo ambayo yalikuwa yakipata maji awali ikiwemo upungufu wa maji katika magati ya DAWASCO.

Tarehe 29 Mei 2011 nilifanya ziara kata ya Saranga na kubaini malalamiko ya muda mrefu ya wananchi kuhusu kero ya maji ikiwemo kutokujulikana ama kutokufuatwa kwa ratiba ya mgawo wa maji.

Aidha katika kipindi husika nimepokea barua toka wateja na wananchi kuhusu maombi mbalimbali ambayo wameyawasilisha kwenu bila hatua stahiki kuchukuliwa au walau kupatiwa majibu kwa ukamilifu.Mathalani maombi ya kuunganishiwa maji ya wananchi wa eneo la Burula (katika barabara ya Kimara Suca kuelekea Golani- barua yao ya tarehe 9 Agosti 2010), Mbezi Msakuzi (Hatua za utekelezaji baada ya barua ya DAWASCO/WSP/187/Vol III/42 ya 25/03/2009; Wananchi wa Msigani kwa ajili ya Wakazi wa kwa Mjanja ( Barua ya S/M/MSG/KN/001/2011 ya tarehe 10/01/2011 ambayo ilieleza mapendekezo yao mahususi kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa na kuomba mkutano kati yao na DAWASCO ili kujadili maombi yao), Wananchi wa Malambamawili (kwa barua yao SM/MSG/MWL/KN/DWSC/02/2011 ya tarehe 3/2/2011).

Naelewa kwamba utatuzi wa kero ya maji katika Mkoa wa Dar es Salaam ikiwemo jimbo la Ubungo unahitaji hatua za muda mrefu, muda wa kati na muda mfupi. Hata hivyo, zipo hatua ambazo zingeweza kuchukuliwa kwa haraka kuhusu mapendekezo yaliyotolewa na wananchi katika Kongamano na pia maombi ambayo yamewasilishwa DAWASCO bila kupatiwa majibu yoyote.

Nataka kupatiwa maelezo kuhusu shughuli ambazo zimetekelezwa na DAWASCO katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari 2011 mpaka Mei 2011 katika kuboresha upatikanaji wa maji kwenye maeneo mbalimbali ya jimbo la Ubungo ikiwemo kuelezwa hatua mahususi ambazo zimechukuliwa kufuatia ripoti ya Kongamano na barua za wananchi.

Huu ni ufuatiliaji katika maeneo ambayo yanahusu wajibu wa DAWASCO; hata hivyo zipo hatua ambazo nimezifanya za kufuatilia mamlaka mengine mathalani Wizara ya Maji (ikiwemo kupitia bunge), na Manispaa ya Kinondoni (ikiwemo kupitia kamati/baraza la madiwani) na wadau wengine mathalani miradi ya washirika wa kimaendeleo na sekta binafsi kwa ajili ya kuchangia katika visima na mtandao wa mabomba ya maji.

Mafanikio yaliyopatikana kutokana na ufuatiliaji na usimamizi huo ikiwemo nitayaeleza katika taarifa za baadae ikiwemo suala la upanuzi wa miundombinu kwa ajili ya kupata suluhisho la kudumu zaidi.

Kwa ujumla pamoja na kuwa zipo hatua ambazo zimefanyika katika kupunguza kero ya maji katika maeneo kadhaa ya Jimbo la Ubungo kufuatia Kongamano la Maji ; bado hali kwa ujumla wake hairidhishi suala ambalo limemfanya nitake maelezo ya kina kutoka DAWASA/DAWASCO kama sehemu ya kutimiza wajibu wa kuisimamia serikali na vyombo vyake.

Naelewa pia jitihada tunazozifanya zinapaswa kuambatana na hatua za kufanyika kwa ukaguzi maalum wa kifedha na kiufanisi wa DAWASA/DAWASCO kufanywa ili kushughulikia tuhuma za ufisadi, udhaifu wa kiutawala, kukithiri kwa upotevu wa maji na mapungufu mengine yanayokwamisha upatikanaji wa maji kwa wananchi wa Jimbo la Ubungo na mkoa wa Dar es salaam kwa ujumla.

