DAWASA: Matengenezo ya bomba la Maji yanaendelea, huduma kurejea baada ya kumaliza

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
DAWASA YAWAHAKIKISHIA WAKAZI HUDUMA BAADA YA MATENGENEZO

Na Crispin Gerald

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Dar es Salaam (DAWASA) imewahakikishia wananchi wanaohudumiwa na Mtambo wa Ruvu chini kuwa huduma ya maji itarejea ndani ya muda uliopangwa kufuatia matengenezo ya bomba kubwa la inch 54 lililopo eneo la Mlalakuwa, Mwenge kuendelea kutengenezwa kwa kasi inayoridhisha.

Akielezea juu ya matengenezo hayo Meneja Uzalishaji na Usambazaji wa maji, DAWASA Mhandisi Tyson Mkindi amesema mafundi wanaendelea na matengenezo ambayo kwa sasa yamefikia asilimia 60, na kwamba huduma ya maji itarejea ndani ya muda uliopangwa na Mamlaka.

"Kazi inaendelea baada ya kuanza tangu saa mbili asubuhi na mpaka sasa (saa 10:13 asubuhi) tumefikia asilimia 60 ya utekelezaji, hivyo tunatarajia huduma kurejea kabla ya wakati tulioutegemea kwa kuwa hamna changamoto yoyote iliyojitokeza mpaka wakati wa utekelezaji," amesema Mhandisi Mkindi.

Naye mwenyekiti wa mtaa wa Mlalakuwa, Ndugu Suleiman Massare amesema kuwa wamejiridhisha na jitihada zinazofanywa na DAWASA katika eneo lake amewataka wakazi wa mtaa wake na waliathirika na matengenezo hayo kuwa na subira kwa kuwa matengenzo yanatarajiwa kukamilika leo jioni.

"Kazi inayoendelea hapa inatia moyo kuwa huduma itarejea ndani ya muda uliopangwa, hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi," amesema Ndugu Massare.

Matengenezo ya bomba kubwa la maji eneo la Mlalakuwa limepelekea kuzimwa kwa mtambo wa Ruvu chini na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma katika maeneo mengi ya Jiji la Dar es salaam kuanzia Mji wa Bagamoyo hadi katikati ya Jiji kwa maeneo ya Ilala hadi Kigamboni.

IMG-20220923-WA0004.jpg
IMG-20220923-WA0005.jpg
IMG-20220923-WA0006.jpg
IMG-20220923-WA0007.jpg
 
Hivi kwani hakunaga matank ya reserve ili wakiwa wanaendelea na huduma ya utengenezaji na urekebishaji maji yawe yanaendelea kutoka? Au bomba linalopaswa kutoa maji kwenye matanki ndo hilo linalorekebishwa? Na kama ndivyo,Je hakuna umuhimu wa kuwa na mabomba ya dharura?
 
Tunafunga maji ili tutengeneze......Kauli za kijima. No parallel link. No reservoir. Kama nchi, uwekezaji kwenye maji, afya, elimu, umeme na miundombinu mingine bado ni changamoto kubwa
 
Hii ni kazi yako wewe, nunua hayo matank kadhaa weka nyumbani kwako.
Hivi kwani hakunaga matank ya reserve ili wakiwa wanaendelea na huduma ya utengenezaji na urekebishaji maji yawe yanaendelea kutoka?au bomba linalopaswa kutoa maji kwenye matanki ndo hilo linalorekebishwa? Na kama ndivyo,Je hakuna umuhimu wa kuwa na mabomba ya dharura?
 
...Kila siku ' Wanatuhakikishia' lakini siku Tatu TU Baadae, tunarudi pale pale....
 
Jana mchana kazi ilikwisha fika asilimia 60. Hadi muda huu saa zaidi ya 36 baadaye maji Ilala hakuna. Tuliambiwa matengenezo ya siku moja.
Ama kweli, zilongwa mbali zitendwa mbali.
 
Jana mchana kazi ilikwisha fika asilimia 60. Hadi muda huu saa zaidi ya 36 baadaye maji Ilala hakuna. Tuliambiwa matengenezo ya siku moja.
Ama kweli, zilongwa mbali zitendwa mbali.
Umeandika nlichotaka kuandika.
Mimi hata sikuwa nafahamu maji yamekata maana mfumo wa maji wa hapa kwangu maji yanaingia kwenye tanm then ndo yanatoka kwenye tank kuingia kwenye nyumba.
Sasa hata maji yakikata nakuwa sina habari nimekuja kushtuka leo maji hayatoki ndani bahati nzuri ni kwanza kuna katank kadogo kana hifadhi ya maji pia.
Yani mpaka jana 60% ila 40% zilizobaki zinaweza chukua siku kadhaa. Kweli hii ndio TZ
 
Back
Top Bottom