Bukyanagandi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2009
- 11,061
- 16,743
Si ndio hapo mkuu, yaani Watanzania tumekubuhu in manufacturing lame excuses - hatikosi sababu - siasa tu 24X7, MTU ungetegemea kwamba Wizara yenyewe ingekuwa na kitengo maalumu cha kukaguwa main water pipes for illogical connections, vile vile na kubaini wanao chepusha vyanzo vya maji, hizi tabia za kufanya mambo wakati wa crisis kama za zima moto mpaka lini?... cheap politics; hayo mabwawa 26 ya kufugia samaki yana-consume kiasi gani cha maji? Put facts on the table badala ya siasa!
Mara oooh, tumemkamata Mchina anayelima mboga mboga tumekuta alikuwa anapampu maji mengi kwenye mradi wake usiku wa manane, akatozwa faini ya million sijui tatu na nusu bila ya kumfikisha kwenye vyombo vya Dola, vifaa vyake vikataifishwa, lakini cha ajabu kesho yake wakakuta Mchina kanunua mitambo mingine na kuendelea na mradi wake kama kawa - hana wasi hata kidogo, cha kujiuliza hapa ni,je, Mchina huyo jeuri hiyo anaipata wapi,je, huko kwao Uchina anaweza kufanya hujuma kama hizo akaendelea kupeta tu!! Haya tuje kwenye mabwa makubwa ya kufugia samaki, kwani si yanaonekana tu hata ukiwa ofisi kwako kwa kutumia Google Earth kupitia kwenye Computer au smart phone - tatizo LA wengi wetu hatuna ubunifu hata kidogo na hatujui jinsi kujituma na kuwajibika.