Dawa za mitishamba ya kichina zinafanya kazi kubwa katikautaratibu mpya wa matibabu ya ushirikiano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa za mitishamba ya kichina zinafanya kazi kubwa katikautaratibu mpya wa matibabu ya ushirikiano

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Dec 8, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,604
  Trophy Points: 280
  Dawa za mitishamba ya kichina zinafanya kazi kubwa katika utaratibu mpya wa matibabu ya ushirikiano vijijini
  [HR][/HR]
  [TABLE="width: 90%, align: center"]
  [TR]
  [TD="class: FontStyle5"]Hivi karibuni naibu waziri wa afya Bw. She Jing kwenye mkutano wa utekelezaji wa kazi ya majaribio ya utaratibu mpya wa matibabu ya ushirikiano vijijini na dawa za mitishamba ya kichina vijijini alisema kuwa, kutumia dawa za

  mitishamba ya kichina, hasa kutumia teknolojia mwafaka ya dawa za mitishamba ya kichina yenye bei nafuu, ambayo ufanisi wake ni mzuri na salama, kunaweza kupunguza gharama za matibabu kwa wakulima, na kutoa

  mchango katika kutatua tatizo la wakulima kuwa maskini kutokana na maradhi.
  Idara ya taifa ya usimamizi wa dawa za mitishamba ya kichina imegundua kuwa, katika sehemu nyingi za China hasa

  katika sehemu zenye watu wengi maskini gharama za dawa za mitishamba ya kichina zinazokubaliwa na wakulima kwa wastani ni Yuan za RMB 6 hadi 8, na gharama za zahanati kwa kila mtu kwa wastani ni ndogo kwa asilimia 20 hadi 30 kuliko dawa za magharibi. Kwenye mkutano huo Bw. She Jing alisema kuwa, bei nafuu za dawa za

  mitishamba ya kichina na matumizi ya teknolojia mwafaka ya dawa za mitishama ya kichina yamepunguza gharama za matibabu kwa wakulima wanaoshiriki kwenye matibabu ya ushirikiano, pia yamepunguza utoaji wa fedha za

  utaratibu mpya wa matibabu ya ushirikiano. Alisema hatua hii sio tu inakaribishwa sana na wakulima hao, bali pia inatiliwa maanani na serikali ya ngazi mbalimbali na sekta mbalimbali za jamii.

  Bw. She Jing amesema majaribio hayo yamethibitisha kwamba dawa za mitishamba ya kichina zinafanya kazi kubwa katika kazi ya majaribio ya utaratibu mpya wa matibabu ya ushirikiano, pia zina uwezo mkubwa, vilevile kazi ya majaribio imetoa fursa nzuri kwa kazi ya dawa za mitishamba ya kichina vijijini.
  Idhaa ya Kiswahili [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mkuu,
  Asaante kwa Thread hii.
  Je, wewe ni Dr?
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Dec 8, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,604
  Trophy Points: 280
  wewe Shida yako kutaka kujua mimi Dr? au una matatizo eleza hapa utasaidiwa upo na mimi?
   
Loading...