Wenu katika utumishi wa umma,

John Mnyika (Mb)
 

Attachments

  • Ripoti Kongamano la Maji 2011, Ubungo[1].pdf
    544.1 KB · Views: 136

Naelewa pia jitihada tunazozifanya zinapaswa kuambatana na hatua za kufanyika kwa ukaguzi maalum wa kifedha na kiufanisi wa DAWASA/DAWASCO kufanywa ili kushughulikia tuhuma za ufisadi, udhaifu wa kiutawala, kukithiri kwa upotevu wa maji na mapungufu mengine yanayokwamisha upatikanaji wa maji kwa wananchi wa Jimbo la Ubungo na mkoa wa Dar es salaam kwa ujumla.

Tunakushukuru Mb kwa jitihada zako, umefanya kazi kubwa sana. kwa kweli suala la upotevu wa maji kwa Dar nzima ni tatizo kubwa. hii inahusiana pia na mpangilio mbovu wa mitaa ambayo inasababisha kukosa sehemu maalumu (ROW) kwa ajiri ya kupitisha mabomba.
mabomba yaliyowekwa tayari hayana ramani (mpangilio unaojulikana) hivyo kukatwa ovyo na wanaokarabati barabara au wanaojenga nyumba.
DAWASCO wanahusishwa na uuzaji wa maji kwa kutumia magari katika mitaa mingi ikiwemo mitaa ya jimbo la Ubungo. hivyo hawapendi maji yatoke katika mitaa hiyo. tunaomba Mbunge usichoke uendelee kupambana nao
Suala la mipango miji kwa Dar - kwanini kwenye makazi mapya bado kuna ujenzi wa kiholela?
kumekuwa na miradi mingi pia NGOs wanaosaidia ku upgrade mitaa ya zamani isiyo na mpangilio (kama Hananasif) lakini kitu cha kushangaza kwa nini halmashauri zinaruhusu watu waendelee kujenga kiholela? ukipita mitaa ya kimara ukiingia kwa ndani huko utashangaa sana, ni vyema suala hili likafanyiwa kazi
 
Dawasco/Dawasa ni wazembe na wanafanya makusudi.No accountability at all.Na ufisadi umezidi hasa DAWASA...Hizo pesa za miradi kutoka WB wanapata sijui zinafanya kazi gani...
 
Dawasa wamekodisha miundombinu ya kusambaza maji kwa Dawasco, kodi ya ukodishaji wanazolipwa Dawasa kutoka Dawasco zingetumika kuendeleza mitambo ya kusukuma maji, tatizo la maji kwa baadhi ya maeneo yangepungua.

Mh. Nnyika huoni kuna kila sababu ya kupeleka mswada Bungeni kuomba kuvunjwa kwa Dawasa, shirika lisilokuwa na tija yeyote kwa maendeleo ya maji mikoa ya Pwani na Dar es Salaam.
 
katika hili naona hawa jamaa wanataka kutuzoelesha kuwa maji ni mgao na lazima kutokua na maji kila siku.
My take: nyinyi viongozi toeni muda na kama hakutakuwa na kinachoendelea ni bora tuchimbe visima na tuondokane na hii adha..
 
Hongera sana MP kwa jitihada zako za ufuatiliaji wa mambo mbalimbali katika jamii yetu! Umeonyesha njia na kama watanzania hatuna budi kukupongeza. Tatizo letu hasa katika mashirika ya umma ni uwajibikaji hasa kuanzia juu, kwa mfano Kama baba ndani ya nyumba hawajibiki ni rahisi hata kwa familia yake kutowajibika, uwajibikaji lazima uanzie juu ili kuonyesha mfano mzuri ngazi ya chini! Baadhi ya viongozi wetu wengi hawana nia nzuri ya kusimamia rasilimali za nchi. mfano mzuri ni yale mabomba ya mchina yaliyotandikwa kwa mbwembwe nyingi sana wakitupa matumaini ya maji kutoka lakini cha kushangaza mabomba hayatoi maji na yalitumia fedha za mlipa kodi lakini hayafanyi kazi.(Maeneo ya Msingwa jimbo la Ubungo) Rasilimali za umma zinateketea kwa viongozi kutokuwa na dhamira safi wakati wa utekelezaji wa miradi mingi. Hii inauma sana ukizingatia tunalipa kodi ili itumike katika maendeleo ya taifa. Nyie mnaojali matumbo yanu hebu badilikeni na mfanye kazi kwa uadilifu na kuzingatia miiko ya kazi zenu.
 
Back
Top Bottom