DAWASA Kibaha mnaboa

luangalila

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
6,325
6,866
Imetia mwezi sasa tangu nipeleke maombi ya kuunganishiwa huduma ya maji katika pagalu langu lililopo Picha ya Ndege lakini hawa jamaa wa DAWASA hawajatuma hata surveyor.

Isitoshe unapotembelea pale ofisi kwenu wateja wengi hufika pale na malalamiko mbalimbali ya huduma mbovu mnazotoa, hamna good customer care kuanzia receptionists wenu mpaka Engineer wenu in short mna kauli mbovu na MNAKWAMISHA maendeleo ndani ya nchi.
 
Mkuu mapato wanayoingiza itakuwa yamewatosha.

Tafuta alternative nyingine kuwapata / kupata huduma tofauti na wao.
 
Kuna namba ninayo kwenye makabrasha yangu. Simu moja tu utamuona huyu surveyor akija kwa kibajaj na mafuta kaweka kwa hela zake.
Subiri ni isachi hiyo namba.
 
Kabla sijakupa hiyo namba hebu hii kitu iweke kwenye DAWASA special thread hapo juu na Mimi nitamstua LUBEMEJA aisome.
 
Kuna dogo aliniomba rushwa leo.
Ni msoma mita anaonekana mlevi mlevi hata viatu Hana anavaa ndala. Ngoja leo nisimharribie kazi
 
Mamlaka zinazohusika ziangazie DAWASA kibaha,niliwahi kufuatiliaji maji nikazungushwa
nikaomba kumuona meneja,katibu mhutasi akanidanganya kwamba meneja hayupo
kaenda kwenye kikao.
Mungu si athumani papo hapo wakaingia watu kutoka wizara ya afya
wanakagua mazingira ya utekelezaji wa mapambano dhidi ya korona,yule mama akaona kigugumizi
akiangalia ameishanidanganya kwamba meneja hayupo,na hawa wakubwa wanamtaka meneja
ikabidi aingie ofisini ampashe habari,wale wageni wakaruhusiwa kuingia. Mimi kuona hivyo na muda wangu ukikuwa mdogo
nikaondoka,ila nilisikitika kuona mama wa makamo anasema uongo mchana kweupe,na ni mtumishi wa umma.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom