Naomba kufahamishwa dawa zinazosaidia mfupa uliovunjika kuunga

Mandinga

Member
Mar 6, 2020
35
45
Wakuu naomba kwa anaefahamu dawa hasa za asili au zozote ambazo zinasaidia mfupa kuunga haraka. Kama hazipo pia naomba nijulishwe au kama kuna njia yoyote inayoweza kutumika kusaidia hili.

Nawasilisha.
 
Kwanini hutaki kwenda hospitali mkuu ukafuate taratibu za kitabibu ikiwa ni pop au antenna?
 
Kwanini hutaki kwenda hospitali mkuu ukafuate taratibu za kitabibu ikiwa ni pop au antenna?
Hosp nimeenda ila si unajua maisha yetu haya hela inaingia pale ukiwa mzima ila ukiumwa mambo yanakata...
 
Hosp nimeenda ila si unajua maisha yetu haya hela inaingia pale ukiwa mzima ila ukiumwa mambo yanakata...
Pole sana mkuu. Ushauri wangu, bora tumia nguvu kutafuta hela uende hospitali utapata tiba ya kudumu. Alafu ukipona utaendelea kuingiza hela kama mwanzo. Hizi short cut za kuunga mfupa kienyeji usije ishia kuoza mfupa mkuu, na biashara ikaishia hapo
 
Mfupa kuunga huwa unaunga, changamoto ni kuchelewa kuunga... Sasa endapo kuna dawa za kuharakisha hili ndio ninazohitaji mimi mkuu
Yes tafuta Dawa inaitwa CALCITRON kama upo dar Nenda Bariki pharmacy au RobbyOne pharmacy au Core pharmacy Utapata!! Ni calcium suppliment ina new technology that give Maximu absorpition ya calcium maana katika mfupa kujiunga tunahitaji calcium nyingi.

Hii ni dawa mpya mikoani bado haijaanza kusambaa, ni ya egypt nzuri sana.
 
Attachments

  • download.jpeg
    download.jpeg
    8.3 KB · Views: 162
Yes tafuta Dawa inaitwa CALCITRON kama upo dar Nenda Bariki pharmacy au RobbyOne pharmacy au Core pharmacy Utapata!! Ni calcium suppliment ina new technology that give Maximu absorpition..ni ya egypt nzuri sana
Nashukuru sana mkuu...
 
Pole sana mkuu. Ushauri wangu, bora tumia nguvu kutafuta hela uende hospitali utapata tiba ya kudumu. Alafu ukipona utaendelea kuingiza hela kama mwanzo. Hizi short cut za kuunga mfupa kienyeji usije ishia kuoza mfupa mkuu, na biashara ikaishia hapo
Kweli mkuu
 
Anatumia nguvu zipi kutafuta hela, na amekwambia amevunjika mfupa
Acha hizo
 
Anatumia nguvu zipi kutafuta hela, na amekwambia amevunjika mfupa
Acha hizo
Hivi kutumia nguvu kutafuta hela ni lazima kutembea na kulima? Hapa katumia nguvu zipi kuomba msaada wa tiba mbadala?

Hivi hapa wa kuacha hizo na kutumia akili ni mimi au wewe?

Wewe kwa akili yako mgando wale watu woooote unaowaona wanatibiwa hospitalini walitumia nguvu kwa kulima na kufanya kazi maofisini au viwandani kutafuta hela za matibabu? Anyway umeshajiita Mtukutu sioni haja kulumbana na wewe. Yeye mwenyewe alishanielewa ila wewe yasiyokuhusu umeshindwa kuelewa. Sio ishu kabisa.
 
Mwaka 2003 Kuna jamaa alivunjika mguu, katika kumpa huduma ya Kwanza akaja jamaa akamuunga, bahati mbaya akamuunga vibaya mguu ukawa Kama umepinda hivi af ukawa unachelewa kupona.

Ikabidi atafutwe mtalaam mwingine. Huyu mtalaamu mpya alipofika, akamchek mgonjwa, akamwambia mzee wake "Nirafutieni kamba imara.

Basi wakatafuta kamba, wakamfunga mgonjwa kwenye kitanda, wakafunga tu akawa comfortable yaani huku wanakula stori Kama kawa.

Basi yule mtalaam mpya, akampaka mgonjwa dawa ya miti shamba kwenye mguupale palipovunjika na kuungwa vibaya. Alipomaliza kumpaka wao (mtalaam, mzazi na watu wengine waliokuwepo wakaenda sebuleni wakaendelea na stori Kama kawaida, stori vicheko na Mambo mengine huku mgonjwa akiwa chumban amefungwa kamba na Yuko comfortable sana tu.

Baada ya Kama dakika 30, Punde si punde, mgonjwa alisikia PAAAAAAAAAAAAAH mguu umevunjika UPYA. Jamaa (mgonjwa) anakwambia siku ile ndo alisikia maumivu makali zaidi ya siku ile alipovunjika mara ya Kwanza.

Basi bwana, baada ya hapo ndo mtalaam akumuunga upya na jamaa alipona vizuri na baada ya muda alianza kucheza mpira Kama zaman tu.

Kuna wazee wanajua dawa bwana, sema kuna wapuuzi wachache wanafanya mitishamba ionekane mibaya
 
Mwaka 2003 Kuna jamaa alivunjika mguu, katika kumpa huduma ya Kwanza akaja jamaa akamuunga, bahati mbaya akamuunga vibaya mguu ukawa Kama umepinda hivi af ukawa unachelewa kupona.....
Sure mkuu... Na mm ndio nahangaika hivyo
 
Kanda ya ziwa wapo wataalam wengi, wanaunga kwa kutumia dawa fulani wala hawagusi kabisa sehemu ilipovunjika. Kuna jamaa tunafanya nae zoezi alivunjika mwaka juzi tukampeleka.

Aliungwa mwezi mmoja tu kawa mzima kabisa. Huyu mganga anatibu kuvunjika mifupa tu. Historia yake ni kwamba aliwahi kuvunjika mguu akaenda kuungwa kwa mzee fulani, baada ya kupona akamplekea yule mzee zawadi ya ng'ombe, mzee alifurahi akamfundisha dawa hiyo.

Kama upo tayar sema niulizie Kama huyo mtaalam bado yupo nitafute na Namba zake, nikupagie
Kuna mzee anaunga maeneo nilipo mkuu (sio mimi)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom