Dawa za Mapenzi..(Shuntama; Mwoshe; Limbwata... n.k.) Wizi Mtupu au Changa la Macho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa za Mapenzi..(Shuntama; Mwoshe; Limbwata... n.k.) Wizi Mtupu au Changa la Macho

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by VoiceOfReason, Jun 24, 2011.

 1. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Kwanini Watu hawaamini kuwa mtu anaweza kupenda kupita kiasi hadi wanadhani kwamba amelogwa...??

  Kwanini watu wakiachwa na wapenzi wao wanakimbilia kwa waganga...?, nadhani ingekuwa bora wangemfata yule aliyawaibia mpenzi wao kwa tuition au wapeleleze ni nini anachompatia ambacho wenyewe hawakumpatia (maujanja)

  Hivi kuna mwanajamii yoyote humu anayeamini hii issue (au ambae ameshaona hii kitu imefanya kazi...?) Binafsi nadhani hakuna dawa zaidi ya upendo na taking care of your partner..,

  Kwa wale wanaojua hii kitu na wana uhakika kwamba inafanya kazi naomba tujuzane ili tui-package vizuri na kuifanyia promotion na marketing ya nguvu na kuiuza nchini pote na kwa wanandoa wote nadhani tutasaidia jamii kwa kupunguza Divorces, na sisi kujitengenezea kipato cha uhakika.

  Jamani tuache kuibiwa pesa zetu na kulishana visivyolika.....
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  hakuna dawa ya mapenzi
  but watu wanapotafuta alternative way sio kwamba wanatafuta dawa ya mapenzi....
  dini zote zinatufundisha vitu kama mikosi.laana,bahati,baraka na kadhalika

  sasa sometimes watu wakiachwa huhisi kuna mkosi hivi..
  kwa hiyo wanachojaribu kukifanya ni kutafuta dawa za mkosi au kuondoa laana hivi na sio dawa za mapenzi
  hii huwatokea sana wanawake.....
   
 3. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo mkuu kuna dawa za kuondoa mikosi au laana
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  sijasema kuna dawa
  ninachosema wanachokifanya kutokana na imani
  tunazozikuta kwenye jamiii
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  labda nikuulize
  wewe unaamini kwenye baraka,mikosi,laana, na kadhalika????????

  unaweza mtukana au kumpiga mzazi wako
  bila ku feel kuna laana utaipata????????

  ukiambiwa kuna nyumba ina mashetani
  unaweza kwenda kuishi??????????
   
 6. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mimi ninaamini kwamba IMANI ni jambo kubwa sana ambalo linampa mtu confidence ambayo bila kuwa nayo ni vigumu kufanikiwa. Kwahiyo mfano kwenye michezo mtu akiamini kwamba wameloga.., ile confidence itamfanya apeform zaidi akiwa na imani kuna nguvu inamsaidia (mfano mzuri vita vya maji maji) mababu zetu ile fikra kwamba risasi zitageuka maji iliwafanya wapigane ambavyo huenda wangekimbia...

  Kutukana mzazi wako huku unaamini kuwa laana itakupata (ni kweli itakupata) sababu utakuwa umepunguza confidence yako na kila jambo baya likikutokea utaamini ni sababu ya laana (ila ukiwa chizi ambaye haamini laana huenda isikupate)

  Inategemea kuhusu nyumba huenda kuishi kwangu pale kukanipunguzia confidence na nikaanza kuhusisha matatizo ya kila siku ya kawaida na hayo mashetani.., au upepo wa kawaida kama ndio shetani.., na hii huenda ikanipunguzia usingizi wangu mnono

  Kwahiyo naona hizi dawa za mapenzi tunaweza kuziita Confidence Booster
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  usiombe yakukute...
   
 8. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Dawa ya mapenzi akili yako tu!..
   
 9. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Yapi Mkuu...., sisemi kwamba majanga mabaya hayapo.., lakini nachosema hayo mabaya yanatokea sababu ya supernatural powers au ni share ya bahati mbaya kwa kila binadamu..., Alafu issue ya kwamba fulani ana mikosi je ni sababu ya ushetani fulani au ni sababu ya mambo fulani anayoyafanya yanapelekea hiyo mikosi...

  I really believe sometimes tunakaribisha wenyewe mikosi kwa matendo yetu..., na kila mtu ana fair share ya mazuri na mabaya
   
 10. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  kuna kitu inaitwa GENDA UGARUKE,
  hiyo ukienda lazima urudii,
   
 11. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mkuu usiwe mchoyo tupe ingredients... ili tuweze kuifanyia package nzuri na kuwauzia wanandoa...,
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,548
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  Mie siamini kabisa kama kuna dawa ya mapenzi. Ila naamini kwamba unaweza kumpenda mtu kupitiliza na hii inasababishwa na vitu mbali mbali kama vile jinsi anavyokujali, kukuheshimu, kukuonyesha mapenzi ya hali ya juu kila siku iendayo kwa Mungu n.k. Wale wasiaomini kwamba unaweza kumpenda mtu kupitiliza hadi uwe umerogwa sijui tuwaite vipi labda ndio wale wanaosema nampenda fulani kwa 55% au 60% sijui asilimia nyingine wanamuachia nani. Nasikia wabongo walioko Bongo na hata majuu wanasafiri hadi Nigeria eti kutafuta dawa ya mapenzi!! maana wanaona penzi limepungua!
   
 13. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Tena kuna Kabila fulani kule Congo (Zaire) kuna jamaa yangu wa Congo alikuwa ananiambia eti akienda kule akipewa chakula hawezi kula (akiamini kwamba akila chakula tu anaweza kulishwa kitu na kujikuta anasahau kwao)...
   
 14. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #14
  Jun 24, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Kama huamini nenda Kenya kwa Wakamba wakuonyeshe "KAMUTEE" inavyofanyakazi
   
 15. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #15
  Jun 24, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Ningependa kuamini sababu Elimu haina Mwisho ndio maana naomba mwanajamii mmoja anieleweshe vizuri na kama uwezekano upo tuweze kupata ingredient ili tuwape wanandoa ambao hawajatulia lakini shida ya hii kitu utawezaje kuhakikisha kwamba kweli ndio imefanya kazi..?
   
 16. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #16
  Jun 24, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Yap...thats all! Labda kuongeza tu kwa matendo na fikra zetu.Its all in our minds. Inajibu pia swali lako la hizo 'dawa'.
   
 17. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #17
  Jun 24, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Kha! Wewe unataka kuwapa wanandoa? Huwa unatoa ushauri kwao na unaona hawaelewi? Kamutee inafanyakazi nimeshuhudia
   
 18. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #18
  Jun 24, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Vipi unaweza ukaniongezea Data kidogo kwa sisi kina Tomaso..., na unajua Ingredients zake..., Kama ni kweli kwanini nisiwape wanandoa au hata mimi mwenyewe kujaribu na mwenza wangu pia..., huoni kwamba hii itasaidia matatizo mengi.? Je ina madhara yoyote?
   
 19. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #19
  Jun 24, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Umemaliza yote!
   
 20. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #20
  Jun 24, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135  Why not using part of that money to revive the love!
   
Loading...